Serikali yapiga mnada meno ya viboko

Serikali yapiga mnada meno ya viboko

young zahabu

Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
80
Reaction score
35
SERIKALI imesema kuwa, Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) itafanya mnada wa hadhara wa meno ya viboko vipande 12,467 vyenye uzito wa kilo 3,580.29.

Imesema mnada huo utakaosimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango umepangwa kufanyika Januari 29, mwaka huu saa nne asubuhi katika Jengo la Mpingo, Barabara ya Nyerere Jijini Dar es Salaam, zilipokuwa ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii (Ivory Room).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk James Wakibara alisema katika taarifa yake kuwa mnada huo utawahusisha wafanyabiashara wa nyara waliopewa leseni ya Nyara Daraja la Kwanza mwaka 2017.

Alisema wafanyabiashara hao wataruhusiwa kukagua meno hayo kati ya Januari, 25 na 26 mwaka huu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa na nusu jioni kabla ya siku ya mnada huo.

Amesema wanunuzi watakaoshinda mnada huo watatakiwa kulipa asilimia 25 ya malipo yote papo hapo na asilimia 75 itakayosalia kulipwa ndani ya siku 14 zijazo baada ya mnada huo.

“Mtu yeyote atakayekuwa ametamka bei ya juu, kisha akashindwa kulipa asilimia 25 ya bei aliyotamka, atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga mnada na hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” alionya.

Alisema meno hayo yatauzwa kwa wastani wa uzito wa nusu kilo bila kugawanywa au kuchambuliwa wakati wa mnada na wanunuzi wataruhusiwa kuondoa bidhaa kwenye eneo la mnada baada ya kulipia ada na kodi husika kikamilifu na kupewa hati ya kumiliki nyara hizo. Source cloudz media
397e189e93cd709d8851dded70988c44.jpg
 
Soon wataanza kunadisha ngada zinazokamatwa
 
Hahahahaha naona wanajihami na dokta SHIKA asije enda kufanya yake

kuwa ataetamka bei ya juu akashindwa kulipa atachukuliwa ni mwenye kuvuruga mnada!
 
bora hlf hiyo hela wailete ifanye maendeleo maana ni za rasilimali nchi hivyo nchi ifaidike nayo.
 
Hayo meno yanatumika kufanyia nini?
Matumizi yake ni yale yale kama ya meno ya Tembo ila haya ya hippo yana thamani ndogo
Sasa naona majangili wengi wamehamia kuuwa viboko kwani hata ubebaji ni rahisi.
Ripoti zinasema wanunuzi wakubwa ni Hong Kong ndio hub na kwetu na jirani Uganda ndio yanatoka kwa wingi.

Hawa wanyama kuna hatari wakatoweka hivi karibuni
 
Hahaha kule kigwangala eti anawatuhumiwa huku mnatuuzia meno ya tembo, kesho mtatukamata eti tuna nyara za serikali.
Zamani walikuwa wanayauza kimyakimya na kutudanganya eti wanayachoma moto hahaha.
Trump aliposema sasa ruksa biashara meno ya tembo yakakosa soko, maana wachina wanayo mengi yetu hayana soko tunapiga mnada, hahaha Tanzania ya viwonder
 
Back
Top Bottom