Serikali yapiga marufuku usambazaji wa sukari ya KK na kuiondoa sokoni mara moja

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Charles Mwijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Mwijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.
Mwijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

image.jpeg
image.jpeg
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Kaijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja(KK) bila ushauri wa daktari.
Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Kaijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.Kaijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBC,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya
View attachment 358650 View attachment 358651

Swali ni kwamba, hiyo sukari iliingiaje sokoni kabla mamlaka husika hazijathibitisha ubora wake? Nani aliidhinisha hilo? Kwa maslahi ya nani? Waliokwisha kutumia wakiweza kuthibitisha madhara waliyopata serikali itawasaidia kulipwa fidia?
 
Safi sana. Hii sukari niliipiga vita sana tokea ilipozinduliwa miaka kadhaa iliyopita, hatimaye serikali sikivu ya Magufuli, serikali yenye kujali maslahi ya wanyonge imeliona hili na kuamua kuingilia kati kabla sukari hii haijasababisha madhara zaidi.

Go Magufuli... Go... Watanzania wazalendo wenye uchungu na Taifa hili tupo nyuma yako tukiunga mkono jitihada zako na kukuombea.
 
Duh sasa mkulima kama mimi taijuaje hiyo sukari? huku moshi na arusha kuna min supermarket kibao zinauza sukari ambazo hazina nembo, zinawekwa kwenye transparent bags.
 
KK
Mbona sio ya leo hii
Inamaana leo ndio imekuwa sio!!
Mbona ina nembo ya TBS

Inabidi utumie kwa ushauri maalum wa Daktari, kama kijiko kimoja kinaweza kukoleza lita moja ya Chai vipi wewe unaekunywa kikombe kimoja kwa kuunga kijiko kizima.?

Mkuu hapa ndio utona hata mamlaka zilizolala zinaamka. Ukiona wanazuia jua sheria ilikuwepo ila waliikalia kwa maslahi yao bila kuwapa wananchi Elimu juu ya madhara wanayoweza kuyapata.!
 
Hehehe I'm curious kusikia research findings, sio tunaambiana juu juu tu kua ina madhara flani, tunaomba data, tupo ambao tunaweza kuzisoma na kuzielewa vizuri, hatukusoma haya mambo ili tufichwe. Isije kua na hii wamekurupuka, "kijiko kimoja tu sukari imekolea" sio sababu, tunataka scientific analysis iwekwe public tuione. Ina maana TBS kui~approve miaka iliyopita walikua hawajaipima kuona kiwango chake? Kama ndio basi wawajibishwe, hiki ni kitu kina~concern afya ya binadamu hakipaswi kuchukuliwa lightly.
 
nawashauri wale wote wanaotaka kutoa ujumbe kwa kulitaja jina la jamaa wawe wanaweka picha ya Pombe au picha ya Kufuli pale panapoitaji kuweka jina la Jamaa ili wasie kuambiwa wametukana
 
Hii nchi bana ina wanasheria wasio saidia raia wake! Tunahitaji taasisi kama TBS (simu feki na bidhaa hafifu/feki), TFDA (bidhaa feki), TANESCO (kuunguza vyombo/nyumba na kukata umeme hpvyo hovyo), DAWSCO (kukata maji bila taarifa/kupampu maji machafu), EWURA na SUMATRA (ajali na migomo ifikie hatua wafungwe wao-akili zitawarudi), nk waanze kushitakiwa:
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Kaijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Kaijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.

Kaijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

View attachment 358650 View attachment 358651
Ongeza Bidii bado hujafikia kiwango cha kuwa mfanyakazi bora kwa vigezo vyangu bado fungia kitu kingine ujipatie point 5.
 
Maswali yako ni mazuri sana lakini hutasikia yakijibiwa.

Swali ni kwamba, hiyo sukari iliingiaje sokoni kabla mamlaka husika hazijathibitisha ubora wake? Nani aliidhinisha hilo? Kwa maslahi ya nani? Waliokwisha kutumia wakiweza kuthibitisha madhara waliyopata serikali itawasaidia kulipwa fidia?
 
Hii si ilikuaga inasambazwa zamani na yule tajiri kijana anayesema anataka kutengeneza ajira za kutosha
 
Swali ni kwamba, hiyo sukari iliingiaje sokoni kabla mamlaka husika hazijathibitisha ubora wake? Nani aliidhinisha hilo? Kwa maslahi ya nani? Waliokwisha kutumia wakiweza kuthibitisha madhara waliyopata serikali itawasaidia kulipwa fidia?

Hivi nyie watu huwa mnasoma maelezo kweli?

Kwani umesikia hiyo sukari ni feki?

Sukari ya KK ni kwa ajili ya kutengenezea vinywaji na sio kwa matumisi ya mtu wa kawaida.

Ndio maana akasema inatakiwa iuzwe kwa watu wa kawaida ila kwa maelezo kamili toka kwa wataalam jinsi ya kutumia kwa matumizi ya kawaida...

Maana ya kijiko kimoja mnaielewa? We ukitumia sukari hii y pa kawaida unaweza ukaweka zaidi ya kijiko kimoja, ila hii ni kali zaidi jamani, si kwa ajili ya matumizi ya kawaida, bali hutengenezwa kwa madhumuni ya viwanda jamaniiiiiiiii....

Sasa mtu unakurupuka na kusema iliingiaje bila kuthibitisha ubora wake, kuna mwingine hapo juu kasema mbona ina nembo ya TBS... Kuwa na tbs sio tatzo tatzo ni matumizi ni ya wapi na kivip?
 
Back
Top Bottom