Serikali ya Rais Magufuli inavyosifiwa mitaani, hakika Upinzani utakuwa na wakati mgumu

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika mwaka jana na Dr. John Pombe Magufuli kuchsguliwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanazuoni na mwanachama wa ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo alinukuliwa akisema na hapa nanukuu "WAPINZANI TUKITAFUTA UMAARUFU KWA KUTEGEMEA MAKOSA YANAYOFANYWA NA SERIKAI YA CCM, KIPINDI CHA JPM TUNAWEZA KUWA NA WAKATI MGUMU" mwisho wa kunukuu.

Hakika nimeanza kuona ukweli wa maneno haya ya Prof. Kitila Mkumbo. Leo nikiwa ndani ya magari yetu ya kusafiria maarufu kama DALADALA nikitokea Mbagala Kwenda Kariakoo, kwa muda wote abiria walikuwa wakitoa maoni yao juu ya Serikali ya Magufuli na siasa zinazofanywa na vyama vya upinzani na hasa CHADEMA kwa mgongo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA).

Ninukuu tu baadhi ya yale yaliyowagusa wananchi hao:

1. Wapo wanaosema hawanielewi, nami nasema watanielewa tu-wananchi hao wakinukuu maneno ya Mh. Rais akiwa kwenye mikusanyiko mbalimbali.

2. Siku hizi bwana hakuna cha mtu kukamatwa na akasema "Unajua mimi ni nani". Wananchi wanakiri kuwa hakuna aliye juu ya sheria na hasa jeshi la polisi linapotekeleza majukumu yake.

3. Wanachokifanya CHADEMA, kugomea vikao vya bunge, kulishtaki jeshi la polisi na kudai maandamano kwa nguvu ni kutaka tu nao waonekane bado wana nguvu na kutaka kupunguza nguvu ya Magufuli maana kero zote walizozipigia kelele ndizo anapambana nazo.

4. Haya matatizo ya ukosefu wa sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa fedha unaonza tarehe moja Julai ambapo kila wizara itapewa fungu lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri sana ana uhakika pesa ameshakusanya ya kutosha na ndiyo maana hata hawa Wazungu wakimletea za kuleta anawapotezea.

5. Hivi sasa wanaofanya maendeleo ni wale wanaopata pesa kihalali, majipu yote hivi sasa hayana chao.

6. Siku hizi kesi zikikaa sana ni siku saba hukumu inatolewa. Si ulimsikia wakati alipokutana na wafanyakazi wa Mahakama alivyoongelea inakuaje watu wanakamatwa na vidhibiti lakini unaambiwa uchunguzi bado unafanyika, uchunguzi gani wakati mtu kakamatwa na madawa ya kulevya?

7. Hospitalini sasa hivi ukienda unapokelewa kama mfalme na lazima upate dawa. Nyie acheni jamani tuliteseka sana.

8. Wafanyakazi zamani walikuwa wanakwenda kazini muda wanaotaka na wakati mwingine walikuwa wakiona wamechelewa wanapiga simu na kuomba wasainiwe halafu hawaendi.

Hayo ni badhi tu ya yale yaliyokuwemo kwenye mazungumzo ya abiria ndani ya daladala. Kiukweli wananchi wana imani kubwa sana serikali ya JPM.

Jambo ambalo sikulijua kabisa ni hili la wananchi kupuuza na kudharau kile kinachofanywa na upinzani hasa yaani kususia vikao vya bunge, kubeza hatua zinazochukuliwa na mhe. Rais Magufuli n.k.
 
Mtaa gani wanaisifu serikali ya JPM, sijui mtaa gani watasifu sukari kuuzwa 3000@kg, mtaa gani ambako hela haipatikani kitaani halafu bei za bidhaa muhimu ziko juu.

Mwezi huu kwa waislam wanakuwa na mahitaji mengi sana ya sukari lkn ndio hivyo.

Hata kama umeupata uDC au umeukosa, kuweni wakweli huko kujikomba kwenu ni maumivu kwa wananchi
 
Huyo mtoa mada kaandika ili asikie watu wana maoni gani. Kiukweli asilimia kubwa wanalalamika sana tena sana...chai siku hizi inanyweka kwa Mwenyekiti na KATIBU wa chama
 
Haya matatizo ya ukosefu wa
sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa
fedha unaonza tarehe moja Julai
ambapo kila wizara itapewa fungu
lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri
sana ana uhakika pesa
ameshakusanya ya kutosha na ndiyo
maana hata hawa Wazungu
wakimletea za kuleta anawapotezea.

Nimecheka sana kweli villaza mpo.
 
Mtaa gani itaje hapa,,labda mitaa ya ikulu huku kwetu watu wamenuna vibayaa mnooo
Soma vizuri, mwandishi kataja, mbona mvivu wa kusoma. Kama alikuwa kwenye gari la kutoka mbagala ni wazi hao walikuwa wakazi wa huko. Hata huku kwentu Gongolamboto ndivyo wanavyosema.
 
Haya matatizo ya ukosefu wa
sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa
fedha unaonza tarehe moja Julai
ambapo kila wizara itapewa fungu
lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri
sana ana uhakika pesa
ameshakusanya ya kutosha na ndiyo
maana hata hawa Wazungu
wakimletea za kuleta anawapotezea.

Nimecheka sana kweli villaza mpo.
Kilichokuchekesha nini? Binafsi naona hao wananchi wana hoja maana fedha za uzalishaji viwandani hivi sasa bado zinatumika za awamu ya nne.
 
Haya matatizo ya ukosefu wa
sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa
fedha unaonza tarehe moja Julai
ambapo kila wizara itapewa fungu
lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri
sana ana uhakika pesa
ameshakusanya ya kutosha na ndiyo
maana hata hawa Wazungu
wakimletea za kuleta anawapotezea.

Nimecheka sana kweli villaza mpo.
Kilichokuchekesha nini? Binafsi naona hao wananchi wana hoja maana fedha za uzalishaji viwandani hivi sasa bado zinatumika za awamu ya nne.
 
Mtaa gani wanaisifu serikali ya JPM, sijui mtaa gani watasifu sukari kuuzwa 3000@kg, mtaa gani ambako hela haipatikani kitaani halafu bei za bidhaa muhimu ziko juu.

Mwezi huu kwa waislam wanakuwa na mahitaji mengi sana ya sukari lkn ndio hivyo.

Hata kama umeupata uDC au umeukosa, kuweni wakweli huko kujikomba kwenu ni maumivu kwa wananchi
Ndiyo maana hao wananchi wanasema tatizo la sukari litaisha mwaka moya Wa fedha ukianza, wanajua kwa sasa lipo au haujasoma mada yote?
 
Back
Top Bottom