Serikali ya kikwete yagoma kulipa pesa za wakulima wa mahindi

Judy Nash

Member
May 10, 2013
41
11
Wanajamvi..

Katika hali ya kusikitisha na kukatisha tamaa, serikali ya Kikwete imeshindwa kulipa pesa za wakulima kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa NFRA. Katika kanda ya Songea takribani vijiji ishirini ambavyo vilikuwa vituo vya NFRA wakulima wake wamekuwa wahanga wa tatizo hili la kuikopesha serikali kwa lazima.Vijiji hivyo ni Madaba, Matiri,Kigonsera,Mgazini,Lugagala,Mpitimbi,,Magagula,Lusonga,Namabengo,Mkongo,Mbinga, Litisha, .....nk

Licha ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa ni jambo la aibu kwa serikali yake kudaiwa na wakulima na kuwaahidi wananchi kuwa pesa hiyo italipwa muda si mrefu,bado imekuwa ni danganya toto kwakuwa tangu aitoe kauli hiyo akiwa Mkoani Njombe mpaka sasa takribani mwezi umepita na hakuna pesa wakulima wamelipwa.
Wananchi hao wanaidai serikali pesa ya mahindi waliyoyauza kwa NFRA tangu septemba na oktoba mwaka huu.Pesa ambayo kimsingi ilitakiwa inunue pembejeo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo za msimu huu wa 2013/2014.
Mvua zimeanza kunyesha lakini wakulima hawana fedha mikononi hiivyo wanapata kigugumizi katika kufanya shughuli zao za kilimo.

Je hii ni haki kweli,katika serikali ambayo inatangaza kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongoo, ikisisitiza kuwa KILIMO KWANZA ndiyo kauli mbiu yao,leo hii wanamdidimiza mkulima na kumfanya ashindwe kuendeleza kilimo ilhali wao wanajilipa mishahara na kuishi maisha mazuri.
Jenista Mhagama,Dr Emmanuel Nchimbi, Vita Kawawa, Kayombo nyie ndio wabunge wetu mbona hatuwaoni mkihangaikia jambo hili ni kweli hamlijui..? Sasa mpo bize na shughuli zipi kama hizi kero za wakulima mnashindwa kuzitatua, mpo kwa ajili ya nani.?..
 
Back
Top Bottom