figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
- Ni kupitia Soko la Hisa la Dar es salaam
Akiongea wakati wa Uzinduzi wa uuzaji wa hisa za kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar e salaam, Dkt.Kijaji alisema kuwa uwekezaji huu utakuza shughuli za soko kwa asilimia kubwa “Hivi sasa wawekezaji katika hisa kwenye masoko ya mitaji hapa nchini ni takribani laki tano,hivyo iwapo wateja wote wa Vodacom milioni 12.4 watashiriki katika ununuzi wa hisa utaongeza uwekezaji wa hisa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa kwa asilimia 2,380%.
Alisema haya yatakuwa ni mageuzi makubwa katika sekta ya masoko ya mitaji na fedha si hapa nchini tu bali hata katika ukanda wa Afrika Mashariki kwani hivi sasa Kenya ina wawekezaji wapatao 1,700,000,Uganda 40,000 na Rwanda 14,000.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao amesema, “Tunayo furaha kuifikia siku ya leo ambapo tumefungua milango kwa wananchi wa Tanzania na tunawakaribisha wanaotaka kuwekeza katika safari hii ambayo tumeianza.Tukio hili ni la kihistoria katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, Vodacom Tanzania imekuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano hapa nchini kuandika historia ya kuuza hisa zake kwa umma kupitia Soko la benki ya NBC yenye matawi nchi nzima na mawakala kwa kuuza hisa kuwashirikisha watanzania wote katika safari ya mafanikio ya kampuni yetu”.
Ferrao alisema kuwa kuanzia leo,asilimia 25% za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC zitauzwa kwa watanzania kutokana na kibali kutoka serikalini kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na mitaji (CMSA)-“Kutokana na matakwa ya sheria hadi kufikia hatua hii tumepata ushirikiano mkubwa kutoka taasisi za serikali za CMSA ,DSE na wadau wengine,nashukuru kwa ushirikiano huu ambao umefanikisha mchakato mzima na leo wateja wetu nchini kote na taasisi mbalimbali za kitanzania zinazo fursa ya wabia wetu kupitia ununuaji huu wa hisa”Aliongeza.
Kuhusiana na mchakato mzima wa ununuaji wa hisa alisema “Kutokana na kuzinduliwa mchakato wa uuzaji hisa kuanzia leo,wanaohitaji kununua hisa watazipata kwa kutembelea matawi yote ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchi nzima “.Alitoa msisitizo kuwa kila hisa itauzwa kwa shilingi 850/-na asilimia 25% ya hisa zinazotarajiwa kuuzwa zina thamani ya shilingi Bilioni 476.
Ferrao alimalizia kwa kusema “Vodacom Tanzania PLC inayo dhamira ya kweli ya kuendelea kuwekeza nchini na kukuza sekta ya mawasiliano na kufanikisha malengo yake makuu ambayo ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidigitali,kuwaunganisha watanzania katika mtandao wake na kubadilisha maisha ya wananchi kuwa murua kupitia ubunifu mkubwa wa kiteknolojia.