Serikali yatoa ratiba ya unywaji wa pombe za kienyeji

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Serikali imewataka wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri, huku ikitaja muda unaoruhusiwa kwa ajili ya kunywa pombe hizo.
Pombe za kienyeji.jpg

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameyasema hayo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo.

“Pombe za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.


Chanzo: IPP Media
 
Hivi hizi sheria hutungwa wakiwa wamelewa hawa waheshimiwa wetu?...yani kweli kule vijijini kusipokuwa na nishati ya umeme waanze kunywa SAA 12 jioni mpaka sita usiku? ha ha ha hawapo serious bwana!...hawajui vijijini tunalala saambili usiku?...usalama was wanywaji na wauzaji usiku huo utadhibitiwa na akina nani?...

Baada ya mavuno kijijini wakae nyumbani tu mpaka sa12 ndo waende kulamba sio?....hizo leseni zinatolewa kwa bei gani? mtaji wa wao je?...haya bwana. Hapa kazi tu!
 
Back
Top Bottom