Serikali yajigamba mafanikio Big Results Now

Serikali yajigamba mafanikio Big Results Now

Joined
Sep 12, 2012
Posts
18
Reaction score
7
Serikali imesema imepata mafanikio makubwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu mpango wa Big Results Now uanze kutekelezwa,

Mafanikio hayo yamepatikana katika secta ya Elimu, Kilimo, Nishati na Uchukuzi
-------------------------------------------------------------------------------
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira amesema Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), umepata mafanikio makubwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu ulipoanza kutekelezwa.

Wassira alisema hayo juzi alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha wa 2014/15.

Alisema mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ni kuongezeka kwa ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne kutoka asilimia 43.08 mwaka 2012 hadi asilimia 58.25 mwaka 2013.

"Ngazi ya elimu ya msingi ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 31 mwaka 2012 hadi asilimia 50 mwaka 2013. Tumeongeza maabara katika shule za kata, kuanza ukarabati wa shule kongwe za kitaifa na kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika shule 56 kati ya 264 za awamu ya kwanza," alisema.

Katika kilimo, alisema mafanikio ni kutoa mafunzo ya kuendesha skimu ya umwagiliaji kwa maofisa 95 na wakulima 95, kupata hatimiliki za mashamba makubwa mawili ya Bagamoyo na Mkulazi (Rufiji), kutoa hati za kimila kwa mashamba madogo 185 na kutoa mafunzo kuhusu biashara.

Wassira alisema katika nishati mafanikio yaliyopatikana ni wateja wapya 138,931 kuunganishiwa umeme ikilinganishwa na lengo lililowekwa la kuwaunganishia wateja 150,000 kwa mwaka 2013/14.

"Tumepunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 21 mwaka 2012 hadi asilimia 19 mwaka 2013," alisema.

Katika sekta ya uchukuzi, Wassira alisema Serikali imeongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuhudumia zaidi ya tani milioni 13, Desemba mwaka jana, ikilinganishwa na tani milioni 12, Desemba mwaka 2012.

"Katika Reli ya Kati, Serikali imekamilisha ujenzi wa madaraja matatu, uundwaji upya wa vichwa vitatu vya treni na kuendelea na uundaji wa vichwa vitano, kukamilisha malipo ya vichwa 13, mabehewa ya mizigo 274, mabehewa 34 ya breki na toroli 30 za umeme," alisema Wassira.

Alisema katika sekta ya maji, mafanikio ni ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 9,644 na kuhudumia wananchi milioni 2.3 waishio vijijini ikilinganishwa na watu 300,000 hadi 500,000 awali.

Katika ukusanyaji wa mapato, Wassira alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kutumia kifaa bora cha uthaminishaji wa bidhaa na kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Mpango huo wa BRN umegawanywa katika maeneo sita ambayo ni elimu, kilimo, maji, nishati, utafutaji wa rasilimali fedha na uchukuzi.

Chanzo: Mwananchi leo, 02 Mayt 2014
 
Labda kwenye mifuko yao!(Viongozi)
 
Serikali imesema imepata mafanikio makubwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu mpango wa Big Results Now uanze kutekelezwa,

Mafanikio hayo yamepatikana katika secta ya Elimu, Kilimo, Nishati na Uchukuzi

Chanzo: Mwananchi leo, 02 Mayt 2014

Kama imepata mafanikio makubwa kiasi hicho na sisi wananchi si tungekuwa tumeyaona?! Binafsi sijaona hayo mafanikio makubwa.

Kwenye Uchukuzi ni mafanikio gani yamepatikana wakati Mashirika ya Reli na Ndege yako taabani?!
 
Uchukuzi si Reli na Ndege tu kijana. Mafanikio ni ongezo la asilimia 14 ya ongezeko la tani za mizigo iliyosafirishwa kulinganisha na mwaka jana, hiyo eneo moja lakini kuna mambo mengi.
 
Serikali imesema imepata mafanikio makubwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu mpango wa Big Results Now uanze kutekelezwa,

Mafanikio hayo yamepatikana katika secta ya Elimu, Kilimo, Nishati na Uchukuzi

Chanzo: Mwananchi leo, 02 Mayt 2014

They are delusional!I thought those results on low IQ population of Tanzanians were biased and wrong,but guess what?The twats in this administration have proven me wrong!!!!
 
Serikali imesema imepata mafanikio makubwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu mpango wa Big Results Now uanze kutekelezwa,

Mafanikio hayo yamepatikana katika secta ya Elimu, Kilimo, Nishati na Uchukuzi

Chanzo: Mwananchi leo, 02 Mayt 2014

Viongozi wetu wanajua kuwa hakuna BIG RESULT YOYOTE iliyopatikana. BIG result niliyoiona ni sherehe za muungano basi! Serikali yetu huwa iko very active kwenye mambo simple simple simple tu, mfano ziara na maadhimisho. Vingine vyote ni zero.

Wanachofanya sasa ni kuwa laghai wananchi kuwa mafanikio yamepatikana huku hata wao wakijua hakuna chochote cha maana. Mbavu zenu!
 
Huu ni unafiki wa kawaida tu huku serikalin> BIG results kwenye elimu kisa yale matokeo ya div 5!! Najua yote haya ni kumridhisha mfadhili tunaemwabudu kila siku. Hakika Hii nchi si HURU, bado tu watumwa kwa kuwa tunatumikia matakwa ya mzungu na mmarekani, mcina na mjapan. BIG RESULTS MATUMBO YENU TU
 
Jana JK aliambiwa, ukuaji wa Uchumi (Ki takwimu) hauendani na kupungua kwa umaskini! Haya nayo ya BRN ni namba tu, hakuna impact so far!. Usanii bongo kama kawa.
 
Uchukuzi si Reli na Ndege tu kijana. Mafanikio ni ongezo la asilimia 14 ya ongezeko la tani za mizigo iliyosafirishwa kulinganisha na mwaka jana, hiyo eneo moja lakini kuna mambo mengi.

hamna kitu hapo ...takwimu za biashara zao vigogo wa intarahamwe....
 
Mafanikio kwenye elimu nimeona kuongezeka kwa div 5 na vitabu vilevile,wanafunzi kuendelea kukaa chini,shule kutokuwa na walimu wa kutosha,shule nyingi kutokuwa na maabara.Hongera BRN kwa mafanikio yaliotukuka.
 
Uchukuzi si Reli na Ndege tu kijana. Mafanikio ni ongezo la asilimia 14 ya ongezeko la tani za mizigo iliyosafirishwa kulinganisha na mwaka jana, hiyo eneo moja lakini kuna mambo mengi.

Duniani kote usafirishaji wa Reli ndiyo unabeba asilimia kubwa zaidi ya mizigo.

Reli yetu imeporomoka toka kubeba tani 1,500,000 miaka kabla ya 2007 hadi chini ya tani 400,000 miaka ya karibuni. Hilo ongezeko unalosema limechangiwa na nini?
 
Yote yanayojiita maserikali ni majinga tu...yanatuhadaa na vijimaneno vya shombo wakati yanabaki kunenepena yenyewe na miubinafsi yao.
 
Back
Top Bottom