Serikali yaiagiza TRL kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

“Kama Serikali tumewekeza vya kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata bidhaa na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.

Amesema Serikali imedhamiria kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya usafiri wa reli hapa nchini.

“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Amezungumzia umuhimu wa TRL kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za ajira na kukuza pato la shirika na taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la Tanganyika.

“Tumieni fursa ya kuwa karibu na nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate mzigo wa kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ambaye yupo katika ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa nyingi za kibiashara.
 
hapa pana uchafu wa kutisha sana ! vichwa vya treni vinavyokarabatiwa na wa Thailand inasemekana bei ya ukarabati wa kichwa kimoja ni 3.5 bil na wakati huo kununua kipya cha kisasa kutoka south africa ni 5bil only , kuna taarifa kwamba pamoja na kwamba tunalipa bilion tatu unusu lakini karakana zinazotumika ni zetu na sisi ndio tunaolipia usafiri na ushuru wa kila kitu , wadau eneo hili linatakiwa kufunuliwa ili kila mwananchi alijue .
 
Mv Liemba meli ina zaidi ya miaka 100,ililetwa na wajerumani.Ahadi ya Kikwete kununua meli mpya iliisha kama mshumaa
 
Serikali imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

“Kama Serikali tumewekeza vya kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata bidhaa na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.

Amesema Serikali imedhamiria kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya usafiri wa reli hapa nchini.

“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Amezungumzia umuhimu wa TRL kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za ajira na kukuza pato la shirika na taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la Tanganyika.

“Tumieni fursa ya kuwa karibu na nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate mzigo wa kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ambaye yupo katika ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa nyingi za kibiashara.

Mie napenda kumkumbusha Mh. Waziri kuwa chanzo cha matatizo ya meli za shirika la Marine Services Co. ambayo iko chini ya wizara yake linachangiwa na vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia usalama wa vyombo hivi. Pamoja na SUMATRA kukagua meli hizi, bado kuna watumishi wa SUMATRA wasio waaminifu ambao hutumia mamalaka waliyopewa kujinufaisha wenyewe. Ni ukweli usiopingika kuwa Wakaguzi wa meli za shirika hili pamoja na meli nyingine za watu binafsi zinazofanya safari zake kwenye maziwa yetu matatu, (Victoria, Tanganyika na Nyasa) wamekuwa wakipokea rushwa ili waandike report nzuri kwa vyombo ambavyo havina sifa na viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanya safari zake. Tatizo jingine linaloikabili kampuni ya Marine service ni baada ya kampuni hii kuwekwa chini ya uangalizi wa Tumpe Mwaijande ambaye ni Director wa Maritime safety and security. Huyu Mama ni mtu hatari sana, na ni mtu ambaye huweka maslahi yake binafsi mbele. Mama huyu alihusika kwa kiasi kikubwa kuuza vyeti vya mabaharia na kujipatia pesa nyingi zisizo halali. Hujuma hii alifanya takribani miaka 7 (1995-2002) alipogundulika kuwa alikuwa akiuza vyeti vya mabaharia kwa watu ambao hata hawajasomea fani hiyo. Cha ajabu baada ya kugundulika alihojiwa tu na tume iliyoundwa na waziri wa wakati huo Mh. Prof. Mark Mwandosya, lakini aliokuwa akishirikiana nao kufanikisha wizi huo ambayo walikuwa waajiriwa wa chuo cha Mabaharia ( Mzee Macho na Bwana Rajabu) walifukuzwa kazi.
Hivyo basi Mh. Prof. Mbawara inabidi ufahamu kuwa watu ambao wamehusika kwa kiasi kikubwa kufisilisi haya mashirika TRL na Marine services Co. wako hapo wizarani kwako.

Kuhusu SUMATRA, ningependa kusema kuwa imeshindwa kusimamia ubora vya vyombo vya majini. Badala yake wamekuwa wapiga deal tu. Kwa mfano sheria inasema kuwa chombo cha majini (Meli) itaongozwa na nahodha aliyepitia mafunzo ya kuongoza meli na awe na lesseni kwa ajili ya kazi hiyo. Pia wafanyakazi wote melini lazima wawe wamepitia mafunzo ya ubaharia (Basic safety training) yanayotolewa na chuo kinachotambuliwa na shirika la umoja wa mataifa IMO. Lakini vyombo vyetu vingi (hasa huko kwenye Maziwa yetu) vina wafanyakazi wasio na sifa. Baadhi ya vyombo vina Manahodha wasio na lesseni au wana lessen fake, na wafanyakazi wengine hawajapitia mafunzo ya ubaharia kabisa. Mfano Kuna Meli huko ziwa victoria inaitwa Super Summa inafanya safari zake kutoka Mwanza mjini kwenda Kamanga na wakati mwingine husafirisha abiria kati ya Mwanza na Nansio Ukerewe. Meli hii asimia 90 ya wafanyakazi wake hawana vyeti kabisa. Chief officer hana lesseni (alisoma chuo cha bahari kafeli hivyo hakupata lesseni). na wafanyakazi wa kada ya chini hawajapitia mafunzo yoyote ya ubaharia. Cha kusikitisha ni kwamba SUMATRA wanalijua hili, na wanajua madhara ya kuruhusu watu wasio nasifa kuongoza meli.

Najua Mh. Waziri Prof. Mbawara wewe pia ni baharia, ni matumaini yangu kuwa unajua sheria na kanuni za ubaharia.
Napenda kuchukuwa nafasi hii kukukumbusha kuwa wakumbushe SUMATRA wasimamie sheria za usafiri wa majini.
Kuanzia ships seaworthiness to Manning. Wasisubiri mpaka ajali zitokee ndo waanze kuunda tume za kuchunguza wakati wangechukuwa hatua mapema.
 
Mungu akuepushe na vitu vyenye ncha kali .
 
Back
Top Bottom