mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Watanzania wenzangu, salaam!
Mimi kwa upande mmoja naipongeza serikali inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kufuatia uwezo na weledi ktk vita dhidi ya ufisadi nchini.
Hata hivyo kuna issue ambazo kama zikiachwa zilivyo zinatia shaka uhai wa CCM, hatutaki tuendelee kushinda uchaguzi kwa kusaidiwa na vyombo vya usalama wala polisi. Hebu sasa tukiwa wanaccm tulioiva tushauri serikali ibadiri mienendo hii:-
1. Sakata la dawa za kulevya polisi ndio wahusike kupeleleza, kubaini na kukamata wahusika badala ya kutajataja majina kienyeji as if hakuna professional police waliobobea ktk upelelezi.
2. Katika mabadiriko ya baraza la mawaziri ajaribu kutoa kipaumbele kwa Wabunge waliochaguliwa majimboni ambao wana uwezo wa kusimamia wizara. Kuteua uwaziri toka kundi la Wabunge walioteuliwa kunatia ukakasi na kuwafanya walioachwa waone kama wametengwa, (tukumbuke walioteuliwa nafasi za juu ni Tulia Acksoni (spika), Ndalichako (waziri elimu), Mbalawa (waziri uchukuzi), Mpango (waziri fedha), Posi (naibu waziri), Mahiga (waziri mambo ya nje) nk nk hii list hapendezi kabisa kwa kuwa Bungeni tuna mtaji mkubwa wa Wabunge toka majimboni.
3. Katika baadhi ya mikoa imethibitika taarifa ya hali ya chakula, njaa na mikakati ya uzalishaji mazao iliwasilishwa. Hivyo, tusivutane ktk hili kwa kuwa baadhi ya maeneo tayari yana upungufu mkubwa wa chakula. Serikali ithibitishe kuwa pamoja na upungufu huo hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa,
4. Mivurugano na mivutano ya kimaslahi - katika vita dhidi ya kukuza uchumi pamoja na kuwa kipaumbele chako ni Tanzania ya viwanda lakini tufahamu kuwa hivi tumefika idadi ya watu takribani 50milioni. Ambapo kati ya idadi hii 70% ni wakulima, hivyo kipaumbele cha kwa kinapaswa kuwa Tanzania ya Kilimo cha kisasa. Viwanda inapaswa kuwa kipaumbele cha pili.
5. Tathmini juu ya mikopo ya wanavyuo wa elimu ya juu - maskini ni wengi
6. Tathmini ya ajira - hapa vijana wengi wako mitaani na fursa za nje ya mfumo wa umma haziwezi kuwafikia wote hivyo upanuzi wa wigo wa sekta binafsi ni muhimu.
7. Watumishi wa umma ni kaa la moto.
Nwasalisha.
Msakila KABENDE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI