Serikali yatoa tamko kuhusu polisi kupiga raia

Serikali yatoa tamko kuhusu polisi kupiga raia

Radiation

Platinum Member
Joined
May 28, 2013
Posts
331
Reaction score
293
Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.
“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.
Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheriaya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wakutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.
Aliyataja mazingira hayo kuwa ni pamoja na kuokoa uhai wa mtu mwingine, kuzuia madharamakubwa ya mwili yasitokee kwake au kwa mtu mwingine na kumzuia mtu anayetenda tendo ovula kubaka au kunajisi mtoto au kufanya vitendo kinyume na maumbile.
Pia kumzuia mtu anayevunja nyumba usiku au unyang’anyi wa kutumia silaha au kuchoma nyumba moto aukufanya kitendo chochote kinachohatarisha uhai wa mtu au mali.
Alieleza kuwa Kifungu cha18 na 18(A) cha Sheria yaAdhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda maliyake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.
Kauli hiyo ya Serikali kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi, ilitolewa ikiwa ni ufafanuzi wa jibu la swali la nyongeza lililoulizwa bungeni Mei 28,2013 na Rashir Ally Abdalah (Tumbe-CUF), ambapo Silima alisema mauaji yanayofanywa na askari polisi ni mauaji ya kisheria.Kutokana na kauli hiyo, Mbunge wa Wawi, HamadRashi Mohammed aliombamwongozo wa spika kupata ufafanuzi wa kauli hiyo, na jana Silima kutoa kauli ya Serikali kujibu mwongozo huo.
“Ikumbukwe pia kuwa, kifungu cha 29 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi Sura322, pamoja na Kanuni za Kudumu za Utendaji za Jeshi la Polisi Na274, vinampa haki ya kisheria askari polisi kubeba na kutumia silaha za moto ikiwamo bunduki na mabomu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku..,”alisemaSilima.
Alifafanua kwamba katika kutafsiri sheria, kanuni na taratibu mbalimbali ikiwamo alizozitaja, mahakama katika nyakati tofauti imetoa msimamo wa kisheria juu ya suala hilo.
Akitoa mfano alisema: “Mathalan katika kesi ya Seif Mohamed Senzagala dhidi ya Jamhuri ya mwaka 1994 kama ilivyonukuliwa na TanzaniaLaw Report ukurasa wa 122, ambapo mshitakiwa (mwomba rufaa) alimjeruhi kwa panga mlalamikaji ambaye alimfuata nyumbani kwakena kuanza kumshambulia.”
Alisema katika kesi hiyo,mahakama ya rufaa pamoja na kuridhia uamuziwa mahakama ya awali wa kumtia hatiani kwa kutumia nguvu kupita kiasi,ilibainisha kuwa mshtakiwa hakustahili adhabu kwani alitenda kosa lile wakati akijihami dhidi ya mashambulizi toka kwa mlalamikaji.
 
sasa tamko la nini wakati pinda keshasema '"…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa"
 
Katika historia ya serikali zilizowahi kutawala nchi ulimwenguni, serikali ya CCM ndo serikali ya kipuuzi na bure kabisa hakujapata kupatikana mfano wake na wala hapatatokea labda wao wenyewe wavunje record yao.
 
tuyajadili haya katika katiba mpya. Sheria shoga kama hizi zitatufikisha pabaya sana.........
POLISI hawahawa wezi wa mali za raia,mara ngapi 2mesikia polisi wamepora mali za raia,,2kumbuke wale wafanyabiashara wa sinza walouwawa na askali ili waibiwe mali zao katika msitu wa polisi uitwao mabwepande....na kariakoo je.........
kwa sheria za kijinga kama hizi zinazowapa mamlaka watu wa akili ndogo kama askali wetu na viongozi wasioweza kuzuia hisia zao kama PINDA....ni ishara mbaya sana kwa inchi inayoitwa ya kidemokrasia kama yetu sisi.....
KATIBA MPYA ITUONDOLEE UCHAFU HUU..................
 
Kwani kuna serikali ngapi Tanzania? na Pinda alipokuwa anatamka kuwa wapigwe alikuwa anawakilisha serikali gani!??
 
Ukweli wote juu ya sual hili umeelezwa vizuri sana na Mtu wa Shamba kwenye bandiko lake hili hapa;
[h=1]Polisi na vyama vya Upinzani. Je Polisi wako Juu ya Sheria?[/h]
1. Utangulizi
Jeshi la Polisi ni chombo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoundwa ili kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu.

2. Lengo la Jeshi la Polisi:
Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu. Jeshi la Polisi lipo kama sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa kila mtu, wakiwemo askari polisi wanafuata sheria katika kila hatua.

3. Majukumu ya Jeshi la Polisi:
Jeshi la polisi lina kazi kadhaa:

  1. Kuzuia na kudhibiti uhalifu.
  2. Kubaini na kuchunguza vizuri wakati wowote uhalifu unapotokea.
  3. Kutayarisha shauri la kweli na lenye ushahidi ili mwendesha mashtaka aweze kuwasiliana mahakamani.
  4. Kukusanya taarifa kuhusu matukio katika jamii ili kuweza kutimiza jukumu la kudumisha sheria na utilivu.

4 Sheria inayoongoza shuguli za Jeshi la Polisi:
Shughuli za jeshi la polisi zinaongozwa na sheria mbalimbali, lakini kwa kiasi kikubwa:

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
  2. Sheria ya Jeshi la Polisi namba 322 (Police and Auxiliary Services Act 2002 Cap 322).
  3. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  4. Kanuni za Polisi (Police General orders).
​
Kwa hiyo Jeshi la polisi lina mamlaka ya kisheria na linapaswa kutumia mamlaka hayo kulingana na taratibu zilizoainishwa katika sheria husika.

Polisi wanaweza kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi, kufanya mahojiano na mtuhumiwa, kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio vinginevyo. Polisi hawawezi kufanya wapendavyo.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Mfano mmojawapo ni matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na nguvu za polisi anapofanya uchunguzi
Sheria ya ushahidi inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Ushahidi wowote uliopatikana kwa kutumia nguvu, hauwezi kutumika kama ushahidi halali, ikibainika mahakamani kuwa ulipatikana kwa njia batili.
Sheria ya Polisi inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu mamlaka na kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi. Sheria hii inasisitiza polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.

Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu. Afisa wa polisi anayetenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki.

5. Gharama za Shughuli za Polisi
Shuguli zote za polisi zinalipwa na walipa kodi wa Tanzania.

Kila mwaka katika kikao cha bajeti, hutengwa fungu maalum kwa ajili ya uwezeshaji wa utoaji wa huduma za polisi katika jamii. Fedha hizi hupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni suala la muungano. Kitengo cha mipango cha jeshi la polisi huandaa mapendekezo ya bajeti, ambayo hupelekwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuridhia, kasha hupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tayari kwa kupelekwa bungeni. Wabunge hujadili na kupitisha bajeti ya polisi. Sehemu kubwa ya bajeti huenda kwenye mishahara. Matumizi mengine ni mafunzo, upelelezi, miundombinu, ujenzi na ukarabati wa nyumba n.k.

Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali hufanya ukaguzi wa akaunti na fedha zilizotumiwa na jeshi la polisi kila mwaka, na taarifa za ukaguzi huwasilishwa bungeni

6. Askari Polisi yuko juu ya sheria?
Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, tajiri kwa maskini, wanaume kwa wanawake, bila kujali dini na itikadi, hata wafanyakazi wa serikali na polisi wanatakiwa kutii sheria na kuishi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa nchini mwetu chini ya Katiba yetu.

Hii ina maana kila tendo linalofanywa na askari polisi lifanywe kulingana na sheria, na iwapo polisi hawatafanya hivyo watawajibika mbele ya sheria. Matarajio ni kuwa pia sheria zilizotungwa zimezingatia haki na usawa.

Askari anayevunja sheira anapaswa kuadhibiwa. Tena kwa kuwa polisi amepewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria, adhabu yake inatakiwa iwe kali zaidi anapovunja sheria.

Iwapo askari ametenda kosa la jinai anapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kama mtu mwingine. Lakini anaweza kupelekwa mahakama

7. Polisi na Rushwa:
Jina zuri la Jeshi la polisi na sifa njema ya watumishi wake inategemea sana uadilifu na uaminifu wa kila askari polisi. Kila tendo la rushwa au tuhuma za rushwa dhidi ya askari polisi inatoa sifa mbaya kwa jeshi la polisi. Hivyo, kila polisi anayefahamu kuwa polisi mwenzake anajihusisha na vitendo vya rushwa na akashidwa kuchukua hatua yoyoyte atakuwa anafanya makosa na atahusishwa kushiriki.

8. Polisi na Maandamano na Mikutano ya hadhara:
Mtanzania yoyote ana haki ya kushiriki katika maandamano kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hii inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko/maandamano ya amani.

Hata hivyo kundi linalofanya mkusanyiko/maandamano hayo katika maeneo ya wazi linapaswa kutoa taarifa kwa polisi si chini ya saa 48 kabla ya mkusanyiko/maandamano hayo. Taarifa inatolewa kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambalo mkusanyiko unapendekezwa kufanyika.

Iwapo kiongozi wa polisi anayepokea taarifa hiyo ana sababu ya msingi ya kuona kuwa mkutano unaopendekezwa unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa umma anaweza kuzuia mkutano huo kufanyika.

Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha amani inakuwepo. Kwa upande mwingine wanapaswa kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa amani na utulivu.

Matumizi ya Nguvu dhidi ya Maandamano au Mkutano wa hadhara.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.

Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.

9. Matumizi ya Silaha za Moto dhidi ya Raia.
Kama ilivyosemwa hapo juu, polisi watatumia nguvu kubwa pale ambapo imelazimika tu, na ambapo njia nyingine zote za udhibiti zimejaribiwa na kushindikana.

Polisi anaweza kutumia bunduki katika mazingira yafuatayo:

  1. Dhidi ya mtu anayetoroka, au
  2. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au
  3. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka asikamatwe
  4. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kumwondoa mtu mwingine kutoka kizuizi halali
  5. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kuzuia ukamatwaji halali wa mtu mwingine.
  6. Dhidi ya kundi linaloharibu mali au kutishia usalama wa raia baada ya kuonya mara tatu

Lakini pale tu askari anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyingine ana ametoa onyo kwa mtu huyo kuwa bunduki itatumika iwapo hatatii na mtu huyo hajali onyo lililotolewa. Pia endapo polisi watakuwa na sababu ya kuamini kuwa wao wenyewe wako hatarini kuumizwa vibaya.

Wanapolazimika kutumia bunduki dhidi ya kundi linalofanya uharibifu au kutishia usalama wa raia, risasi zinapaswa kulengwa chini na katika kundi linaloonekana ni tishio, lakini si kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi linapoonyesha dalili la kutawanyika askari wanapaswa kusitisha upigaji risasi.

Polisi wanaolazimika kutumia risasi wanawajibika kutolea maelezo kila risasi waliyotumia kwa kuandika taarifa inayowekwa katika kumbukumbu.

Pale itakapothibitika kuwa polisi ametumia nguvu isiyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.


10. Haki za Watu wanaowekwa Mahabusu.
Askari polisi wanawajibika kuwapeleka mahakamani watu waliowaweka mahabusu ndani ya masaa 24. Hata hivyo kwa watu waliokamatwa kwa kibali, kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo, polisi lazima wakupeleke mahakamani mapema iwezekanavyo.

Askari hawaruhusiwi kupiga, kutisha au kutia hofu mtu aliyewekwa kizuizini, na anayekiuka anaweza kuadhibiwa kwa kosa hilo.

Askari polisi ana haki ya kuhoji walio kizuizini, lakini hawezi kulazimisha mtu yeyote kuongea kitu chochote ambacho mtuhumiwa hana habari nacho, au kitu ambacho mtu hataki kukisema, au kukiri makosa ambayo polisi wanataka akiri.

Ungamo la kosa mbele ya polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika mahakamani kama ushahidi.
 
Katika matukio mengi polisi walioua raia hayasapotiwi na mazingira yaliyoruhusiwa na sheria hii. Huyu waziri amekengeuka na kwa maana hii naye ni muuwaji maana anatetea uuwaji. Tungekuwa na Bunge lenye viongozi makini, angetakiwa kuainisha kila tukio la uuaji lililifanywa na polisi na aoanishe ni kivipi sheria ilikuwa inasupport uuaji utokee.
 
nimejaribu kuangalia vitendo vya polisi kuua raia katika maandamano mbalimbali hapa nchini na kutafuta kipengele chake katika mlolongo wote hapojuu pamoja na ule uliotolewa na Ame Silima sipati mahali ambapo inakubaliana. Wanaouawa katika maandamano ni watu ambao hawana silaha mikononi, waandishi wa habari, wauza magazeti, watoto washule na wengine kama hao.
Miaka michache nyuma kuna wanafunzi wa shule moja ya msingi walikaa barabarari kushinikiza wawekewe matuta katika barabara ambayo inapita hapo shuleni kwao kavile ajali zimezidi wanafunzi kugongwa na magari, polisi walipokwenda kuwatimua walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto hatimaye mwamafunzi mmoja akapigwa risasi. Hivi kweli tembo akipigana na sungura anahaja ya kutumia silaha?
 
Alieleza kuwa Kifungu cha18 na 18(A) cha Sheria yaAdhabu Sura namba16 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002, kinampa haki mtu yeyote akiwemo askari kujilinda, kumlinda mtu mwingine, kulinda maliyake au mali ya mtu mwingine ikiwemo ya Serikali na taasisi zake, ambayo iko chini ya uangalizi wake kisheria.
Wakuu mimi hapa naona pamenikuna! Polisi nao kipigo kinawahusu kisheria inapokuja haki ya mimi raia kujilinda dhidi yao.
 
Wakuu mimi hapa naona pamenikuna! Polisi nao kipigo kinawahusu kisheria inapokuja haki ya mimi raia kujilinda dhidi yao.

Kiukweli hata mimi nimeguswa mnoooo,hapo ni self defense ndiyo inayofanya kaz,maana sote tunalindwa kwa sheria.

Safi sana mkuu kwa kuturuhusu.
 
Nilivyoelewa hapa ni kwamba hata raia anaruhusiwa kupiga (self defence) kama akipigwa. Kwa kuwa polisi wameruhusiwa kupiga basi na raia wameruhusiwa kujitetea. Tuache kulalamika sasa. Hongera pinda. Hongera silima
 
Nilivyoelewa hapa ni kwamba hata raia anaruhusiwa kupiga (self defence) kama akipigwa. Kwa kuwa polisi wameruhusiwa kupiga basi na raia wameruhusiwa kujitetea. Tuache kulalamika sasa. Hongera pinda. Hongera silima


Wewe bi jipuuzi kati ya wapuuzi,mifano yote hapo inatetea udhalimu wa polisi na sio raia,kama Police ruksa kuchukua sheria mkononi kwa kupiga je mahakama kazi yake??!!

Mwangosi aliuliwa kwa Lisa lipi hapo,achilia mbali Kofi cha Kombe na Korimba??!!
 
Wewe bi jipuuzi kati ya wapuuzi,mifano yote hapo inatetea udhalimu wa polisi na sio raia,kama Police ruksa kuchukua sheria mkononi kwa kupiga je mahakama kazi yake??!!

Mwangosi aliuliwa kwa Lisa lipi hapo,achilia mbali Kofi cha Kombe na Korimba??!!

Hukunielewa. Rudia kwa UTULIVU. Halafu usiandike kwa harakaharaka!
 
Mi Nadhan Pinda Na Wazir Wake Wasione Kwamba Polis Wananguvu Sana Kupita Raia Wanatukamata Sabab Tunawaheshim Na Kuheshim Sheria Ila Kwa Kauli Hiyo Ya Pnda Kwamba Wapigen Tu! Itafka Hatua Wananchi Nao Watasema Km Mbwahi Na Iwe Mbwahi Afu Ndo Ataona Kati Ya Polis Na Raia Nani Mtemi Ukizngatia Polis Wenyewe Tunaish Nao Mitaan Tunacheza Nao Disko Kiubabe Sometime Tuna..............
 
Mi Nadhan Pinda Na Wazir Wake Wasione Kwamba Polis Wananguvu Sana Kupita Raia Wanatukamata Sabab Tunawaheshim Na Kuheshim Sheria Ila Kwa Kauli Hiyo Ya Pnda Kwamba Wapigen Tu! Itafka Hatua Wananchi Nao Watasema Km Mbwahi Na Iwe Mbwahi Afu Ndo Ataona Kati Ya Polis Na Raia Nani Mtemi Ukizngatia Polis Wenyewe Tunaish Nao Mitaan Tunacheza Nao Disko Kiubabe Sometime Tuna..............
 
Wanasiasa kweli wengi wao ni bogus wanasahau kuwa kila mtu akianza kutafsiri sheria kadri ya ufupi wa upeo wake basi technically hata raia wanahaki kisheria kujihami dhidi ya shambulio lolote linaloweza kumdhuru.
 
Back
Top Bottom