Serikali yaanza kujenga kiwanda gesi Mtwara

Serikali yaanza kujenga kiwanda gesi Mtwara

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
HATIMAYE ujenzi wa kiwanda cha kusafisha gesi kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam umeanza mkoani Mtwara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation (CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.

"Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park," alisema Maswi.

Alisema baada ya ziara hiyo kushindwa kufanyika Jumapili iliyopita, uongozi wa wilaya ulikutana na viongozi wa kijiji na kufikia mwafaka uliofanikisha kuanza kwa ujenzi huo.

Alisema kuanzia mradi huo kutatoa ajira za kawaida kwa wakazi saba wa maeneo yanayozunguka mradi huo na kwamba kazi hiyo itaongeza mahitaji ya bidhaa mbalimbali na huduma katika Kata ya Msimbati

"Mathalan kuku, matunda na mboga za majani vinahitajika sana. Sasa wananchi ambao awali, hawakutaka kuelezwa lolote, wameanza kuchangamkia fursa hizo jambo ambalo litawanufaisha zaidi," alisema.

Ujenzi huo ulielezwa kuwa unatekelezwa sambamba na mwekezaji kujenga visima vitatu vya maji safi na salama kijijini Madimba.

Alisema mwekezaji pia atasambaza umeme kwa kaya 300 za ndani na jirani ya kijiji hicho na kwamba vifaa vitakavyotumika katika kazi hiyo vinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.

Maswi alisema shule zote kwenye Kata ya Msimbati kikiwamo Kijiji cha Madimba, zitakarabatiwa na mwekezaji huyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa wananchi waishio maeneo ya mradi kunufaika na uwekezaji.

Hata hivyo, habari nyingine zinaeleza kuwa ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo la mradi ili kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwapo.

Mgawo wa umeme
Akizungumzia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo mengi nchini hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa kuna mgawo wa umeme kinyemela, Maswi alisema kamwe Taifa halitaingia gizani.


Alisema kukatika kunakotokea sasa kumesababishwa na kazi za kiufundi zilizotarajiwa kukamilika jana jioni... "Kwa taarifa nilizonazo, mtambo mdogo uliopo Ubungo unabadilishwa na kuwekwa mkubwa, pia Kipawa kuna matengenezo ya transfoma ili kuwezesha usambazaji wa umeme hadi Kisarawe na nyie mnaweza kwenda mkashuhudia kinachoendelea."

Hata hivyo, taarifa kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma, Morogoro, Arusha na Mwanza zinasema kumekuwa na tatizo kubwa la umeme kwa wiki mbili sasa.

 
Vizuri lakini MBONA ni WACHINA? ni MIKOPO ya KICHINA baada ya kuona contract yao ya WIZI ya BOMBA itakufa hapo itabidi kila kitu kama spare vinunuliwe CHINA ni sawa na MATATIZO YA TAZARA tuliyo nayo Wamejenga kitu kisichokuwa na International Standrs only Chinese can replace it...
 
Huu ndio upumbavu mimi huwa nakataa
Rais Jakaya Kikwete akiangalia shughuli za uzalishaji umeme hivi karibuni, baada ya vutanikuvute ya muda mrewfu Serikali imeamua kujenga kiwanda cha gesi mkoani Mtwara

Ujenzi huu sio zao la vuta nikuvute, hata mwanzo kiwanda hiki ilikuwa kijengwe hapo hapo, tatizo lilikuwa ni mizozo ya fidia za mashamba ya watu huko Msimbati. Sasa mwandishi anaandika kipuuzi namna hii kiasi inaonekana kwamba labda kiwanda hicho kilipangwa kujengwa sehemu nyingine na sasa ujenzi umehamishiwa hapo.
 
Miandishi ya kibongo bana,anataka watu waamini kuwa hakikupangwa kujenga hapo ila jana ndo serikali imeamua kijengwe hapo,na tayari wameanza kujenga.
 
Hii issue ya social coperate responsibility upuuzi mtupu ni sawa na kutegemea fadhila za muwekezaji. Muda umefika wadau wote washirikishwe kwenye mikataba ili makubaliano yawe na nguvu kisheria.
 
ina maana mkataba wa ujenzi wa bomba kuja Dar es Salaam/Bagamoyo (the inflated cost) haupo tena yaani umevunjwa!!!????
 
Akizungumzia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo mengi nchini hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa kuna mgawo wa umeme kinyemela, Maswi alisema kamwe Taifa halitaingia gizani.


Lol, hii nchi jamani....
Hayo maneno ya mtaalamu hayo na sio mwanasiasa.......
Kwani wenzetu wanatafsiri vipi kuwa gizani??

Tuache ngonjera umeme haupo stable, hata Dar hapa umeme unazingua sana..... kwa wiki ya 3 mfululizo sasa.....
 
Back
Top Bottom