Serikali yatangaza bei mpya ya unga Dar

Nitarudi hapa kutamka maneno stahili siku nikienda dukani na kukuta KWELI kilo ya unga ni shs. 900/-

Sent from my GT-P7500 using Tapatalk 2
 
Soko huria limeishia wapi? Na kwanini unga na sio kitu kingine? mfano kodi za nyuma (wapangaji), au maharagwe?
 
Kila kitu ni Dar es Salaam. Gesi ya Mtwara inatakiwa iende Dsm, hata pia bei za chakula zishuke Dsm tu.

Kwa nini bei isishuke pia kwa watu wa maeneo kama ya Nanjirinji, Malivundo, Mkanyageni, Mismbati, Nkungi, Fukayosi n.k. Au haya maeneo hayapo kwenye ramani ya Tanzania?
 
mkuu usinikumbushe hii stori. vibali vilitolewa kwa wachaga karibia vyote. watu walikuwa wananunua sim cards ambazo hazijasajiliwa na kumpigia mkuu wa wilaya ya ilala na kumtukana na wengine walimtukana live. again, vibali vilitolewa kwa upendeleo sana na viligubikwa na rushwa za kati ya milion 2-5
 
Ule uchumi wa soko umeshindwa; si waliache soko liamue bei?

hizo ni habari za kwenye media ili kuwafurahisha wadanganyika! nani atasimamia bei hiyo mpya kuhakikisha kwamba bei ya unga ni Tsh. 900/=? mbona sukari tu ilimshinda mhe. Pinda kusimamia bei aliyotangaza! as long as tuko soko huria na TZ hatuna reguratory board ya kudhibiti bei za vyakula tunaoteshwa ndoto na serikali yetu!
 
Hivi Tan 3000 inaweza kumaliza matatizo ya gharama za unga Dar ambayo inasemakana ina watu zaidi ya million 7??

Mmmh, Hizi takwimu zinanichanganya. Dar es salaam ina watu zaidi ya million saba kama London or Paris. Are you sure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…