Serikali yagawa hati za viwanja 4,333 Ubungo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amegawa hati za viwanja 4,333 ambavyo vimekamilika kupimwa katika Kata ya Kilungule A, Manispaa ya Ubungo huku hati 88 zikikabidhiwa papohapo kwa wananchi.

Waziri Lukuvi alisema jana kuwa kumekuwa na ubadhirifu wa baadhi ya watendaji katika halmashauri, kwa kukwamisha vibali vya ujenzi kwa wananchi ili kuendesha shughuli za maendeleo.

“Wananchi wanatakiwa kupewa vibali vya ujenzi ndani ya wiki moja baada ya kukamilisha umilikishwaji wa ardhi ambayo tayari imeshapimwa na kupangiwa matumizi maalumu, kwa watendaji wa halmashauri hasa kamati za ujenzi kukwamisha mpango huu iwe mwisho,” alisema.

Alifafanua kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam wananchi wengi wanaishi katika maeneo ambayo hayajapimwa na kupangiwa matumizi maluumu, huku asilimia 25 ndiyo wanaoishi maeneo yaliyopimwa.

“Watu ambao wamejichukulia maeneo kiholela wataanza kulipa kodi ya majengo, kwa kuwa wanatumia miundombinu ya Serikali na manispaa,” alisema.

Pia, alifafanua kuwa Serikali imepunguza bei za urasimishwaji wa ardhi kwa asilimia 67.

Mbali na hilo, aliwataka watendaji wa Halmashauri ya Ubungo kuzungumza na mmiliki wa eneo la Twiga lililoko Kimara Baruti ambalo limetelekezwa bila kuendelezwa ili lipangiwe matumizi mengine ya maendeleo.

“Halmshauri kupitia mkuu wa wilaya zungumzeni na mmiliki huyo kama kuna fidia muanze kulipa kidogokidogo, au aeleze mpango wa eneo hilo akibisha nina uwezo wa kulichukua maana hatuwezi kukubali mtu amiliki eneo bila kuliendeleza wakati kuna huduma lukuki zinahitajika kwa wananchi,” alisema Waziri Lukuvi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi, Profesa John Lupala alisema Serikali imekusudia kutoa hati za viwanja 400,000 kila mwaka nchini.

Naye Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob alisema wananchi kupatiwa hati hizo itaisaidia halmashauri kuongeza kipato kwa kuwa watu wameongezeka katika mpango rasmi.

“Halmashauri itaongeza kipato chake kupitia kodi ya majengo huku asilimia 20 ikiingia katika mfuko wake, fedha znazobaki zinaingia katika mfuko wa Serikali,” alisema Jacob.

Mnufaika wa mpango huo, Baton Kiha alisema Serikali imemkomboa kwa kuwa hakuwa na uhakika wa kuendesha biashara zake, hivyo kupitia hati hiyo ana uwezo wa kukopa kwenye taaususu za fedha.

Chanzo: mwananchi
 
Akakope kistaarabu wasije wakaichukua iyo nyumba
 
Back
Top Bottom