Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 4,315
- 10,017
Wanabodi,
Huu ni utafiti mdogo nilioufanya katika mwenendo wa fedha ndani ya serikali ya Rais JPM.
Ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya mwisho, serikali ya Rais Kikwete iliajiri takribani waalimu elfu 31 kwa kila mwaka ambapo ndani ya miaka mitatu waalimu zaidi ya elfu 80 waliajiriwa.
Katika kipindi cha miaka mitatu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli serikali imezibana ajira za ualimu na kumekuwa na upungufu wa takribani waalimu 40 au zaidi ukilinganisha na wale walioajiriwa katika miaka mitatu ya mwisho ya utawala wa Kikwete.
Kwa average mwalimu mmoja analipwa mshahara wa Tsh 500,000 kwa mwezi na hivyo kufanya alipwe 6,000,000 kwa mwaka.
Walimu elfu 40 ambao ajira zimefutwa ina maana serikali imeokoa takribani Tsh bilioni 720 za mishahara ambayo ilipaswa kutumika kulipa waalimu hao elfu 40 ndani ya miaka mitatu.
Hilo ni eneo moja tu la ubanaji wa matumizi.
Serikali inajitapa kujenga hospitali za wilaya 67 nchi nzima. Ambapo ukipiga hesabu ni hospitali moja imegharimu bilion 1.5 hivyo hospitali zote zimegharimu takriban billion 100 na milion 500 za Kitanzania.
Vilevile, serikali inajitapa kujenga vituo vya afya 400 nchi nzima. Wastani wa gharama za ujenzi wa kituo cha afya ni tsh milion 600 ambapo kwa vituo vyote serikali imetumia zaidi ya Tsh bilioni 240.
Ukijumlisha gharama hizo utakuta serikali imetumia si zaidi ya billion 350 katika ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za wilaya nchi nzima.
Ninachotaka kusema ni kwamba Serikali hii ukiichunguza kwa makini ni serikali ya kifisadi maana hizo zote zilizotumika katika ujenzi huo hazizidi hata nusu ya pesa zilizookolewa kwenye eneo moja tu la mishahara ya waalimu ambao wangeajiriwa.
Zipo sehemu nyingi fedha zimeokolewa hivyo kuna walakini mkubwa katika matumizi ya fedha za umma kipindi hiki cha utawala wa Rais Magufuli.
Kuna fedha lukuki zimekopwa ambazo ni tsh trilion kadh, kuna fedha kutoka kwenye makusanyo ya kodi sekta binafsi, kuna fedha kutoka kwa wahisani n.k
mvuv