Serikali ya CHADEMA ni kubwa mno!

Uelewa wa mtoa mada unatia mashaka ....................balaza kivuli liwe kubwa liwe dogo lina gharama gani? kwa nini uwa tese watu wa chache kufuatilia watu wengi wakati hawana gharama? mimi naona ni dogo mno lakini wa kiunda serikali 15 wanatosha kabisa
 
Ugonile malafyale? Twa mbombo? Naona ndugu yangu malafyale una wivu wenzio wakitawala kwa kuwa jina lako lina maanisha mtawala. Kama huelewi maana ya kivuli pole sana, kesho jua likiwaka angalia kivuli cha jua.

Si kweli kuwa serikali kivuli lzm ifuate mfumo wa kila kitu kutoka kwenye serikali halisi!
 
Duh...you're right whether they like it or not, baraza kivuli la mh.mbowe ni kubwa sana, kwa maoni yangu lingetosha kuwa na wabunge 13 na yeye mwenyewe wa kumi na nne. Gharama ziko, ackudanganye mtu. Waziri kivuli anaingia moja kwa moja kwenye kamati husika ya kudumu ya bunge kama mjumbe wa kamati, eg. Mnyika ambaye ni waziri kvli wa Nishati/Madini tayari ni mjumbe wa kamati hyo chini ya m/kit wake J.makamba, anapokea posho ya vikao vya kamati hyo kama wajumbe wengine na kulipiwa nauli endapo kamati itakuwa na ziara ndani na nje ya nchi, hivyo gharama zinaongezeka kwa ukubwa wa baraza kvli!
 
Afrika Mashariki is just like a department in the foreign affairs and international cooperation!

Then,ili kupunguza wizara ningeshauri Wizara ya Maliasili iunganishwe na Wizara ya Mazingira;Wizara ya Ofisi ya Rais-Utawala Bora iunganishwe na Wizara ya Mambo ya Ndani;nyinginezo nyingi tu zinastahili kuunganishwa!

lengo liwe ni kuionyesha CCM kuwa wanakosea mno kwa kuunda serikali kubwa!
 
Kulikuwa na nafasi ya kuunganisha wizara. Kwamfano Mr. Mbowe angeweza kuunganisha "Ujenzi na mawasiliano" Ofisi za Rahis ni nyingi sana, nk nk.
Kimantiki wamechemsha, nakubalina na mtoa hoja.
 
Great thinker no more. How can someone come with this type of thread?, What is shadow stands for?. Anyway I need a break from reading these types of thread.
 
hicho ni kivuli cha kikwete kama huelewi.wapeni chadema madaraka muone kazi kwa vitendo.


Kivuli siku zote huwa na Features nyingi lakini si Zote.
Kwa mfano kama umevaa nguo ya Bluu kivuli bado kitakuwa cheusi.
Ni serikali kivuli if you know ze meaning.
 
Kwanza we malafyale kuna kitu hukijui au umetumwa nini na rais kikwete baraza la mawaziri kivuli hulielewi nini? Muulize vizuri msando albert.
 


uwezo wako wa kufikiri unatakiwa kuongezewa mwamko.UMEAMBIWA SERIKALI KIVULI.NI LAZIMA IENDANE SWAMBAMBA NA WIZARA ZILIZOPO.
DR SLAA ALISEMA VILE KWAKUWA YEYE NDIYE ANGEPANGA WIZARA.
 
Mkuu hebu kua kama mtu aliyefuta ujinga kidogo.Baraza dogo sana litashindwa pia kufuatilia serikali ipasavyo.Mfano,angeweza kusema Waziri mmoja Kivuli asimamie wizarz tatu za JK,lakini hii ni realistic?Mtu mmoja atawezaje kupambana na serikali au wizara tatu zilizojaa uvivu?Kinachotakiwa ni kufanya ufuatiliaji wa man to man,kila wizara iwe na waziri kivuli mmoja.Jk yeye ameweka mawaziri 2 na wengine 3.Kama mpaka sasa hujaelewa,basi itabidi urudi tena shule au uwasitaki waliokupa vyeti kwa maana walionesha umefauku kumbe sivyo
 
Kwa kawaidi kivuli kinakuwa sawa kabisa na kitu chenyewe ili tu scale inaweza kuwa tofauti. Mafano kivuli cha mti kinaweza kuwa kidogo kwa sababu ya scale tu, lakini ukweli ni kwamba ukichunguza kila undani wa mti upo kwenye kivuli. Sasa unawezaje kupunguza baraza la mawaziri kivuli wakati real object ni kubwa. Mfano kuweka wizara ya mambo ya nje chini ya waziri kivuli moja ni upeo wa hali ya juu sana. Ila wewe kwa sababu ya kuganda kwa akili zenu na sera zenu za kuskwanda unataka kulazimisha kivuli kiwe kidogo ili mwone inawezekana kuunda serikali ndogo. Nakwambia ninyi ni vilaza na mtaendelea kuwa vilaza mpaka siku mtakapotoweshwa katika nchi hii.
 
Lakini tukiangalia maana ya kivuri ni reflection ya kitu fulani.Kilichoundwa na Mbowe ni reflection ya baraza la mawaziri la serikali.Hata kama sheria inakuruhusu je utacombine wizara 3 iwe wizara moja,je mnampa majukumu mangapi huyu waziri kivuri.Kwa upande wangu bado naona ni baraza dogo ukilinganisha na la serikali.Ila kama CDM wangekuwa wamekamata dola ni juu yao hata kuunda wizara 10 zinazokidhi mahitaji ya taifa
 
Huyu mtoa hoja c mzima na cku zote wa2 wa aina hii wanatoa hoja za kipumbavu dhidi ya wapinzani mbona hutoi hoja za msingi{umeme,reli,air TZ,bandari,elimu,dawa,ufisadi}ikisha sema CCM wakweli au waongo walipokuwa wanatoa ahadi mbele ya walalahoi
 

ndugu malafyale umepotoka kidogo
naamini nia yako ni njema kabisa lakini kuna mambo 2 umeshindwa kuyaelewa either kwa makusudi au kwa bahati mbaya,sheria haisemi kiongozi wa kambi ya upinzani anaweza kupunguza wizara kama anavyotaka,serikali ina wizara na mawaziri 27,manaibu waziri 23,jumla 50,sheria inasema lazima hizi wizara zote ziwe na waziri kivuli,ndivyo alichokifanya mbowe kuna mawaziri kivuli 27 hata hiyo ya africa mashariki unayoisema ipo na waziri kivuli wake ni mustapha akuunay(mp mbulu chadema)
manaibu WAZIRI wako wa 2 fedha NA tamisemi,jumla 29,utaona kwamba baraza hilo linamawaziri 26 ambao ni lazima wawepo na manaibu waWILI na alitoa ufafanuzi wa uzito wa wizara alizoona zinahitaji manaibu kama nilivyoorozesha hapo juu.
pia bila kusahau kUtoka 50 hadi 29 ni Punguzo la asilimia 42%,naomba ninukuu msemo wa kingereza unaosema no research no right to speak,hivyo sitaki kuamini ulikuwa na nia ya kupotosha,naamini ulikuwa na nia ya kukosoa ili kujenga,unless u say so.kumbuka chadema walisema wao kama wangepewa ridhaa ya kuongoza na kuunda serikali wasingekuwa na wizara zinazozidi 20,serikali ya ccm sasa ina wizara 27,pia walisema baraza lao la mawaziri yani mawaziri na manaibu hawatazidi 24.PAMOJA NA SERIKALI KUWA NA MANAIBU WAZIRI WAPATAO 23,WAO WANAMANAIBU WAZIRI 2 TU.KWA MSISITIZO BOFYA HAPO USIKILIZE NA KUJIONEA MH.MBOWE YouTube - Mh. Freeman Mbowe akitangaza baraza lake la mawaziri vivuli leo (Michuzi Blog)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…