Serikali yafuta vibali vyote vya makampuni ya uwindaji vilivyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka huu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
30fe3a4e5a38f03d1b0bc5f475a66708.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Oktoba 22, 2017 amefuta vibali vyote vilivyotolewa na wizara yake vya uwindaji wa makampuni ili kuwa na utaratibu mpya wa uombaji kwa njia ya mnada.

Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo jioni hii wakati wa kuhitimisha mazungumzo yake na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii na Maliasili aliokutana nao mjini hapa Dodoma.

"Kwa mamlaka niliyonayo. Natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa makampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia naagiza watendaji wote wanaosimamia ili, wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mchakato huo wa mnada ufanyike na uwe wa wazi ", alieleza Dkt. Kigwangalla.

Pia ametoa onyo na maagizo mazito kuhakikisha kuwa vitalu vyote vyenye migogoro ikiwemo vile vya Loliondo, Natroni na maeneo mengine kutotolewa kwa vibali vya uwindaji mpaka hapo watakapokamilisha tatizo la migogoro hiyo.

Aidha, ametoa agizo kwa hoteli 10 zilizobinafsisha kutoka Serikalini zirejeshwe ndani ya siku 60 kuanzia sasa huku akiagiza watendaji waandike barua kwa msimamizi wa hazina.
 
Hatua hii ni chanya na itaongeza mapato yatokanayo na uwindaji wa kitalii. Wakati wizara ikiandaa mnada ni vyema ikapitia upya madaraja ya vitalu hasa vile vilikuwa vimevamiwa na wafugaji na wakulima ambao sasa wanatolewa katika misitu na "game reserves" na maeneo ya WMAs. Msimu wa uwindaji ubaki miezi Sita (Julai hadi Desemba) kila mwaka. Mgao wa mapato kwa
WMA yatokanyo na ada za wanyama upande hadi 70% ili jamii zinazohifadhi maeneo haya zinufaike kwa kuboresha huduma za jamii na uchumi wa kaya
 
Nasikia kajiapiza kuwa hawezi kung'oka pale Utalii na Maliasili, akumbuke tu wengi wamepita hapo.
 
Kwan vibali vya mwanzo waligawiwa bure je utaratibu ukoje kwa gharama za vibali vya mwanzo...uyu waziri anajua io wizara ndo machinjio ya wasiotakiwa
 
tusubiri kulipwa fidia ya usumbufu maana aliyetoa alikuwa na mamlaka kama yakwako
 
Nasikia kajiapiza kuwa hawezi kung'oka pale Utalii na Maliasili, akumbuke tu wengi wamepita hapo.
Vitalu ndio vilikuwa vinawang'oa wengi..nyalandu vimemtajirisha sana hivyo..huyu kauona huo mtego mwanzoni kabisa..kwa hilo tamko kigwangalah angekuwa fisadi kama kina nyalandu hadi kesho asubui angekuwa billioni wa kutupwa
 
30fe3a4e5a38f03d1b0bc5f475a66708.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Oktoba 22, 2017 amefuta vibali vyote vilivyotolewa na wizara yake vya uwindaji wa makampuni ilikuwa na utaratibu mpya wa uombaji kwa njia ya mnada.

Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo jioni hii wakati wa kuhitimisha mazungumzo yake na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii na Maliasili aliokutana nao mjini hapa Dodoma.

"Kwa mamlaka niliyonayo. Natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa makampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia naagiza watendaji wote wanaosimamia ili, wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mchakato huo wa mnada ufanyike na uwe wa wazi ", alieleza Dkt. Kigwangalla.

Pia ametoa onyo na maagizo mazito kuhakikisha kuwa vitalu vyote vyenye migogoro ikiwemo vile vya Loliondo, Natroni na maeneo mengine kutotolewa kwa vibali vya uwindaji mpaka hapo watakapokamilisha tatizo la migogoro hiyo.

Aidha, ametoa agizo kwa hoteli 10 zilizobinafsisha kutoka Serikalini zirejeshwe ndani ya siku 60 kuanzia sasa huku akiagiza watendaji waandike barua kwa msimamizi wa hazina.
Serikali Iangalie kwa makini hatua wanazozichukua kwasasa bado tuna vita vya Madini halafu tunaanzisha vita kwenye utalii. Naona hii ni Perestroika ya Tanzania
30fe3a4e5a38f03d1b0bc5f475a66708.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Oktoba 22, 2017 amefuta vibali vyote vilivyotolewa na wizara yake vya uwindaji wa makampuni ilikuwa na utaratibu mpya wa uombaji kwa njia ya mnada.

Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo jioni hii wakati wa kuhitimisha mazungumzo yake na wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii na Maliasili aliokutana nao mjini hapa Dodoma.

"Kwa mamlaka niliyonayo. Natamka kwamba, nafuta rasmi vibali vyote vya uwindaji kwa makampuni vilivyotolewa na wizara yangu kwa mwaka huu. Pia naagiza watendaji wote wanaosimamia ili, wahakikishe wanaandaa mchakato ndani ya siku 60 ili mchakato huo wa mnada ufanyike na uwe wa wazi ", alieleza Dkt. Kigwangalla.

Pia ametoa onyo na maagizo mazito kuhakikisha kuwa vitalu vyote vyenye migogoro ikiwemo vile vya Loliondo, Natroni na maeneo mengine kutotolewa kwa vibali vya uwindaji mpaka hapo watakapokamilisha tatizo la migogoro hiyo.

Aidha, ametoa agizo kwa hoteli 10 zilizobinafsisha kutoka Serikalini zirejeshwe ndani ya siku 60 kuanzia sasa huku akiagiza watendaji waandike barua kwa msimamizi
 
Serikali Iangalie kwa makini hatua wanazozichukua kwasasa bado tuna vita vya Madini halafu tunaanzisha vita kwenye utalii. Naona hii ni Perestroika ya Tanzania
Vita ya kiuchumi haieleweki ni vurugu vurugu tu,no action plan and how to execute it
 
Back
Top Bottom