Serikali ya Kikwete lazima ifunge mkanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Kikwete lazima ifunge mkanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kasitile, May 11, 2011.

 1. kasitile

  kasitile Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa Mdororo wa Uchumi ulioikumba Marekani na nchi za Magharibi kati ya mwaka 1929-1933,kuna shujaa aliibuka.Franklin Delano Roosevelt ambaye wakati huo alikuwa anagombea urais wa Marekani alikuja na mikakati kabambe ya kuinua uchumi,mikakati hiyo inajulikana kama "NEW DEAL",mipango hiyo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Roosevelt ndiye rais wa Marekani aliyekaa muda mrefu madarakani (1933-1945),na ambaye anakumbukwa sana na Wamarekani.

  Nchi yetu nayo imepitia vipindi vigumu sana.Wakati wa vita vya Kagera Mwalimu Nyerere aliwaambia wananchi wafunge mkanda kutokana na kuwepo na maisha magumu kwa wananchi.Tumeendelea na kufunga mikanda hadi sasa.Wakati wa Mwalimu Nyerere,angalau uongozi ulikuwa unaonyesha juhudi,na hata maisha waliyokuwa wanaishi viongozi,angalau walionyesha nao wanafunga mikanda.

  Kwa sasa kuna malumbano kati ya Waziri wa Fedha bwana Mkullo na Bwana Zitto.Malumbano hayo yanatokana na kauli ya Zitto Kabwe kuwa serikali haina fedha,kiasi kwamba imefika sehemu inakopa mishahara.Mkullo amejibu hoja ya Zitto kwa usanii zaidi na dharau bila kutoa hoja za kushawishi.Naomba ni-declare interest;mimi ni mtumishi wa umma katika Local Govenment.

  Hakuna ubishi kwamba serikali haina fedha kwa sasa.Miradi mingi ya Maendeleo inayoendeshwa kwa ruzuku toka serikali kuu imekwama kwa sababu fedha hamna.Ruzuku ya kuendesha ofisi imeshuka kwa kiasi cha kutisha na kufanya maisha ya wachakachuaji serikalini kuwa magumu sana.Mfano,Halmashauri inayotakiwa kupata ruzuku ya kuendesha ofisi kiasi cha Tshs 50,000,000/= (General Fund),kwa sasa inapata kiasi cha Tshs 10,000,000/=.Kwa hiyo zile local government ambazo zinategemea kwa kiasi kikubwa ruzuku toka serikali kuu,zinashindwa kujiendesha kwa sasa.Anayebisha aje na vielelezo,nami nitavimwaga hapa hata kama maadili hayaruhusu.Lakini hatuwezi kunyamaza huku mambo yakienda mrama.

  Licha ya kwamba hali ya uchumi kwa wananchi na serikali kuwa mbaya sana,viongozi wetu wakuu wanaongoza kwa kuishi maisha ya anasa.Mfano ni semina elekezi inayoendelea huko Dodoma,ni ufujaji wa fedha za umma kwa kiasi cha kutisha.Posho za safari,semina,ununuzi wa mafuta ya magari,ununuzi wa magari ya kifahari ambayo sio ya lazima ni mambo yanayotakiwa kutazamwa upya.Misharara ya mawaziri na wabunge hayana mahusiana na maisha ya watu wanaowaongoza.

  Akiba ya taifa lazima iongezwe sana,kwanza kwa kupunguza sana na kwa busara matumizi ya serikali.Serikali ikusanye kodi kutoka kwa makampuni makubwa badala ya kuwabana wananchi wa kawaida.Vitu vya anasa vinavyoingizwa nchini bila kutozwa ushuru wa forodha lazima vipigwe marafuku.Kila kitu lazima kitazamwe kwa hali yake halisi na kuachilia mbali suala la kutaka sifa za kijinga kama rais wetu anavyopenda.Tukichukua jumla ya gharama za Rais,mawziri na wabunge,ni gharama kubwa za kutisha sana,laiti wananchi wangelijua hili,hatari ya vita inaweza isiepukike.

  Mwisho japo si kwa umuhimu,niseme,serikali lazima itambue dhamana kwa wananchi.Katika hali kama hii viongozi wetu lazima watangulie kufunga mkanda kabla ya wananchi.Lakini kwa ujeuri wa viongozi wetu wa Afrika bila kelele za wananchi hawawezi kubadilika.Mabadiliko huletwa na wananchi "Rice can only be cooked inside the pot".Asanteni,naomba kuwasilisha.
   
 2. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Afadhali wewe umeona hata wanazopata kwa sasa, hawa hawatafunga mikanda maana wameishasema huu ni wakati wao sisi tulie tu, cha maana tushaulinane mikanda jinsi ya kuwafunga hiyo mikanda. Wao wamelegeza mikanda maana matumbo bado hayajajaa na wana njaa kama mfalme wa Majuju, aliyemeza magogo na matakataka mengine na kila dakika alilia Njaaaaaa!!!!. Tusipowaziba midomo waache kula tumekwisha, kwani zile tunazoshangaa kuwa ni hela nyingi kwao nivijisenti tu kwa sasa:biggrin1::biggrin1::pound::pound::pound::pound:, tukinyamaza tumekwisha na tutajijutia wenyewe na wajukuu zetu weraaaaaaaa!!! kufa hatufi ila cha motooooooooo!!! tutakiona:A S 103::A S 103:
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nchi changa!
   
Loading...