Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Gharama za usafiri wa anga nchini zinatarajiwa kupungua kutokana na serikali kujiandaa kuliwezesha Shirika la Ndege nchini (ATCL), kuwa na ndege zake lenyewe.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua kiwanja cha ndege cha nduli Mkoani Iringa na kubainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kiasi cha shilingi bilioni 500 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.
Aidha Prof Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Mkoani Iringa Bi Hana Kibupile kuhakikisha kwamba uwanja wa ndege wa Iringa unafanya kazi katika viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuvutia wasafiri wengi wanaoelekea hifadhi ya Ruaha kutumia uwanja huo na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake meneja ya uwanja, Bi. Kibopile amesema licha ya ongezeko la abiria wanaotumia kiwanja hicho bado changamoto za ubovu wa kiwanja hasa kwenye Barabara ya kuruka na kutua ndege imekuwa ni sababu ya ndege kubwa kushindwa kutua kwenye kiwanja hicho.