Serikali yasitisha usajili wa NGO’s

Serikali yasitisha usajili wa NGO’s

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,190
Katibu-Mkuu-Wizara-ya-Afya-Maendeleo-ya-Jamii-Jinsia-Wazee-na-Watoto-anayeshughulikia-Maendeleo-ya-Jamii-Sihaba-Nkinga.jpg

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Sihaba Nkinga.

Serikali imetangaza usitishaji wa usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) kuanzia Agosti 21 hadi Novemba 30, mwaka huu ili kufanya uhakiki wa NGO’s zilizosajiliwa.

Hatua hiyo imetangazwa jana na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Sihaba Nkinga, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

“Napenda pia kuujulisha umma kuwa kuanzia Agosti 21, 2017 hadi Novemba 30, 2017 usajili wa NGO’S mpya utasimamishwa, ili kutoa fursa kwa wataalamu kuchakata taarifa kutoka kwenye vituo vingine kuhakiki NGO’s zilizosajiliwa,”amesema Nkinga.

Bw. Nkinga amesema baada ya uhakiki huo unaotarajia kufanyika nchi nzima kukamilika, NGO’s zote ambazo hazitakuwa zimefanyiwa uhakiki zitafutwa kwenye Rejista na hazitaruhusiwa kuendesha shughuli zao nchini.

“Wakati tunaendelea na zoezi la uhakiki tutafanya tathmini ya mwenendo wa uhakiki katika kanda zote nchini na hatimaye kutoa uamuzi stahiki, ili kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanikiwa na wadau wetu wanahudumiwa kwa ufanisi mkubwa,”amesema Nkinga huku akiwakumbusha wahusika wa NGO’s kuwasilisha vyeti vyao vya usajili mapema kwa njia ya mtandao.

“Niwakumbushe pia, kuwa ni vema kuzingatia kuwa wakati wa uhakiki kila NGO’s inatakiwa kuwasilisha cheti halisi cha usajili na nakala ya cheti hicho, NGO-Fomu/UHK/2017 iliyojazwa vizuri. Fomu hii inapatikana katika tovuti ya uratibu wa NGOs kwa anuani ya www.tnnc.go.tz, stakabadhi za malipo ya ada ya mwaka au hati ya malipo benki toka kusajiliwa kwa shirika, Barua kutoka kwa ofisa maendeleo ya jamii (Mkoa/ wilaya/halmashauri au Manispaa) ikithibitisha uwapo wa ofisi ya shirika na nakala ya katiba ya NGO iliyothibitishwa na msajili wa NGOs,” amesema Nkinga.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania, Nicholaus Zacharia, amewatoa hofu wamiliki wa mashirika hayo na kuwataka kila mmoja kushiriki katika uhakiki huo.

“Sisi kama viongozi wenu tumejilidhisha serikali haina mpango wowote mbaya na Azaki zetu, hivyo mtu atakayekwambia usishiriki katika uhakiki anakutakia uende jehanamu,”amesema Zacharia.

Hata hivyo, Zacharia ameiomba serikali kuona ni jinsi gani inaweza kuanzisha bodi itakayokuwa inasimamia mashirika hayo tofauti na baraza hilo ambalo limekuwa likidumu kwa miaka mitatu.

Chanzo: Bongo 5
 
Ukitaka kujua nchi inayoelekea shimoni hizi ndo dalili zake
 
Watakatili watu, wengine walikuwa kwenye mpango wa kusajili NGOs za kusaidia yatima, wajane na waathirika wa UKIMWI!!!!
 
Badala ya kuongeza ajira wanapunguza ajira, jana manesi wasiuze maduka ya dawa, juzi makampuni yanaacha kuzalisha, kesho migodi itafungwa, hiyo ndiyo Sera yao ya viwanda
 
Keshokutwa utasikia mifuko ya viroba(visalfeti) vimepigwa marufuku kwa sababu vinatumika kuwekea maiti na kizitupa baharini hahahahahahaha hii ndiyo Serikali ya kukurupuka
 
Hapo kuna NGO's inatafutwa tu, hiyo ni uzugaji tu... Usikute hiyo NGO's Jesca alinyimwa Kazi, anataka kulipa kisasi.... Unajua operations zote zinazoanzishwa nchi hii, sio endelevu!.. Huwa wanapanga tu wanataka kumkomoa nani, na wakishampata operation inakufa... Unaona Operation ya madawa ya kulevya!.. Muhusika alikua Manji ndiye waliyemlenga kwa sababu zao Binafsi kabisa... Je operation ipo?... We subir mtaona

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Watakatili watu, wengine walikuwa kwenye mpango wa kusajili NGOs za kusaidia yatima, wajane na waathirika wa UKIMWI!!!!
Mbona ni muda mfupi sana...si mpaka Nov, 30/2017 tu! Uhakiki ni muhimu ukizingatia hali ya usalama na usambazaji madaya ya kulevya duniani.
 
Kuna NGO kazi zake zilikuwa ku promote USENGE, Ufiranaji na kugawa KY bure za kuweka njia ya haja kubwa ili usodoma na ugomora ufanywe vizuri... Serikali yetu safiii sana, ni kuwabana hao wahuni pia NGO zingine zinaweza kufadhili ugaidi na uchochezi wa kisiasa...

Vetting kali ipite kwa kila NGO..
 
Back
Top Bottom