RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Serikali imemnyanyang’anya mwekezaji wa kampuni ya Via Avition karakana ya kutengeneza na kutunza ndege iliyopo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kuirudisha kwa shirika la ndege ATCL kutokana na mwekezaji kulipa ushuru mdogo wa dola elfu tatu kwa mwezi huku yeye akiingiza malioni ya fedha hali iliyotajwa kuwa ni kuitia serikali hasara na ufujaji wa rasimali za Umma.
Akitoa maamuzi hayo waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbarawa aliyetembelea uwanja huo na miradi mingine ya wizara yake kukagua utendaji wa kazi amesema serikali imefika hatua hiyo baada ya mwekezaji kupewa miaka kumi ya uendeshaji wa karakara hiyo lakini amekuwa akilipa fedha kidogo na kuitia hasara serikali hiyo imeichuka na kuirudisha serikali kwani hakuna muda wa kufumbia macho hujuma za rasimali za umma.
Akizungumzia maamuzi hayo mwekezaji wa kampuni ya Via Aviation Suzani Machibe amesema kwakuwa shirika la ndege Tanzania ATCL halina uwezo wa kujiendesha kutoka na na uchache wa ndege zake walitumia karakara hiyo kwa matengenezo ya ndege ya mshirika mengine hivyo ameiomba serikali kutonyanyang’anya na badala yake waingine naye ubia kuendesha karakana hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Bakari Murusuru amesema watatekeleza maagizo ya serkali ikiwamo kukabiliana tatizo la upitwishaji wa dawa za kulevya pamoja na utoroshwaji wa nyara za serkali kwa kuimarisha ulinzi pamoja na kuweka mitambo ya kisasa katika uwanja huo.