Mwana wa Mungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2008
- 1,003
- 85
Nimelazimika kuandika suala hili, naweza kusema mimi mdau wa tasnia ya sheria, mwenyezi Mungu amenisaidia nimezunguka maeneo mengi duniani kikazi nikilitumikia taifa, na nimewiwa kutoa maoni yafuatayo kwa serikali iyaangalie kwa makini.
Suala lenyewe linahusu watu wanaoitwa STATE ATTORNEYS au kwa kiswahili, MAWAKILI WA SERIKALI. hawa ni watu walioko chini ya mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na mkurugenzi wa mashitaka, ni wadogo zangu, wengine wake zetu. actually kwenye familia yetu tunao wawili. lakini maisha yao hayabadiliki, ni magumu kusema kweli. hivi serikali yao huwa haiwaangalii hawa watu, nimetembea nchi nyingi, kada hii haifanani kabisa na kada zilizoko nchi za wenzetu ambazo ziko kama wao.
Matokeo yake, kinachoendelea kwa mawakili wa serikali ni kwamba, watu wanakimbia kada. anakaa kidogo akishaona hapafai, anapiga hela za rushwa, halafu ana lala mbele anaenda kuwa mwanasheria wa kujitegemea. mtu kama huyo serikali inakuwa imeshampatia mafunzo mengi/training nyingi sana kwa garama ya serikali, lakini hata kabla hajainufaisha serikali kwa kile alichokisomea, ameona hakuna faida kuwa wakili wa serikali na anaondoka kwenda kuwa mtetezi wa washitakiwa wanaoshitakiwa na serikali. na zaidi ya wengi wanaoondoka, ni wale ambao wamefikia level ya senior, kwa hiyo waliobaki ni wale ambao ni junior tu ambao hawana uwezo mzuri kuendesha kesi na kutetea serikali, matokeo yake serikali inazidi kushindwa kesi kwasababu waliopo ni majunior tu hawana experience, wenye experience wameondoka kukimbia ofisi...na hao majunior wakipata experience na kuwa seniors basi wanaondoka kukimbia kada. hivyo tusishangae kwanini serikali inashindwa kesi kila siku, ni kwasababu waendesha mashitaka waliopo ni juniors , seniors wameondoka wamekimbia ofisi.
Binafsi nawaonea huruma hawa wadogo zangu, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. ninakuomba MAGUFULI, angalia kwa jicho la huruma kwa hii ofisi, kwasababu hawa wakiamua kuharibu kesi serikali isishinde, majambazi wote wataachiwa huru bila kufungwa, hao unaowakamata wala rushwa wataachiwa bila kufungwa, watarudi kwa wananchi na wananchi wataishi bila amani kabisa. hao vibaka watarudi mtaani, hao wabakaji watarudi mtaani, hapo ndipo mtaona ni ya muhimu. angalia mshahara wao, angalia kama kuna allowance zozote, angalia wanakoishi, angalia risky allowance zile unazowapa polisi kwanini hawa hauwapatii wakati nao wako kwenye risky sana? au unataka waharibu kesi ili usipate sifa? na mwanasheria mkuu wa serikali huwa hawaongelei kabisa kuwatetea hawa watu, wakati jaji mkuu anawatetea sana mahakama na mahakama maisha yao yamerahisishwa sana, kwanini mwanasheria mkuu wa serikali hapiganii maslahi ya watu wake? ni kwanini? basi wataondoka wote ili muendelee kuwa na wafanyakazi wasio na uzoefu, nao wakipata uzoefu wakimbie muendelee kupata kazi ya kuwatrain wapya ili nao waje kukimbia badae. kwaheri, hayo ni yangu ya moyoni.

1. WAKILI wa serikali ni mtu ambaye ana risky nyingi sana, ni prosecutor wa kesi kubwa za ajabu, lakini analipwa hela kidogo sana.
2. Inakuwaje wakili anayelipwa hela kidogo sana, ukampa aendeshe kesi ya bilioni moja, mbili au hata milioni mia. hawezi kuwa compromised kweli? wakili analipwa hela kidogo, mshitakiwa anaweza kumpa hela inayotosha mafao yake akistaafu, kwanini asile rushwa?
3. Wakili anaishi nyumba mbovu, amezungukwa na washitakiwa, washitakiwa ndio majirani zake, kwanini asishirikiane nao, no wonder anaweza hata kuamua kuwa rafiki wa watenda makosa na kutengeneza network kwasababu analipwa kidogo, anaishi maisha risky mtaa wa wahalifu kwasababu huko ndiko ana afford kulipa kodi na halipwi risky allowances.
4. Wakili hana usafiri, anapewa lift na washitakiwa.
HII NI OFISI PEKEE AMBAYO HAINA MAJENGO YAKE BINAFSI ZAIDI YA JENGO MOJA TU la makao makuu. hivi viongozi haina?
5. Wakili hana hela kuendesha familia, lakini amezungukwa na washitakiwa wanaoweza kumlipia ada ya watoto wake hadi wanamaliza, atashindwaje kuharibu kesi?
6. Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni ngumu kufanya kazi na haina msemaji. ni ofisi ya aibu sana kwasababu majengo karibia yote nchini wamepanga, wakati PCCB wamejenga majengo yao karibia kila mkoa. wakati huohuo upo ushahidi kuonyesha kwamba kila mkoa kuna kiwanja ambacho ofisi hii imepewa ili kujenga jengo, sasa angalia hiyo kodi wanayolipa kwa mwezi ni shilingi ngapi ambayo ingewashinda kujenga majengo yao, na ni kwanini wanapenda kupanga tu, huko kupanga kunamfaidisha nani na kunamwathiri nani? je kunamwathiri mtu binafsi au wafanyakazi? ofisi haina marupurupi hivi mnafikiri watu wataendelea kufanya kazi ofisini kwenu kweli, hivi kuna mtu anasoma ili ateseke?

7. Hii ni ofisi ambayo imeshikilia mambo mazito sana yanayoisaidia serikali lakini serikali haiijali hii ofisi. hii ni ofisi inayoishauri serikali mambo ya msingi, hii ndio ofisi inayoshitaki wauaji, majambazi, na wahalifu wote ili raia mkae kwa amani. hii ni ofisi ambayo inatoa ushauri na kusaidia wananchi bure, ni ofisi ya wananchi, lakini serikali haiwathamini kabisa. hivi ni kwanini?
Matokeo yake, kinachoendelea kwa mawakili wa serikali ni kwamba, watu wanakimbia kada. anakaa kidogo akishaona hapafai, anapiga hela za rushwa, halafu ana lala mbele anaenda kuwa mwanasheria wa kujitegemea. mtu kama huyo serikali inakuwa imeshampatia mafunzo mengi/training nyingi sana kwa garama ya serikali, lakini hata kabla hajainufaisha serikali kwa kile alichokisomea, ameona hakuna faida kuwa wakili wa serikali na anaondoka kwenda kuwa mtetezi wa washitakiwa wanaoshitakiwa na serikali. na zaidi ya wengi wanaoondoka, ni wale ambao wamefikia level ya senior, kwa hiyo waliobaki ni wale ambao ni junior tu ambao hawana uwezo mzuri kuendesha kesi na kutetea serikali, matokeo yake serikali inazidi kushindwa kesi kwasababu waliopo ni majunior tu hawana experience, wenye experience wameondoka kukimbia ofisi...na hao majunior wakipata experience na kuwa seniors basi wanaondoka kukimbia kada. hivyo tusishangae kwanini serikali inashindwa kesi kila siku, ni kwasababu waendesha mashitaka waliopo ni juniors , seniors wameondoka wamekimbia ofisi.
Binafsi nawaonea huruma hawa wadogo zangu, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. ninakuomba MAGUFULI, angalia kwa jicho la huruma kwa hii ofisi, kwasababu hawa wakiamua kuharibu kesi serikali isishinde, majambazi wote wataachiwa huru bila kufungwa, hao unaowakamata wala rushwa wataachiwa bila kufungwa, watarudi kwa wananchi na wananchi wataishi bila amani kabisa. hao vibaka watarudi mtaani, hao wabakaji watarudi mtaani, hapo ndipo mtaona ni ya muhimu. angalia mshahara wao, angalia kama kuna allowance zozote, angalia wanakoishi, angalia risky allowance zile unazowapa polisi kwanini hawa hauwapatii wakati nao wako kwenye risky sana? au unataka waharibu kesi ili usipate sifa? na mwanasheria mkuu wa serikali huwa hawaongelei kabisa kuwatetea hawa watu, wakati jaji mkuu anawatetea sana mahakama na mahakama maisha yao yamerahisishwa sana, kwanini mwanasheria mkuu wa serikali hapiganii maslahi ya watu wake? ni kwanini? basi wataondoka wote ili muendelee kuwa na wafanyakazi wasio na uzoefu, nao wakipata uzoefu wakimbie muendelee kupata kazi ya kuwatrain wapya ili nao waje kukimbia badae. kwaheri, hayo ni yangu ya moyoni.
Last edited by a moderator: