Wakulima wa miwa Kilombero wamtaka Rais akifika Kilombero aitishe mkutano wamueleze malalamiko yao

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
295
925
Wakulima wa Miwa wa Bonde la Kilombero wamemng'ata sikio Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa katika ziara yake Kilombero asikubali kuongea na viongozi wa Amcos kwani kwa sehemu kubwa wanatumiwa na Waziri Bashe kuficha aibu ya kutunga sheria ya kuua kilimo cha miwa na viwanda vya sukari.

Badala yake wamemuomba Rais Samia atume watu wake nje ya mfumo wa Wizara ya Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Moro na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwani ni kama wana njama ya pamoja na kufanyanyia sanaa mheshimiwa Rais akifika Kilombero ionekane wakulima wa miwa hawana malalamiko yoyote.

Wamemuomba Mheshimiwa Rais akifika Kilombero aitishe mkutano wa wakulima wote wa miwa na kuzungumza nao kwenye mkutano wa pamoja wamueleze malalamiko yao dhidi ya waziri wa kilimo na asikubali kuandaliwa mkutano wa viongozi wa AMCOS kwani wao wako upande wa kumtetea Bashe na maovu aliyofanya kwenye sukari.
 
AMCOS ndio taasisi halali inayowakilisha wakulima wa miwa, hatuwezi kumkutanisha Rais na wahuni tu, na madalali. Ushirika ndio msingi wa maendeleo ya kilimo.

Kama Seif anatafuta pa kupenyea, hakuna, yeye aendelee kumjaza mahela Mpina na waandishi wa habari
 
Seif gani huyo?
 
Hii nchi ngumu sana
 
Attachments

  • Screenshot_20240801_134238.jpg
    Screenshot_20240801_134238.jpg
    139.3 KB · Views: 7
AMCOS ndio taasisi halali inayowakilisha wakulima wa miwa, hatuwezi kumkutanisha Rais na wahuni tu, na madalali. Ushirika ndio msingi wa maendeleo ya kilimo.

Kama Seif anatafuta pa kupenyea, hakuna, yeye aendelee kumjaza mahela Mpina na waandishi wa habari
Mafisadi utawajua tu.
Hao AMCOS ni watu wa njaa wahujumu uchumi wakubwa.
Mwaka 2022 na 2023 wameuza pembejeo za ruzuku na viongozi wa vijiji hadi aibu.
Angalau mfumo mpya wa 2024 wa kuhakiki mashamba na kuchukua GPS coordinates umepunguza wizi huo.

Hatutaki kuwafungisha watu lakini Mimi nimeuziwa dawa za ruzuku maduka ya pembejeo na mitaani/vijijini zenye nembo ya government of Tanzania.
 
Wewe ndio kundi hilo hilo la wezi wa pembejeo
 
AMCOS ndio taasisi halali inayowakilisha wakulima wa miwa, hatuwezi kumkutanisha Rais na wahuni tu, na madalali. Ushirika ndio msingi wa maendeleo ya kilimo.

Kama Seif anatafuta pa kupenyea, hakuna, yeye aendelee kumjaza mahela Mpina na waandishi wa habari
Sawa Mr Bashe
 
Wewe ndio kundi hilo hilo la wezi wa pembejeo
Kwa hivyo Mimi ndiyo nimeenda kuwauzia maduka ya pembejeo pesticides za ruzuku za serikali?
Nilipewa dhamana ya kuzisambaza na serikali?
Sisi wakulima tunaenda dukani tunazikuta zinauzwa.
 
Wakulima wa Miwa wa Bonde la Kilombero wamemng'ata sikio Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa katika ziara yake Kilombero asikubali kuongea na viongozi wa Amcos kwani kwa sehemu kubwa wanatumiwa na Waziri Bashe kuficha aibu ya kutunga sheria ya kuua kilimo cha miwa na viwanda vya sukari.

Badala yake wamemuomba Rais Samia atume watu wake nje ya mfumo wa Wizara ya Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Moro na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwani ni kama wana njama ya pamoja na kufanyanyia sanaa mheshimiwa Rais akifika Kilombero ionekane wakulima wa miwa hawana malalamiko yoyote.

Wamemuomba Mheshimiwa Rais akifika Kilombero aitishe mkutano wa wakulima wote wa miwa na kuzungumza nao kwenye mkutano wa pamoja wamueleze malalamiko yao dhidi ya waziri wa kilimo na asikubali kuandaliwa mkutano wa viongozi wa AMCOS kwani wao wako upande wa kumtetea Bashe na maovu aliyofanya kwenye sukari.
Ninavyoelewa wafanya biashara waagizaji sukari toka nje sio rafiki na ukulima wa sukari kwa hivyo wanakula njama kuhujumu wakulima wa sukari. Wafanya biashara hao wengi wana asili ya kihindi na kuagiza sukari unakuta ni biashara ya familia zao miaka tangu wameletwa na wakoloni kujenga reli kisha wakaingia biashara. Serikali ikiwaendekeza na njama zao za kuhonga vigogo wa serikali nchi hii haitakaa milele ijitosheleze kwa kujitegemea kwa mahitaji yake ya mazao na viwanda kama vya sukari. Hivyo hivyo kwa ngano. Nakumbuka jaribio la kulima ngano huko karatu awamu ya kwanza kwa msaada wa canada ukihujumiwa kwa wafanya biashara kugoma kununua ngano ya nchini na kuendelea kuagiza toka nje. Ukienda kwa wale wa kuagiza magari lazima kila mwaka serikali inunulishwe magari ya kifahari hata kama sio kipaumbele mradi hao wadosi wafanye bishara.
 
wakulima hawana mtetezi
 
Sisi walaji tunauliza kuwa sukari ipi itauzwa 2000 kwa kilo?

Hii ya ndani ya nchi au hiyo ya kuagiza ?
 
Back
Top Bottom