G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Tofauti kabisa na wakuu wengine wa mikoa, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Paul Makonda anatumia gari maalum ya serikali ambayo ni Lexus brand new tena ya mwaka 2016 na siyo V8-Toyota Land Cruiser kama wakuu wengine wa mikoa wanavyotumia.
Siwezi kusema kuwa hii gari ni yake binafsi maana ina usajili wa serikali chini ya lebel ya "RC DAR"
Sasa kama ni yake binafsi basi huu utakuwa udhaifu mwingine kuruhusu gari binafsi kutumia identity ya serikali. Tuliwahi kusikia kuwa alikarabati ofisi ya umma kwa fedha binafsi.
Ila tuishie kuamini kuwa hii ni gari ya serikali kwakuwa ina Identity ya kiserikali na maana kuu. Sasa ni lini serikali ikawa na ubaguzi dhidi ya watendaji wake? RC wengine watembelee V8-Toyota Land Cruiser ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa sasa bila kubadilishwa na huyu atembelee gari jipya kabisa la bei ya ghali sana kuliko V8-Toyota Land Cruiser? Au ndo yale yale ya kusema kuwa "first Magufuli second Makonda?" Eti wa kusemea juu ya Makonda ni Magufuli pekee na hata Simbachawene hana mamlaka hayo (? )
Haya ndiyo yanayotufanya tuamini kuwa ni usanii ule ule wa kuongea haya na kutenda yale. Na kwa kweli ikithibitika kuwa ni gari yake binafsi iliyosajiliwa kwa identity ya kiserikali itakuwa ni kashfa nyingine dhidi ya serikali.
Hongera Makonda kwa kupewa kiti cha enzi cha Tanzania na (baba yako).