Serikali yasema wawekezaji wa kilimo cha miwa wameanza kujitokeza

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Waziri Mkuu, KASIM MAJALIWA amesema Serikali imejipanga vyema ili tatizo la upungufu wa sukari ambao umelikabili Taifa kwa sasa liwe historia kuanzia mwakani.

Amesema kwa kuanzia tayari wamejitokeza wawekezaji kadhaa kutaka kuwekeza katika kilimo cha miwa.

Waziri Mkuu amesema hayo bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu maswali kwa Waziri Mkuu alipotakiwa na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni FREEMAN Mbowe kuelezea ni lini sukari ya ziada itawasili nchini kuziba pengo lililopo.

Waziri Mkuu amesema mpango wa Serikali wa kuruhusu uwekezaji katika kilimo cha miwa katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani upo katika hatihati kufuatia moja kati ya kamati za bunge kusema kuwa siyo vyema eneo hilo kutumika kwa kilimo cha miwa na uz alishaji wa sukari.

Amesema hali hiyo inatokana na kiwanda cha sukari kuhitaji maji mengi ambayo yangetoka Mto Wami wakati maji hayo hayo yanatakiwa pia kutumika katika mbuga ya wanyama ya Saadani ambapo kipaumbele imeshauriwa iwe mbuga ya wanyama na viwanda kujengwa sehemu nyingine.
 
Back
Top Bottom