Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
Waziri Maghembe alikabidhi tuzo hiyo juzi jijini Dar es Salaam na kusema serikali inatambua mchango mkubwa alioutoa, Dk. Goodall, katika uhifadhi wa sokwemtu pamoja na wanyama wengine.
Alisema Tanzania ni nchi ya uhifadhi kwa Bara la Afrika na inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa inatumia eneo kubwa kwa ajili ya kuhifadhi viumbe hasa wanyamapori na misitu.
Maghembe alisema katika hifadhi za taifa 16 zenye wanyama mbalimbali, kuna hifadhi mbili za Taifa, ambazo ni Gombe na Mahale zenye wanyama wanaohifadhiwa kwa asilimia kubwa wakiwamo sokwemtu na katika dunia hizo ndizo hifadhi zenye sokwemtu wengi kupita zote.
“Kazi aliyoifanya huyu mtaalamu kwa zaidi ya miaka 60 ni kufanya utafiti juu ya wanyama hawa na kujua ikolojia yao, mahitaji yao katika hifadhi, chakula, jinsi wanavyoishi na jinsi ambavyo wanashabihiana pamoja na kujua magonjwa yao, hivyo amefanya kazi kubwa na serikali imetambua mchango wake na kuamua kumpatia tuzo hiyo ,” alisema Maghembe.Alisema Dk. Goodall ametambua vitu vitatu vikubwa katika sayansi na kwamba alijua sokwemtu wana uwezo wa kujitambua, wana hisia zao kama za binadamu na wanatumia nyezo katika maisha yao katika kujitafutia vyakula vyenye aina ya protini.
Aidha, alisema mtaalamu huyo amekusanya takwimu ambazo zina maana kubwa katika uhifadhi wa sokwemtu na wanyamapori, ambazo zimefahamika kimataifa, hivyo msimamo wa serikali ni kuendeleza kazi aliyoifanya na kupanua taasisi ya utafiti ya wanyama.
Maghembe alisema kabla ya sokwemtu kufanyiwa utafiti walidhani binadamu yuko tofauti na mnyama huyo lakini ikabainika kuwa vinasaba vyao ni kama binadamu na asilimia 99 ni sawa na binadamu na kwamba tofauti ni kwamba ubongo wa binadamu ni mkubwa kuliko wa sokwemtu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Allan Kijazi, alisema tuzo hiyo amepatiwa kwa sababu ametumia zaidi ya miaka 60 kwa ajili ya kufanya utafiti na amesaidia kuwapatia taarifa za kutosha kuhusiana na mienendo na tabia za sokwemtu.
Alisema taarifa hizo zimewasaidia kuweka mikakati sahihi ya namna wanavyoweza kuwasimamia wanyama hao endapo zingekosekana taarifa hizo huenda idadi ya wanyama hao ingekuwa ni ndogo kuliko ilivyo sasa.
Kijazi alisema wanyama hao wanapenda kuishi katika mazingira ya asili hawatambui mipaka hivyo wamekuwa na tabia ya kutoka na kurudi hifadhini kutokana na kuhama kwao imesababisha idadi ya Sokwemtu kupungua na wengine kuuliwa.
Naye Dk. Goodall alisema amefurahishwa kwa tuzo hiyo na kwamba utafiti huo aliuanza katika mazingira magumu lakini ndoto yake imetimia huku akisisitiza umuhimu wa kutunza maeneo yenye uhifadhi.
Chanzo: Nipashe