Serikali yatenga Tsh. Bilioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa Meli mpya Ziwa Victoria

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Serikali imetengaTsh. Bilioni 21 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Victoria katika Mwaka wa Fedha 2016/17 ili kutekeleza ahadi iliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuondoa adha ya usafiri katika ziwa hilo.

Hayo yamesemwa jana Bungeni Dodoma na Naibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe (CHADEMA), Mhe. Joseph Michael Mkundi aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuleta meli mpya katika Ziwa Victoria.

“Serikali ina mipango thabiti ya kujenga meli mpya zitakazotoa huduma ya usafiri na usafirishaji katika Ziwa Victoria na maziwa mengine makuu ya Tanganyika na Nyasa,”alisema Ngonyani.

Kuhusu ukarabati wa meli ya MV Butiama iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Bandari za Mwanza na Nansio Ukerewe, Ngonyani alisema tathmini ya uharibifu ilibaini kuwa injini iliharibika sana na isingefaa tena kutumika kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo.

Aidha, Ngonyani alisema ilibidi inunuliwe injini nyingine mpya pamoja na gia boksi yake na kuongeza kuwa tayari Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ilikamilisha mchakato wa kupata injini stahiki kwa ajili yamelihiyo kwa beielekezi.

Ngonyani alisema kuwa katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17 serikali kupitia MSCL imetenga Tsh. Bilioni 3.6 kwa ajili ya matengenezo ya meliya MV Butiama ambayo yanataraji kukamilika ndani ya miezi kumi.

Kwa mujibu wa Ngonyani, MV Butiama ilisItisha huduma ya usafiri kati ya Mwanza na Nansio, Ukerewe mwaka 2010 baada ya injini yake kupata uharibifu mkubwa wa kukatika mhimili wake (Cranshaft).

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kuhusu ukarabati wa Meli ya MV Liemba alisema mazungumzo yanaendelea na Serikali ya Ujerumani kuikarabati meli hiyo ambayo imefanya kazi kwa miaka zaidi ya mia moja.
 
Back
Top Bottom