Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 33,703
- 40,335
SERIKALI mkoani Katavi kuanzia sasa imeruhusu wazee wa jadi na machifu mkoani humo kufanya matambiko katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi iliyopo wilayani Mlele ili wanyama waishio humo wasiweze kuuawa na majangili kama ilivyo katika hifadhi nyingine za taifa nchini.
Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk Rajab Rutengwe wakati akifungua mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili kwa kina Mpango Kamambe wa Mji wa Mpanda na Mwongozo wa Ukuaji wa Mji huo 2014-34 uliofanyika mjini hapa.
Aliongeza kuwa wazee hao wa jadi pamoja na baadhi ya machifu wameruhusiwa kufanya matambiko katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi kila mwaka ili wanyama waliomo humo waweze kuzaliana kwa wingi, lakini pia kutouawa kiholela na majingili kama ilivyo katika Hifadhi kadhaa za taifa nchini.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Sitalike kilichopo karibu na hifadhi hiyo ya Katavi wakizungumza kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, wamekiri kuwa kutokana na kutofanyika kwa matambiko ya jadi majingili sugu wamekuwa wakiua kiholela wanyama wakiwemo nyati,tembo na twiga.
source: habarileo
My take: wanajf ni kweli tambiko litazuia ujangili!?