Kessy Wa Kilimanjaro
JF-Expert Member
- Jan 23, 2016
- 327
- 208
Kwenye hoja hii nitatoa aina ya uongozi wa serikali ambao Tanzania inatumia, haswa kiuchumi, na kwanini hiyo aina ya serikali ni chanzo cha matatizo yanayo wapata wananchi na siyo ufumbuzi.
Source:
The World Factbook
Aina ya serikali ambayo Tanzania inatumia ni Unitary Presidential Democratic Republic. Hii inamaanisha kwamba raisi ndiyo mkuu wa serikali na mkuu wa nchi. Hapa unaona tatizo la kwanza na hatua ya kwanza ya hii hoja.
Serikali inampa mtu mmoja nguvu ya kuamua jinsi watu watakavyo ishi maisha yao na hiyo nguvu hamna binadamu anaye stahili kuwa nayo. Msingi wa serikali ni kwamba ina amua kwamba yenyewe, iwe; Mahakama, Bunge, au ofisi ya Raisi ina stahili kuwa na nguvu ya kuendesha maisha ya watu. Kinachotokana na hii nguvu ni kwamba serikali kama ya Tanzania ina miliki mali ya ardhi yote na inazuia uhuru wa kibiashara na fikra.
Nchi yeyote ambayo Rais anapewa nguvu kama aliyopewa Rais wa Tanzania unakuta kwamba Raisi anatumia nguvu hiyo kunwanyasa watu. Raisi anaanza kupitisha sheria za kutoa vitu kwa bure lakini kiukweli hamna kitu duniani ambacho ni bure. Hapa ndipo tutaona tatizo linaanza.
Points.
i. Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inatumia mbinu za Ujamaa (Socialism) na hata mbinu za Communism ambazo zinanyima haki, na uwezo wa uchumi na biashara kukuwa.
ii. Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imenyima Haki za Kumiliki Mali (Private Property Rights) kitu ambacho kinahitajika kukuuza unchumi.
iii. Serikali ya CCM inazuia ubinafsishaji wa ujenzi wa miundombinu ambao sekta ya ubinasishaji ingeweza kujenga vizuri kuliko selikali.
iv. Serikali inanyima haki za uhuru wa kusema (freedom of speech) kwasababu inajua kwamba ikisemwa na kuumbuliwa kwa makosa yake watu wataamka.
Hizi point ndiyo nilizoona muhimu kuongelea.
Kuhusu point ya kwanza kwamba serikali inatumia mbinu za Ujamaa na Ucommunism, na kwamba hizo mbinu zinanyima haki na kuzuia uchumi kukuwa ni kweli. Kwa mfano serikali ya Nyerere ambayo ilimiliki viwanja vyote na kujihusicha na uchumi wa watu binafsi, ilisababisha inflation ipande kwa 30% mwaka 1980. Serikali baada ya miaka 26 baadaye bado haijajifunza. Inajihusisha na biashara kwa kuweka bei ya sukari na kuzuiya sukari kutoka nje kuingia ndani. Ambacho serikali inashindwa kuelewa ni kwamba hiyo sukari ni ya kisasa na East Africa nzima hamna viwanda vinavyo tengeneza hiyo sukari ambayo inahitajika kwenye kutengeneza vinywaji vya kisasa. Sasa hivyo viwanda vinakaribia kufunga ambacho inamaanisha watu watakosa kazi. Pia serikali imefukuza biashara nyingine hapo.
Source:
http://allafrica.com/stories/201603151444.html
Kwenye nchi zote zilizoendelea kwenye sekta ya ubinafsi kuna haki za kumiliki mali na pia uwezo wa kukopa hela. Ukiwa na haki za kumiliki mali, investors wa nje wanaona faida kuja kuinvest kwenye inchi yako. Hivyo ndivyo watu wanavyo weza kupata kazi kutokana na hao investors kuanzinsha kampuni zao hapa na kujenga viwanda. Hizo sekta zinaimarisha ukuwaji wa vibali. Pia kukiwa na private property rights yaani haki za kumiliki mali/viwanja binafsi watu wanaweza kutumia mali zao kupata mikopo na kuanzisha biashara, kitu ambacho kingeweza kukuza ajira na kazi.
Source:
The roundtrip transaction cost is high in Tanzania
Serikali pia inazuia uanzishaji wa biashara na inafanya iwe ngumu kupitia Benki Ya Tanzania. Benki hii imeweka interest rate yani kile unacholipa juu ya deni ulilokopa benki iwe mpaka 12%. Walishawahi kuiweka mpaka 27% na Uchumi ulikufa kabisa. Interest rate ya 12% ina wazuia wale wafanya biashara wadogo uwezo wa kushindana na biashara kubwa kwasababu hawawezi kulipa hiyo interest rate. Ukiongeza na kodi juu ya deni kubwa unaweza kuona jinsi watu wanvyo anza kujenga majengo Tanzania alafu wanashindwa kumaliza. Ukiangalia facts za uchumi kwenye miaka ambayo interest rates zilikuwa chini uchumi ulipanda, lakini uchumi umekuwa hauendi popote pale Benki ilivyo pandisha interest rates mpaka 12%.
Source:
Tanzania Interest Rate | 2002-2016 | Data | Chart | Calendar | Forecast
Kwenye ujenzi wa miundombinu ukimuuliza msoma uchumi yeyote kinacho hitajika siyo serikali kukopa hela kwa wachina au michango ambayo hata haifiki kwenye kazi iliyo tumiwa, lakini ni mashindano ya kampuni binafsi. Serikali ya Tanzania inafanya kazi kama serikali za wacomunist za wachina na Russia ambao walishindwa wao wenyewe kuendesha nchi kwasababu hamna ukuwaji wa GDP kwenye nchi zinazo nyima haki ya kumiliki mali na ubinafsishaji. Hata china unaona walivyo ama kwenda kwenye Capitalism ndiyo nchi ikaanza kukuwa. China kwenye miji yake ilipo ruhusu umiliki wa kibinafsi yani (private property rights), hiyo miji imeendelea. Haswa haswa, kampuni za nje zingeweza kujenga viwanda, barabara, hospitali, shule, madaraja, na kurahisisha usafiri kama serikali ingewaruhusu umiliki, na ingeacha kunyang’anya biashara za watu, na inge binafsisha sekta ya healthcare, sekta ya shule, na sekta ya usafiri, na ya ujenzi, na kuleta kampuni zishindane kwenye kutowa huduma bora hivi vitu visinge kuwa vigali kiasi vilivyo saivi. Hata sekta ya umeme kwenye nchi zilizo endelea ni kampuni binafsi zinashindana kutoa umeme.
Hii source inaonyesha jinsi infrastructure itakavyo jengwa ikibinafsishwa, inaongelea marekani lakini hata tanzania tunaweza tukipata investors.
Encouraging Private Infrastructure Investment
Serikali ambazo zinajali wanachi wao kitu cha kwanza ambacho kinalindwa ni uhuru wa hao wananchi kusema wanachotaka. Haijalishi kama anayesemwa ni Raisi au msafisha choo wa ikulu, wote watasemwa kama nchi ina uhuru. Tanzania ya leo tunaona kwamba hatujafika kiwango hicho cha uhuru. Yani kama Halima Mdee alivyosema bungeni “tumefika kwenye nyakati ambazo Raisi hashikiki”. Na yeyote aliyesoma historia anajua kwamba Raisi akiwa hashikiki kinachofwata ni Udictator (Dictatorship). Raisi angekuwa anasemwa angekuwa anafanya mambo kwa umakini zaidi kwasababu anajua watu wanaangalia kila hatua yake. Sihitaji kusema mengine zaidi kwasababu mmeona magazeti yanafungwa na watu wa Jamiiforums kusakwa, na hata wabunge wengine kuwekwa jela.
Mjadala wangu ni kwamba sekta binafsi pekee ndiyo inaweza kujenga uchumi wetu na siyo serikali. Kama mnahitaji mifano niulizeni. Na kama mnakubali cha kufanya ni kuanzisha hii mijadala madarasani na nyumbani na hata mitaani kuwaamsha watanzania kuhusa swala la uchumi wetu na jinsi serikali inavyo uharibu.