Serikali yaanza kuifumua sera ya elimu ya 2014

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo akizundua ripoti ya Elimu tuitakayo iliyoandaliwa na taasisi ya Haki Elimu leo, Dar es Salaam


Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo amesema Serikali imeanza kuifanyia marekebisho sera ya elimu ya mwaka 2014 kufuatia maoni ya wadau wa elimu ili iende na wakati.

Akizindua ripoti ya elimu ya 'Elimu Tuitakayo' iliyoandaliwa na taasisi ya HakiElimu leo Alhamisi Aprili 29, 2021 mkoani Dar es Salaam, Dk Akwilapo amesema mchakato huo utashirikisha wadau wote ili kuondoa malalamiko.

"Serikali inadhamiria kufanya marekebisho ya sera ya elimu ya mwaka 2014, wadau wote wa elimu watashirikishwa kwa sababu elimu ni suala la jamii, sisi Serikali ni wasimamizi tu," amesema Dk Akwilapo.

Amesema ripoti hiyo itasaidia kuainisha maeneo yenye upungufu katika sera hiyo.

"Naamini mchango wenu utasaidia katika mchakato unaoendelea. Maudhui yaliyomo yatasaidia kuboresha yakiwemo mafunzo na upatikanaji wa miundombinu," amesema.

Akizungumzia utoaji wa elimu bila malipo, amesema sera hiyo imesaidia kuongeza udahili wa wanafunzi.

"Katika miaka sita ya utekelezaji wa sera hii kumekuwa na ongezeko la udahili la wanafunzi, hata hivyo kumekuwa na changamoto za ubora. Serikali inaendelea kuzitatua ikiwa pamoja na ujenzi wa miundombinu na kupeleka vifaa," amesema.

Awali, mkurugenzi wa HakiElimu, Dk John Kalage ameishukuru Serikali kwa kuipitia upya sera hiyo akisema walishapeleka upungufu na mapendekezo yao.

"Miezi sita baada ya kuzinduliwa sera hiyo mwaka 2015 HakiElimu tulitoa andiko la kuonyesha maeneo yenye upungufu,” amesema.

Amebainisha kuwa miongoni wa upungufu wa sera hiyo ni elimu kushindwa kutatua tatizo la ajira kwa vijana, “tumekuwa tukiwaambia vijana wajiajiri, watajiajirije wakati elimu waliyopata kwa miaka 10 au 16 haikumsaidia?”
 
Back
Top Bottom