Serikali yashusha gharama za Urasimishaji

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuanzia sasa gharama za urasimishaji haitazidi shilingi 150,000 badala ya 250,000 iliyopangwa awali na makampuni yatakayoenda kinyume yatachukuliwa hatua ikiwemo kufutwa.

Lukuvi alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Makampuni ya Upangaji na Upimaji yanayofanya kazi ya urasimishaji katika mitaa mbalimbali nchini pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, baada ya Wizara yake kuona zoezi la urasimishaji linasuasua wamegundua asilimia 30 pekee ndiyo iliyorasimishwa tangu kuanza zoezi hilo na hali hiyo imechangiwa na uwezo mdogo wa wananchi wengi kumudu gharama za urasimishaji.

Waziri Lukuvi alisema, alichotegemea kwa makampuni yaliyopewa kazi ya urasimishaji ni kuwa na uzalendo kwa kushusha gharama lakini yameshindwa kupunguza gharama jambo lililoifanya serikali kuona haja ya kupitia upya gharama hizo na kubaini gharama za msingi ili kumuwezesha mwananchi kupata hati na kusisitiza punguzo hilo halitawahusu waliolipia gharama za urasimishaji.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameyataka makampuni yanaoyoendesha zoezi la urasimishaji kuhakikisha kiasi cha fedha inachowatoza wananchi kinaishia hatua ya Hati na gharama itakayolipwa na mwananchi baada ya kurasimishwa ni kodi ya ardhi na kuyatahadharisha kutochukua muda mrefu kukamilisha zoezi hilo.

Amewataka wananchi wote wanaoishi kwenye maeneo yasiyo rasmi kuhakikisha wanaingia katika zoezi la urasimishaji ili kupata hati itakayowawezesha kiuchumi na kusisitiza kuwa suala hilo linafanyika kwa nia njema kwa nia ya kuwaongezea mtaji wananchi kwa kupatiwa nyaraka itakayowasiadia kukopa fedha benki.

Akigeukia suala la Leseni za Makazi, Waziri Lukuvi alisema zoezi hilo linaendelea vizuri katika jiji la dar es Salaama kwa gharama ya shilingi elfu tano hadi hatua ya upatiwaji leseni ya makazi na kusisitiza kuwa leseni hiyo siyo ya kudumu bali itakuwa kwa miaka mitano na kuwataka wananchi walio katika maeneo ya urasimishaji kuendelea na zoezi hilo kwa kuwa wizara inayo kanzi data itakayotunza takwimu za mazoezi yote mawili.

‘’Tunataka kuwa na database ya nani anamiliki ardhi kiasi gani na kila mwananchi lazima awe na leseni ya makazi au hati kwa lengo la kushiriki kulipa kodi’’ alisema Lukuvi

Hata hivyo, Lukuvi alisikitishwa na baadhi ya Makampuni ya urasimishaji kushindwa kutoa takwimu wakati wa zoezi la upimaji zinazoendana na miongozo ya wizara na kuyataka yote yaliyoenda kinyume kurudia zoezi na kuongeza kuwa kuna makampuni 34 yaliyotuma takwimu ambazo ni chafu na kuyapongeza makampuni mawili ya Visible Planners na Afro Max kwa kufuata taratibu zote za urasimishaji.

Lukuvi alionya baadhi ya makapuni ya urasimishaji kuacha kuwalaghai wananchi kwa kuwapatia leseni za makazi badala ya hati kwa gharama za urasimishaji na kusema kufanya hivyo ni kosa la uhujumu uchumi na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
 
Utaratibu wa Malipo ukoje mkuu...
 
Tatizo lipo kwenye utekelezaji !

Nani waku enforce hiyo?

Watendaji pale Wizarani na halmashauri bado wanaurasimu mkubwa!

Watendaji wako bado ni shida !
 
Hivi huwa Mnakuwa na vikao kazi?
Je huwa mnataarifa ya maombi ya hati kwa wiki au mwezi ni mangapi?
Yaliyokubaliwa na kutolewa hayo ni mangapi?
Yaliyokataliwa yamejibiwa kwa waombaji?
Sababu za kukataliwa ni zipi?
Je wangapi wameomba vibali vya ujenzi kwa kila wiki au mwezi?
Je vibali vingapi vimetolewa kati ya vilivyoombwa?
Je vilivyokataliwa wananchi wamepewa majibu na sababu za kukataliwa?

Yani watendaji wengi Ardhi ni shida kubwa!

Yani wamekalia “delaying technique tu”
 
  • Thanks
Reactions: ita
Kama wanakupaga taarifa ya utendaji huenda wanafanya kuzipika tu
 
Kiujumla wizara hii bado kunashida kubwa sana! Mfano kampuni inatangaza kuuza viwanja kwa bei ya 75000 kwa mwezi ndani ya miaka mitatu, lakini wanakwambia baada ya kumaliza kulipia mteja atalazimika kulipia gharama za kufuatiria hati wizarani lakini gharama hizo hazitajwi.
Pili... mteja atalazimika kulipia kodi ya pango la aridhi ambayo nayo haitajwi ndani ya miaka hyo itakuwa bei gani.
Tatu.... ndani ya miaka hiyo huruhusiwi kupanda hata mgomba ndani ya eneo hilo.
Mwisho... malipo hayo ya kila mwezi yanawekwa kwenye account number ambayo haijatajwa kwenye mkataba lakini pia mkataba huo haujaea Authorised na wizara ya aridhi au halmashauri husika.

Ninacho kiona watu wanapigia hesabu ya 75000x36 wanaona ni bei nafuu au 38000x36 lakini kitakachokuja kuwakuta watajikuta wamenunua viwanja hivi kwa 9ml.au zaidi tofauti na hesabu inayoonekana sasa.
Lukuvi anatakiwa ayaangalie haya makampuni yanayojitangaza kwenye vyombo vya habari vinginevyo ajiandae kwa migogoro mipya ambayo mwananchi atakuwa kishapoteza kwa mujibu wa mikataba ya makampuni haya.
 
Back
Top Bottom