georgemwaipungu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 2,779
- 589
SERIKALI YA MAGUFULI NAYO NI JIPU JINGINE.
inahitaji kutumbuliwa.
UCHAGUZI MEYA ILALA,KINONDONI NA JIJI LA DAR ES SALAAM.
Mara ya kwanza waliletwa Wabunge viti maalumu toka Zanzibar eti nao wapige kura Kinondoni ili tu CCM ishinde wa guvu.Upinzani wakagoma.
Upinzani wakafungua kesi mahakama kuu kutaka mahakama itoe mwongozo wa tafisri ya sheria kuhusu uhalali wa wabunge wa zanzibar kuletwa Bara kupiga kura kwenye halimashauri wakati serikali za mitaa na tawala za miji na mikoa si mambo ya Muungano kiasi cha kuleta watu wa Zanzibar ama baadae kupeleka wabunge wa bara Zanzibar.
kabla Mahakama kuu haijatoa mwongozo Uchaguzi ukaitishwa tena kufanyika leo Jumamosi.
Upinzani wakaamua kupeleka zuio mahakamani kuwa uchaguzi wa meya ilala na kinondoni usifanyike leo mpaka kesi ya kuhusu tafisri ya kisheria kuhusu uhalali wa wabunge wa zanzibar kupiga kura kinondoni utolewe na ilitegemewa kesi kufanyika 29/01/2016,ili wale tu wanaoruhusiwa kupiga kura ndio washiriki na si vinginevyo.
Mahakama kuu jana ilitupilia mbali pingamizi la wapinzani na kusema uchaguzi unaweza kuendelea hata kama mwongozo kuhusu wabunge wa Zanzibar haujatolewa.
Wapinzani wakaona isiwe tabu, si na wao wana wabunge viti maalumu toka Zanzibar.
Leo wapinzani nao wakaleta wabunge wa viti maalumu toka Zanzibar wakiwemo wa CUF na CHADEMA. Na CCM kama kawaida walileta wale wa mwanzo japo hawakujua kama na wapinzani wamekopi na kupaste staili ile.
Kwa kitendo hiki ilikuwa ama wabunge wote toka Zanzibar waruhusiwe kupiga kura ama wote wasipige kura.
Kama wangepiga kura wote, CCM ingeshindwa.
Kama wasingepiga kura hao wa Zanzibar kitu ambacho ndio sahihi, bado CCM wangeshindwa uchaguzi.
Wakaona hii ishakuwa noma na mipango yao imebuma.
Ghafla zikatolewa taarifa kuwa uchaguzi hautafanyika kwa sababu kuna ZUIO LA MAHAKAMA.
DUUUUUUUUH.nashangaa kwa kweli.
watu wakahoji limetoka wapi na limetolewa lini na liliwekwa na nani?
Majibu yakawa ni kwamba zuio limetolewa na Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jana Ijumaa na aliyeweka hilo pingamizi ni kada wa CCM. Hiyo ilifanyika kimyakimya(mpango wa siri huu maana haiwezekani wasiseme).
hali kama hii imetokea Ilala.
Lakini maajabu ni kwamba jana Ijumaa MAHAKAMA KUU imetoa ruling yaani mwongozo kuwa uchaguzi uendelee lakini jana hiyohiyo MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU nayo ikatoa pingamizi uchaguzi usiendelee.
sasa uamuzi upi ufatwe?kati ya ule wa Mahakama kuu na ule wa Mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Kisheria Mahakama kuu ina nguvu kuliko Mahakama ya hakimu mkazi.Na maamuzi ya Mahakama kuu pia yana nguvu kushinda maamuzi ya mahakama ya hakimu mkazi. Hivyo maamuzi ya kwamba uchaguzi uendelee yalipaswa kufuatwa.
Chaajabu ni Kwamba Mkurugenzi kafata maamuzi ya Mahakama ya hakimu mkazi iliyo ndogo kimamlaka kuliko Mahakama kuu iliyo na mamlaka makubwa na maamuzi yake HAYAPASWI KUPINGWA NA MAHAKAMA YA CHINI YAKE.
kwa hali ya kawaida Zuio la mahakama ya kisutu halikuwa na nguvu kisheria mbele ya maamuzi ya Mahakama kuu.
Kwa nini haya yanatokea?Jibu ni kwamba serikali ya Magufuli ni JIPU linalotakiwa kutumbuliwa.
Huu ni zaidi ya uhuni kufanywa na Serikali ya Magufuli.Nasema serikali kwa kuwa wote wamekaa kimya toka uhuni wa kwanza na kuruhusu yote haya tena mbele ya mawakala wa serikali akiwemo mkurugenzi.
Kama ccm wangeona leo wapo wengi basi uchaguzi ungefanyika washinde kwa kutumia wabunge wa Zanzibar.Kwa kuwa hawako tayari kuachia manispaa hizi leo tena wakaahirisha uchaguzi baada ya kugundua hawashindi kwa kuleta wabunge wa zanzibar.
Magufuli wakati analihutubia bunge alisema kuna majipu.
wakati anaomba kura alisema atakuwa Rais wa wote.Maana yake atasimamia misingi ya haki.KIKO WAPI? hata bomoa bomoa haizingatii misingi ya haki.
Kitendo cha mizengwe yote katika uchaguzi wa manispaa ya kinondoni na Ilala imedhihirisha pasi na shaka kuwa CCM na serikali ya Magufuli ni JIPU.
serikali ya Magufuli imeendelea kuruhusu uporwaji wa wazi wa Demokrasia pale ambapo inajulikana CCM haistahili kutoa meya ilala wala kinondoni wala meya wa jiji kwa uwiano wa madiwani.
Ni ujinga unaovuka mipaka kwa watu wazima kwenda kuchukua Wabunge toka Zanzibar eti waje kinondoni kupiga kura.
Haya yote yanafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi hii na yanafanyika chini ta serikali ya Magufuli.
Yako wapi maelekezo ya papo kwa papo kuhusu ukiukwaji huu wa sheria?
Kwa muda wote haya yote yameachwa yafanyike bila mishipa ya aibu.
Huwezi kuwa kiongozi wa kusimamia maovu badala ya kuyakemea ama huwezi kuwa kiongozi ukawa kimya wakati kuna maovu yanatendeka.
Kitendo kinachofanywa na CCM na Serikali ya Magufuli ni KUTENGENEZA AKINA NKURUNZINZA NA NTARAHAMWE NCHINI kitu ambacho ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa.
Inaniwia vigumu kuamini kuwa hawa ndiyo waliweza kumpa haki Lowasa kwenye kura za Urais.
Hivi hata aibu hamuoni?Kuanzia Ikulu kwa Rais mpaka kwa waziri na huyo mkurugenzi?