Serikali ya CCM yafufua DECI

kennedy lufulondama

New Member
Dec 8, 2012
2
2
SERIKALI YA CCM YAFUFUA DECI


Katika hali isiyotegemewa na watanzania walio wengi, serikali ya Chama cha Mapinduzi ambayo mara zote huwa ndiyo ya kwanza kutokea na tukio la kwanza lisilovutia hisia za wengi, imefufua ule mchezo wa kuchangia kupitia kupanda na kuotesha mbegu uliokuwa unaendeshwa na Taasisi ya Deci.

Kufufuliwa kwa mchezo huu kunadhihirishwa na kitendo cha serikali kuondoa zuio la mafao ya kujitoa baada ya kupigiwa kelele na wadau wa hifadhi ya jamii ikidaiwa kuwa uamuzi wa serikali kuzuia mafao ya wanaoacha kazi kabla ya umri wa kustaafu ulikuwa na madhara makubwa kiuchumi na kijamii kuliko faida.


Mchezo huo ulioibuka miaka mine iliyopita ulipigwa marufuku na serikali kutokana na namna ulivyokuwa unaendeshwa na madhara yake katika uchumi wa Taifa mchezo huo ulihusisha upandaji mbegu (uchangiaji) na kusubiri mbegu kuota (kuiva kwa amana) ambapo ilikuwa ni miezi miwili tu mpanda mbegu kuweza kuvuna mafao ambayo ni shilingi kwa shilingi au asilimia mia ya kiasi cha mchango.
Hata hivyo, mchezo huo ulifutwa na serikali kutokana na namna ulivyokuwa unaendeshwa hasa namna ya ugharimikiaji wa mbegu zilizoota (amana zilizoiva) ambapo michango ya wanachama wapya ndiyo kilikuwa chanzo pekee cha kugharimikia mafao ya mbegu zilizoota, badala ya mafao yatokanayo na uwekezaji.

Kimantiki, mchezo huo wa kulipa mafao ya mbegu zilizoota kwa kutumia michango ya wanachama wapya wanaopanda mbegu ili udumu na uwe endelevu, unahitaji kuwepo na wachangiaji wengi wanaopanda mbegu na wachangiwaji wachache ambao mbegu zimeota ili kutengeneza pembetatu iliyosimama yenye sura ya piramidi. Na ili mchezo huo udumu kwa muda mrefu na kuwa endelevu, inatakiwa pembetatu lililosimama lenye sura ya piramidi lisipinduke na kuwa pembetatu lililolala, yaani idadi ya wachangiwaji (mbegu zilizoota) kuzidi idadi ya wachangiaji (mbegu zinazopandwa). Na hii ndiyo ilikuwa hofu ya serikali iliyolazimu kufutwa kwa mchezo huo.

Sasa narudi kwenye Deci iliyofufuliwa na serikali ya CCM. Na historia ya mchakato wa kufufua Deci ya serikali ya CCM ulikuwa kama ifuatavyo:- Katika mkakati wa kufufua hiyo Deci, Mnamo tarehe 23/2/2012 serikali ilisoma mswaada na mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya jamii 2012 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mnamo, mwezi Aprili, 2012 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitia saini mswaada huo katika kuahalalisha ufufuo wa Deci. Na mnamo tarehe 22/07/2012 serikali ilitoa tangazo katika gazeti la serikali ikipiga marufuku wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii wanaoacha kazi kudai na kulipwa mafao ya kuacha kazi kabla ya umri wa kustaafu.

Bila shaka, tangu serikali itangaze kuanza kutekeleza sheria ya kuzuia mafao ya mwanachama anayeacha kazi kulikuwa na kelele nyingi toka kwa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii wakiwepo wanachama walilalamika kutokushirikishwa katika mchakato wa mabadiliko hayo, hali iliyosababisha serikali kusalimu amri hasa baada ya kugundua kuwa endapo ingeng'ang'ania hoja hiyo, bas pasipo mashaka yoyote serikali ingeondolewa madarakani kwa vuguvugu la wafanyakazi.

Hata hivyo kitendo cha serikali kusalimu amri na kukubali kuondoa zuio la kulipa mafao ya wanachama wanaoacha kazi kabla ya muda wa kustaafu hakujatatua tatizo lililopo katika mfumo wetu wa hifadhi ya jamii ambalo ni ukata wa fedha uliopelekea serikali kujinusuru kwa kutunga sheria inayozuia kudaiwa.

Na hili la serikali kutunga sheria kuzuia mafao mara nyingi hutokea katika kutekeleza mapendekezo ya mthamini wa mifuko ya hifadhi ya jamii hasa baada ya kutokuridhishwa na hali ya kifedha katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kwa sababu tatizo ni ukata wa fedha na vile vile serikali ilikubali kuachana na sheria inayozuia kulipa mafao husika kama njia ya kujinusuru isiangushwe na wafanyakazi na si kwa tatizo la ukata wa fedha katika mfuko kutatuliwa basi pasipo mashaka yoyote, serikali imeanza kugharimikia mafao ya wanachama wanaodai kwa kutumia michango ya wanachama waliopo kazini badala ya kutumia michango ya wanachama walioacha kazi inayotakiwa kutokana na mapato ya uwekezaji na kutoa nafasi kwa michango ya wanachama waliopo kazini kuwekezwa ili kuweza kugharimikia mafao yao katika siku za usoni badala ya fedha za wanachama kugharimikia uendeshaji wa serikali hasa baada ya serikali kushindwa kutumia vizuri fedha za walipa kodi na kutumia michango ya akiba ya wananchi wake kwa ajili ya siku za usoni kuendeshea nchi.


Ni katika hali hii ya serikali kugharimikia ulipaji mafao kwa kutumia michango ya wanachama wapya waliopo kazini badala ya kugharimikia mafao hayo kwa kutumia pato litokanalo na uwekezaji wa michango ya wanachama ndiyo kunakaribisha unaendeshaji wa mfumo wa hifadhi ya jamii unaofanana na uendeshaji wa kuchangiana uliokuwa unaendeshwa na Taasisi ya Deci.

Kwa hali hii ambayo gharama zake ni kuweka hatma ya maisha wastaafu wa baadaye waliopo kazini sasa kuwa mashakani kwani serikali haitaweza kuwalipa mafao wafanyakazi wengi wa migodini ambapo migodi mingi itakuwa imefungwa kutokana na madini kuisha mfano madini ya dhahabu ambayo yana tabia ya kuisha.


Na katika suala hili, pamoja na kusomeshwa na kupata ujuzi kwa kutumia pesa za walipa kodi, wanasiasa na wataalamu wa masuala ya hifadhi ya jamii wanaojua jinsi mfumo wetu wa hifadhi ya jamii ulivyo na matatizo tunayopitia hawataki kuujuza umma jinsi serikali ya CCM ilivyopoteza dira katika kukidhi matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 11 inayotaja haki na wajibu wa serikali katika kuwalinda raia dhidi ya umasikini wa kipato magonjwa na uzee.
Na ninajua wapo wanasiasa wenye nia nzuri na Taifa kama akina John Mnyika wa CHADEMA, ambaye alithubutu kutaka kuwasilisha Bungeni hoja binafsi kupinga serikali kuzuia mafao ya kujitoa, lakini naomba Mh. John Mnyika ajue kuwa kitendo cha serikali kuondoa zuio la sheria ya mafao hakujatibu matatizo yaliyopo katika mfumo wa hifadhi ya jamii bali kitendo cha serikali kutunga sheria ya kuzuia hayo mafao kulitakiwa kuwa chachu ya kupata fursa ya kuwa na mjadala wa kitaifa wa kuuchunguza na kuuchambua mfumo wetu wa hifadhi ya jamii, kwani wazungu wanasema No smoke without five.

Chonde chonde washikaji tugangamale kuiipinga Deci hii iliyoanzishwa na watawala wa CCM wanaotaka kutekeleza ilani yao kwa kutumia akiba za wananchi ili piramidi lisipindukie kwetu tukaadhirika kwani wahusika hawatakuwepo kipindi tutakapoanza kuayaona madhara ya mchezo wa Deci walioufufua.

Imeandikwa na:
KENNEDY LUFULONDAMA MWANAHARAKATI WA MASUALA YA HIFA
 
kweli ukiwa mjinga utaendelea kuitwa mjinga

Wajinga ni wengi Tanzania,na juzi hapa gazeti la Majira nalo linatoa tahariri ya kuponda fao la kujitoa,hiyo ni haki ya mwajiriwa lazima apewe mara tu anapoona hana ajira ya kudumu ili aweze kujikimu.
 
Pumzika kwa amani mleta uzi, nimesoma kuna thread kuwa umetutoka duniani
 
Acha kabisa ukisema DECi unanitonesha kidonda. Siku za mwisho nilijaribu kuwekae300000 kwa majaribio kumbe ndio lala salama. Yaani we acha tu, niliishia kuilalaani serikali kwani ilikua wapi mpaka wezi hao wakapenya? Watu wa mwanzo walifaidi kweli, hata hivyo aliyenishauri ni mwanamke, na akatokomea acha tu. Basi na washindwe na kidonda kimepoma ila mtoa haha umenitonesha kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kabisa ukisema DECi unanitonesha kidonda. Siku za mwisho nilijaribu kuwekae300000 kwa majaribio kumbe ndio lala salama. Yaani we acha tu, niliishia kuilalaani serikali kwani ilikua wapi mpaka wezi hao wakapenya? Watu wa mwanzo walifaidi kweli, hata hivyo aliyenishauri ni mwanamke, na akatokomea acha tu. Basi na washindwe na kidonda kimepoma ila mtoa haha umenitonesha kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mleta uzi kafariki jana hivyo sio rahisi kujibu tena comments zenu, labda tu mseme R.I.P
 
Wajinga ni wengi Tanzania,na juzi hapa gazeti la Majira nalo linatoa tahariri ya kuponda fao la kujitoa,hiyo ni haki ya mwajiriwa lazima apewe mara tu anapoona hana ajira ya kudumu ili aweze kujikimu.


Mkuu Hivi Fao La Kujitoa Ppf Lipo Na Watu Wanachukua Pesa Zao Sory Kama Unauelewa Kidogo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom