Serikali ya Dk.Shein yanadi jeuri

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,488
Likes
27,324
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,488 27,324 280
SERIKALI iliyoundwa na Dk. Ali Mohamed Shein baada ya kufutwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa 25 Oktoba 2015 imesema, pendekezo la kuwepo serikali ya mpito ni ‘upuuzi mtupu’, anaandika Mwandishi Wetu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Balozi seif Ali iddi katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) uliojadili na kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Balozi Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema, hakutakuwa na serikali ya mpito wala ya mseto pia hakutakuwa na uchaguzi mwingine kabla ya mwaka 2020.

Kauli ya Balozi Seif inatokana na malalamiko ya Chama cha Wananchi (CUF) kutaka kurudiwa kwa uchaguzi huo kwa maeleza kuwa, Dk.Shein amerejea madarakani kwa njia haramu.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa mgombea urais wa CUF visiwani anaelezwa kushinda.

Kabla ya kumalizwa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kwenye majimbo yote Zanzibar, Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) alifuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai ya kuwepo kwa kasoro mbalimbali.

Hatua hiyo ililalamikiwa na kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, wasomi, makundi ya kutetea haki pamoja na mataifa ya nje.

Pamoja na malalamiko hayo, ZEC chini ya Jecha ilitangaza marudio ya uchaguzi kuwa tarehe 20 Machi mwaka huu kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Hatua hiyo ilisababisha CUF na vyama vingine vha upinzani kugomea marudio ya uchaguzi hu.

Hali hiyo iliiweka Zanzibar katika sintofahamu na hata kusababisha majeshi ya nchi kuelekezwa visiwani humo huku baadhi ya raia wakitajwa kukimbia kisiwa hicho kuhofia kutokea machafuko kama ilivyokuwa mwishoni mwaka 2000
 
Last emperor

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Messages
5,052
Likes
1,865
Points
280
Last emperor

Last emperor

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2015
5,052 1,865 280
Watavuna wanachopanda...mwisho wa ubaya aibu...
 
Mdudu halisi

Mdudu halisi

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2014
Messages
2,608
Likes
4,153
Points
280
Mdudu halisi

Mdudu halisi

JF-Expert Member
Joined May 7, 2014
2,608 4,153 280
Maisha ya wananchi wa Zanzibar hivi sasa hayana utofauti na yale wanayoishi wananchi wa Somalia.
 
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,064
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,064 280
Cuf wametishia ku***ba kumbe wanaharisha wasubiri tu 2020
 
Lupyeee

Lupyeee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Messages
2,689
Likes
2,794
Points
280
Age
48
Lupyeee

Lupyeee

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2016
2,689 2,794 280
Cuf ni mdudu gani mpaka abembelezwe kiasi hiki .

Mwamuzi akiamua mechi irudiwe alafuTimu Fulani isitokee uwanjani kuna kubembelezana tena hapo??

Hizi ni zama za hapa kazi tu
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
18,242
Likes
29,929
Points
280
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
18,242 29,929 280
Uchaguzi wa October 25,2015 ni sawa na Mtu aliekufa anaetaka kuushuhudia tena asuburi Yaumul Qiyaama-Mh.Aboud
 
B

Bekabundime

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Messages
1,698
Likes
1,234
Points
280
B

Bekabundime

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2014
1,698 1,234 280
sifa za kijinga
Cuf ni mdudu gani mpaka abembelezwe kiasi hiki .

Mwamuzi akiamua mechi irudiwe alafuTimu Fulani isitokee uwanjani kuna kubembelezana tena hapo??

Hizi ni zama za hapa kazi tu
 
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,568
Likes
2,221
Points
280
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,568 2,221 280
Jecha kiboko yao. Wataisoma namba.
 
Mwana

Mwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Messages
5,060
Likes
1,404
Points
280
Mwana

Mwana

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2010
5,060 1,404 280
SERIKALI iliyoundwa na Dk. Ali Mohamed Shein baada ya kufutwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa 25 Oktoba 2015 imesema, pendekezo la kuwepo serikali ya mpito ni ‘upuuzi mtupu’, anaandika Mwandishi Wetu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Balozi seif Ali iddi katika hotuba yake ya kufunga mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) uliojadili na kupitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Balozi Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema, hakutakuwa na serikali ya mpito wala ya mseto pia hakutakuwa na uchaguzi mwingine kabla ya mwaka 2020.

Kauli ya Balozi Seif inatokana na malalamiko ya Chama cha Wananchi (CUF) kutaka kurudiwa kwa uchaguzi huo kwa maeleza kuwa, Dk.Shein amerejea madarakani kwa njia haramu.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa mgombea urais wa CUF visiwani anaelezwa kushinda.

Kabla ya kumalizwa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kwenye majimbo yote Zanzibar, Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) alifuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai ya kuwepo kwa kasoro mbalimbali.

Hatua hiyo ililalamikiwa na kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, wasomi, makundi ya kutetea haki pamoja na mataifa ya nje.

Pamoja na malalamiko hayo, ZEC chini ya Jecha ilitangaza marudio ya uchaguzi kuwa tarehe 20 Machi mwaka huu kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Hatua hiyo ilisababisha CUF na vyama vingine vha upinzani kugomea marudio ya uchaguzi hu.

Hali hiyo iliiweka Zanzibar katika sintofahamu na hata kusababisha majeshi ya nchi kuelekezwa visiwani humo huku baadhi ya raia wakitajwa kukimbia kisiwa hicho kuhofia kutokea machafuko kama ilivyokuwa mwishoni mwaka 2000
Balozi Seif Idd ni Makamu wa Pili wa Rais!
 
Forum statistics

Threads 1,235,705
Members 474,712
Posts 29,231,179