Serikali ya walimu haina urafiki na walimu

BABA-D

JF-Expert Member
Jul 23, 2015
1,216
996
Tunaipongeza serikali ya Mheshimiwa Mwl MAGUFULI pamoja na Mheshimiwa Mwl MAJALIWA kuendelea kutumbua majipu na hvyo kupelekea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Katika hatua nyingine walimu wengi walio makini wanajiuliza kama serikali ya walimu (MAGUFULI na MAJALIWA) inayo nia ya dhati ya kushughulikia matatizo ya walimu.

Mfano: Walimu wa manispaa ya ILEMELA-MZA, Halmashauri ya IFAKARA na Halmashauri URAMBO na halmashauri nyingi tu bado wanadai hela zao za kusimamia mtihani wa kidato cha nne.
Kibaya zaidi hakuna aliyejitokeza kusemea tatizo hlo.

Tunajiuliza au dhana ya KAZI TU bila POSHO imehamia kwa walimu?

Halafu tunaona ni maajabu sana kama inawezekana kulipwa kwa wasimamizi wa kidato cha pili na hata wasahihishaji. (KIPAUMBELE NI NINI)
Tunaomba sasa tufahamishwe kinachoendelea
 
Walimu watafanya kazi kwa vinyongo rohoni mwisho wa yote watapatikana vilaza kwenye maofisi
 
Mishahara yao midogo,halafu haina usawa kulingana na viwango vya elimu ya mtu husika.Jamani walimu! Wagosi wa kaya njoni
 
Hii ndio fani isiyo tambua merit za watu ingawa ndio inayofundisha watu wawe na merit. Hvi unaposhidwa kuitambua Masters na PhD katika ualimu utaitambua wapi? Huwa siielewi serikali yangu badala ya kutumia weledi na manguri na wabobevu wa kufundisha darasani wao wapo tu na nyaraka zao kandamizi. MTU unajilipia mwenyewe Masters or PhD ya ualimu unarudi unamkuta mwajiri kwa dharau anakwambia ulisoma kwa manufaa yako na yye mwajiri ana degree sana Masters. Kiukwel waheshimiwa liangalieni hili
 
Madeni ya walimu kwa ujumla ni donda ndugu ambalo linaelekea kuwa kansa. Tunaomba serikali ya awamu ya tano ishughulikie ulipwaji wa madeni yote ya walimu bila kubagua. Ili walimu waweze kulipwa madeni yao yote tunaomba watu wa TAMISEMI wake kuhakiki madeni hayo badala ya kuwatumia wakuu wa idara na waajiri ambao kwa makusudi hupoteza nyaraka za madeni ili walimu hao wasilipwe na kutoa taarifa za bongo kuwa ktk halmashauri flani hakuna walimu wanaoidai serikali. Inauma sana.
 
Tunaipongeza serikali ya Mheshimiwa Mwl MAGUFULI pamoja na Mheshimiwa Mwl MAJALIWA kuendelea kutumbua majipu na hvyo kupelekea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Katika hatua nyingine walimu wengi walio makini wanajiuliza kama serikali ya walimu (MAGUFULI na MAJALIWA) inayo nia ya dhati ya kushughulikia matatizo ya walimu.

Mfano: Walimu wa manispaa ya ILEMELA-MZA, Halmashauri ya IFAKARA na Halmashauri URAMBO na halmashauri nyingi tu bado wanadai hela zao za kusimamia mtihani wa kidato cha nne.
Kibaya zaidi hakuna aliyejitokeza kusemea tatizo hlo.

Tunajiuliza au dhana ya KAZI TU bila POSHO imehamia kwa walimu?

Halafu tunaona ni maajabu sana kama inawezekana kulipwa kwa wasimamizi wa kidato cha pili na hata wasahihishaji. (KIPAUMBELE NI NINI)
Tunaomba sasa tufahamishwe kinachoendelea

Ukishaitwa mwalimu ujue ni shida tu
 
LOWASSA angekua Rais labda sawa maana ni mtu anaesikiliza changamoto za watu lakini uyu Walimu mtaisoma namba na mtamkumbuka Shemeji yenu KIKWETE maana ktk utawala wake aliweza kuongeza mishahara na kujari madaraja zaidi ya 250% sasa kila mtumishi ebu aache inafiki ajiangalie ktk legacy ya Mkwere mshahara wake umepanda kwa % ngapi? ktk legacy ya Mkwere maendeleo yake binafsi yapoje ikilijganishwa na legacy ya MKAPA? Watu washaanza kumkumbuka MKWERE maana kila mwez wa saba ilikua lazima baba wa watu afanye kitu achilia madaraja ya kitukishi...Ngoja tumsubirie uyu lakini wanaomjua wanasema watumishi IMEKULA KWAO
 
Back
Top Bottom