Serikali ya China yakabidhi 'scanner' kwa bandari za Dar es Salaam na Tanga

TPA

Member
Sep 28, 2016
49
71
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia ubalozi wake hapa nchini imekabidhi rasmi mashine mpya ‘scanner’ (gantry & mobile) mpya za ukaguzi wa mizigo zitakazotumiwa na Bandari za Dar es Salaam na Tanga kudhibiti mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti mizigo haramu kama vile pembe za ndovu, mihadarati na bidhaa nyingine haramu.

Tukio la makabidhiano hayo limefanyika ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, Machi 01, 2017 mbele ya wageni na wadau mbalimbali wa Bandari ikiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Mapato Tanzania (TRA).

Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deudedit Kakoko na Wajumbe wengine wa Bodi ya Mamlaka, Dkt. Francis Michael, Dkt. Jabiri Bakari, Bi. Jayne Nyimbo na Bw. Renatus Mkinga.

17038824_630475767158595_8701500543703726469_o.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Lu Youqing wakiweka saini hati za makabidhiano ya Scanner zilizotolewa na Serikali ya China kwa Bandari za Dar es Salaam na Tanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.

17098688_630376900501815_3409802851491369712_n.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing wakibadilishana nyaraka za makabidhiano za scanner mpya za kukagua mizigo bandari ya Dar es Salaam na Tanga hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko.

17021665_630377043835134_471785708105915100_n.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (kulia) akisoma hotuba yake wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya scanner za ukaguzi wa mizigo hivi karibuni.

17103294_630475787158593_6400165885204031855_n.jpg
Prof. Mbarawa akikata utepe kuzindua rasmi matumizi ya scanner za mizigo huku Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka, Wajumbe wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko wakishuhudia.

16996389_630376993835139_1678893478677059319_n.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) akipewa maelezo ya uendeshaji wa scanner mpya na Meneja Mradi Bw. Mtani Rugina.

16938847_630377083835130_8746263828787713864_n.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (wapili kulia) akikabidhi zawadi maalumu ya picha ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing ikiwa ni ishara ya kuishukuru Serikali ya China kwa mchango wake wa kuziendeleza Bandari za Dar es Salaam na Tanga.

17103246_630376943835144_2454780143714327381_n.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TPA.

16939287_630377120501793_5699472872275385046_n.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dowuta Taifa, Bandari ya Dar es Salaam pamoja na Wafanyakazi wa TPA wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya scanner mpya za ukaguzi wa mizigo.
 
Hongera, ila ni vizuri ziangaliwe kwanza kwenye ubora wake ili isije ikawa inashindwa kuditect mizigo ya wadau maana Tanga na Dar ndo madambwe yaliyokuwa yanatumika huko awali!
 
Back
Top Bottom