Serikali ya Rais Magufuli imekuathiri kwa kiasi gani?

HUNIJUI SIKUJUI

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
1,335
1,546
Habari zenu wakuu,

Hii serikali haitanii, simpigii mtu debe ila kwa kweli nime i-feel kweli, tofauti na serikali iliyopita hii imeleta athari za moja kwa moja katika maisha yangu na nimehisi uwepo wake,field husika sitoitaja hapa.

Vipi wewe mwenzangu?
 
Mimi nakufa njaa . wamemzuia muuzaji wangu Wa jumla Wa DVD kwa hiyo hapa sina Mali mpya kabisa kisa bongo movie wskati siuzi hata kazi zao hata moja. Wazee Wa kukurupuza aka mizuka.
 
Mimi ninakula mala mbili kutwa sina uwezo wa kula mala tatu. Nakunywa chai ya mzaiwa kikombe kimoja, chapatti moja na mayai ya kuchemsha mawili. Jioni nakula wali wa shs 1500 nalala, kabla ya hapo mchana nilikuwa nakula ugali samaki kama shs. 3000 hivi hiyo sasa nimefuta.
 
Mie kwangu poa saaana,ila Jirani yangu ndio anaumwa Ugonjwa wa moyo kwa kasi ya MAGUFULI.

Biashara zangu zinaenda kama kawaida,na faida kubwa zaidi nikwamba kumekuwa na wepesi saaaana kwenye ofisi za Umma kihuduma,na heshima imerudi baina ya wafanyakazi wa serikali na sie wahitaji wa huduma.

Kubwa zaidi,watu watakula mapato yao ya halali,
 
habari zenu wakuu
hii serikali haitanii,simpigii mtu debe ila kwa kweli nime i-feel kweli,tofauti na serikali iliyopita hii imeleta athari za moja kwa moja katika maisha yangu na nimehisi uwepo wake,field husika sitoitaja hapa

vipi wewe mwenzangu?
Kwanini usinge uliza kwamba serikali hii imeleta faida za moja kwa moja kwa akina nani?

Samahani mkuu...
Najaribu kufikiria tofauti
 
Sio wote wataiona neema, kama mliuza DVD bila utaratibu mlitegemea mfaidike, nyinyi ndo majipu mnatumbuliwa ili na wengine wapate neema!
Utaratibu upi unaousema!? Kuwasaidia bongo movie ndio utaratibu kisa walikuwa jukwaani wakati Wa kampeni!? Si walikuwa wanalipwa lakini au walipanda bure!?
 
Serikali inapobana matumizi, uzalishaji unapungua katika soko la bidhaa, pia hupelekea uwekezaji kupungua na kuleta athari katika soko la fedha.
 
Mie kwangu poa kwani muadilifu nampenda John Magufuri kwani napenda kazi
 
Kama umeathirika ama wewe au wa karibu yako alikuwa ana kipato kisicho halali
Wote walioathirika ni baada ya mirija ya wizi nk kufungwa

Mkuu athari (effect) yaweza kuwa in +ve or -ve way. Naona kama umechukulia -ve effect tu. Kwani hiyo mirija kufungwa kunaweza kuleta +ve effect kwa baadhi ya watu and vice versa.
 
Mie kwangu poa saaana,ila Jirani yangu ndio anaumwa Ugonjwa wa moyo kwa kasi ya MAGUFULI.

Biashara zangu zinaenda kama kawaida,na faida kubwa zaidi nikwamba kumekuwa na wepesi saaaana kwenye ofisi za Umma kihuduma,na heshima imerudi baina ya wafanyakazi wa serikali na sie wahitaji wa huduma.

Kubwa zaidi,watu watakula mapato yao ya halali,
Hapa Umenena Mkuu, Kweli Wew Sio Jipu Tupeane Dili Basi Hata La Kufagia Ofisini Kwako Mkuu
 
Ktk Kuweka Mambo Sawa Kuna Athari Hasi Na Chanya Huwa Zinajitokeza.
Kwa Waliokuwa Wanafanya Biashara Halali Wanakula Shavu Kubwa Maana No Figisu Kuanzia Ngazi Ya Chini Hadi Ya Juu.
 
Back
Top Bottom