Serikali yateua RPC Tarime, Rorya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yateua RPC Tarime, Rorya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Jul 9, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Serikali yateua RPC Tarime, Rorya [​IMG] [​IMG] [​IMG] Thursday, 09 July 2009 04:39 Na John Daniel, Dodoma

  SIKU chache baada ya Waziri Mkuu Bw. Pinda kutangaza hatua kadhaa za kurejesha amani wilayani Tarime,Serikali jana imetangaza kuundwa rasmi Mkoa wa Kipolisi Rorya na Tarime chini ya Kamanda Costantine Massawe.

  Uamuzi huo ulitangazwa bungeni jana na Waziri wa mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha wakati akifanya akijibu hoja mbalimbali za wabunge baada ya kuwasilisha bajeti ya wizara hiyo.


  Akitoa majumuisho ya bajeti ya bajeti hiyo, Bw. Masha alisema Serikali imefanya juhudi za maksudi kuunda kanda hiyo ili kukomesha mapigano hayo


  “Tatizo la mapingano hayo ni tangu ukoloni hivyo ni jambo la kihistoria na juhudi za Serikali zitakuwa bure iwapo wananchi hao hawatabadilika,” alisema Bw. Masha

  Alisema tatizo la mapigano jamii ya Kikurya si la kwisha leo wala kesho hivyo jambo hilo linahitaji muda wa kutosha kulishughulikia


  Kuhusu suala la vitambulisho vya taifa, alisema mradi ulianza mwaka 1968 wakati mama yake akiwa na umri wa miaka 18 yeye alikuwa bado hajazaliwa

  Alisema hivyo si kweli kuwa ucheleweshaji wa mradi unatokana na yeye kama baadhi ya wabunge wanavyodai.

  "Mimi naomba Bunge linipe nafasi nimalize maradi huo majalada ya kwenda katika kikao cha Baraza la Mawaziri yameandaliwa baada ya hapo watarudisha majibu kwa Katibu Mkuu na Bunge litajulishwa,"alisema.

  AwaliKambi ya Upinzani Bungeni iliitaka Serikali kulieleza Bunge hatua iliyofikiwa katika mradi wa utengenezaji vitambulisho vya taifa huku ikihoji hadithi mpya katika maendeleo ya mradi huyo mkubwa na kudai kuwa sh. bilioni 4.3 zilizotengwa kwa
  ajili ya mradi huo zinaendelea kuneemesha watu wachache.


  Pia kambi hiyo ilitaka Serikali
  kuchukua hatua ya haraka kulinda hali ya amani na utulivu nchini kwa kukomesha vitendo vya ualifu wa kutumia silaha zilizoanda kuibuka tena nchini kwa kasi .  Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kwa
  Wizara ya Mambo ya Ndani, Msemaji wa kambi hiyo Bw. Ibrahim Mohammad Sanya, (CUF), alisema ni wakati muafaka kwa Serikali kuwaeleza Watanzani hatua iliyofikiwa katika mradi wa vitambulisho na kuhoji
  sababu zinazofanya Serikali kushindwa kukabidhi kazi hiyo kwa RITA.  “Tangu mwaka 2006 hadi sasa 2009 bado
  mchakato unaendelea tu, kila siku tunaambiwa hadithi mpya, kuhusiana
  na vitambulisho hivyo, pesa za walipa kodi zinazidi kuwaneemesha
  baadhi ya watu katika kadhia nzima ya vitambulisho vya uraia, je
  Serikali inawatendea haki Watanzania?" alihoji Bw. Sanya.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,498
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Wanajiandaa kuwadhibiti wapinzani 2010 baada ya funzo walilolipata uchaguzi wa Tarime.
   
Loading...