Serikali yanuka uozo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yanuka uozo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 6, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Serikali yanuka uozo
  • Wateule wa JK wachafuka

  na Mwandishi wetu
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  KUBAINIKA kwa tuhuma nzito za ufisadi na uporaji wa mabilioni ya fedha kumefichua uozo mkubwa uliozigubika taasisi za serikali zikiwamo wizara mbalimbali, kiasi cha kuwalazimisha baadhi ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

  Ubadhirifu mkubwa ulioibuliwa na kamati mbalimbali za Bunge kila kona, umeiweka serikali ya Rais Kikwete katika wakati mgumu, kutokana na ukweli kwamba wanaotuhumiwa kuhusika na uporaji huo wa kutosha ni wale aliowateua kuongoza taasisi hizo.

  Wizara nyingi zilizofika mbele ya kamati za Bunge zilibainika kuhusika na matumizi mabaya ya fedha kiasi cha kuwalazimisha wakuu wa wizara hizo wakiwamo mawaziri kutimuliwa na kuamriwa kujipanga upya kutoa maelezo ya namna gani fedha za umma zimetumika vibaya.

  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ndiyo inayoongoza kwa kugundua ‘madudu’ katika wizara na idara nyingi za serikali, kiasi cha kuwafanya wabunge wa kamati hizo kutoa maagizo magumu yakiwamo ya kutishia kuwafikisha katika vyombo vya dola wakuu wa taasisi hizo.

  Moja ya wizara zilizokumbwa na tuhuma hizo ni ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inayotuhumiwa kutumia sh bilioni 1.1 kama fidia kwa wakazi waliopisha nguzo za mkongo wa taifa, huku ikishindwa kuwasilisha vielelezo vya matumizi ya fedha hizo.

  Maelezo ya Katibu Mkuu wake, Florence Turuka, kwa wajumbe wa kamati hiyo kwamba wizara iliwalipa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) kwa ajili ya kuwaondoa wananchi walio pembezoni mwa barabara ili kupisha uwekaji wa nguzo za mkongo wa taifa, yalionekana kama utani kiasi cha kumwagiza mtendaji huyo kupeleka vielelezo hivyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuona iwapo malipo hayo yamewafikia wananchi kweli ama la.

  “Uamuzi wa kamati ni kwamba kuanzia Jumatatu tunawapa siku tatu ili mvipate vielelezo hivyo na kuviwasilisha kwa CAG ili akague malipo hayo kama kweli Tanroads waliwalipa watu ama vinginevyo,” alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo, Zainabu Vullu.

  Wizara nyingine ambazo ziliwekwa ‘kitimoto’ huku nyingine zikilazimika kurudishwa na kamati za Bunge ili zijipange upya ni pamoja na ile ya Fedha na Uchumi, Maliasili na Utalii, Ujenzi na Tamisemi.

  Wakizungumzia tuhuma hizo, vyama vya CHADEMA na CUF kwa wakati tofauti vimesema kuwa hali ya nchi ni mbaya na vimemtaka Rais Kikwete kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na hali mbaya ya uchumi inayolikabili taifa kwa sasa.

  Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika amekaririwa jana akisema kuwa, watanzania wengi na hasa vijana wamekata tamaa ya maisha na kama Rais Kikwete asipochukua hatua za haraka, hali ya amani itatoweka. Kauli ya Mnyika inafanana na iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ambaye mara mbili ameeleza wasiwasi ke juu ya tishio kubwa la uvunjifu wa amani, iwapo hali ngumu ya maisha na kukosekana kwa ajira kwa vijana hazitachukuliwa hatua za haraka kukabiliana na tatizo hilo.

  CUF kwa upande wao, kimesema kupanda kwa gharama za maisha na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ni ushahidi tosha kuwa Kikwete, ameshindwa kuiongoza nchi.

  Chama hicho kimemtaka mkuu huyo wa nchi akubali kusaidiwa na vyama vya upinzani kwa kuunda haraka serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Katika maazimio ya Baraza Kuu la Chama hicho yaliyosomwa jana mbele ya waandishi wa habari na Naibu Katibu Mkuu wake, Julius Mtatiro (Bara), CUF kimesema serikali ya CCM imeshindwa kutoa dira sahihi ya kukabiliana na hali mbaya ya uchumi, badala yake kila kiongozi aliyeko serikalini anafanya kazi ya kumnyooshea kidole mwenzake.

  CUF kimesema taifa lipo katika hali mbaya kwa sababu serikali haitaki kushauriwa na wataalamu na badala yake kutumia siasa hata katika masuala ya kitaalamu.

  Mtatiro, alisema Baraza Kuu limeshitushwa na hali ufisadi mkubwa unaoibuliwa na kamati za Bunge za ambapo mabilioni ya fedha za walipa kodi wanyonge zinaliwa na wajanja wachache bila wahusika kuchuliwa hatua za kisheria.

  “CUF tunamtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwakatama wahusika wote waliotajwa ili wafikishwe katika vyombo vya sheria kwa vile Rais Kikwete ameelemewa na ameshindwa kutatua matatizo makubwa yanayolikabili Taifa,” alisema Mtatiro.

  Baadhi ya wataalamu wa utawala na uchumi, wameliambia Tanzania Daima kuwa kama serikali haitaamua kuchukua maamuzi magumu ya kurekebisha hali mbaya ya uchumi, ipo hatari kubwa ya kuvurugika kwa amani nchini.
  “Watu waliokwiba fedha za umma wanajulikana, lakini hawakamatwi, huku watoto wa wakulima wakinyimwa fedha za mikopo ya elimu na wengine wakilazimishwa kutozwa ada kwa kulipa dola badala ya shilingi. Hii ni hatari, na sijui viongozi wanataka hali iweje ndipo wachukue hatua,” alisema mchumi mmoja mwandamizi anayefundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  BAK, you got to be mad, to be a sober Tanganyikan,

  CAG aangalie na matumizi ya miaka 50 ya Uhuru ambao haupo, hivi tumetumia shillingi ngapi mpaka sasa? Ilikuwa ni lazima kweli, kufanya hiyo adventure? Hizo hela zingekwenda kwenye elimu hasa vyuo vikuu tungekuwa wapi?

  Kila nikisoma magazeti najisikia kama vile kizunguzungu, Mfano ni Kasri la RC mtwara ambalo kwa miaka mitatu limekomba billioni moja na millioni mia nne
   
 3. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,596
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  mkuu naunga mkono hapo kwenye matumizi ya miaka 50 ya uhuru,mimi nafanya kazi za video production nimeona jinsi baadhi ya taasisi za serikali zinavyotoa hela kwa ajili ya hichi wanachoita documentary juu ya miaka hamsini ni wizi mtupu, kipindi cha tv cha dk 30 kinatengenezwa kati ya sh mil 4 na nusu mpaka mil 6 ukiangalia utengenezaji wa kipindi chenyewe na ubora wake hata ukipewa laki 5 unatengeneza na wala usipate hasara na hii ni tofauti na airtime ktk tv ambayo cjui wanaenda lilia bei gani ktk station.
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  A tip on the iceberb, allowance, time wasted,( not spent) etc etc
   
 5. g

  geophysics JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa ndio mwisho wa dunia ..2015 hatufiki...msiamini ngojeni.... 2015 dola moja itakuwa sawa na sh.3000 za tanzania.
  Rais na viongozi wa ngazi za juu wataendelea kuneemeka na kupata matibabu nje ya nchi... Mwananyamala, Temeke na Ilala hospitali watu wataendelea kufa kama Sodoma na Gomora....Let's wait and see
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,209
  Trophy Points: 280
  Mkuu NN, ndio matatizo ya kuwa na Serikali taahira ambayo haijui kabisa vipi vinastahili kuwa vipaumbele vyake. Wapo wapo tu hawana mipango yoyote inayoeleweka katika kuendesha Serikali. Angalia jinsi walivyovurunda kwenye ile Mkurabita.
   
 7. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,596
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  nadhani ulikuwa wamaanisha iceberg na sio iceberb, ok hapo kwenye allowance nakubali lkn time wastage nakataa coz hiyo alawansi c ndio imelipia huo muda uliopoteza au allowance ni nini labda mi ndio sielewi vizuri.
   
 8. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Watanzania sijui tuko je kweli. Kinachonishangaza ni kuwa wako mawaziri wanajua fika kuwa nchi inaenda kombo lakini badala ya kujiuzulu ili kuamsha ule umoja wa kitaifa na kutoa nafasi ya watu wanaostahili na kiongozi wa nchi kulazimika kuchukua hatua, wanbakia kulalama na kuongea kiaina aina ili waonekane wako kinyume nyume hivi, lakini wanaendelea kuwahi ofisini na kukaa tu ofisini bila kuzalisha chochote na kuendelea kuchota mshahara na kutumia magari nyumba na stahili nyingine kutoka migongo ya wananchi waliopigika na umaskini.

  Kwa kweli mtu kama Six, pombe, tiba nk wanafanya nini kwenye hii serikali sasa hivi?. Hivi kwanini nchi yetu viongozi hawajiuzulu?


  Mungu ibariki Tanzania!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  I can swear and bet that a larger part of the leadership do not know why they hold the positions. Unaamka asubuhi, unaambiwa kuanzia leo wewe ni RC, walllahi unaenda kuapishwa wala hujui majukumu yako. Unaamka asubuhi unateuliwa waziri wa wizara, unaapishwa hujui unaenda ofisini kufanya nini. Kwa sababu huna na hujui cha kufanya unabakia kutafuta safari kila mahali na kurudi bungeni kujibu maswali ya wabunge basi.

  Ukimess up hata kiongozi wako hajui kama umemess up hakufukuzi kazi badala yake anampa CAG ( mhasibu) achunguze kosa la jinai.

  Kwa sababu na yeye hajui yuko pale kufanya nin, walai hakata,i anachunguza na kwa sababu hajui kuwa hiyo sio fani yake naye anatoa wrong conclusion na ana mess up.

  Inaundwa tume nyingine kuangalia huyo bwana alivyomess up, basi ni kama paka anavyofukuza mkia wake. Ikifika miaka 50 ya uhuru tunashinda Mnazi Mmoja kucelebrate failures zetu kwa wiki kadhaa.

  This is Tanzania, where the unexpected always occurs and the expected never happens.
   
Loading...