sizzya007
JF-Expert Member
- Mar 15, 2016
- 771
- 2,415
Wajameni, hamna mtu anayelipinga swala vijana kupata kazi na kujishughulisha, hayupo! Isipokuwa na vigumu sana kuamini yanayofanya na serikali ya awamu hii ya tano, mengi yanaonekana yako kisiasa, na hii ni hatari, nchi inaongozwa kwa mihemko ya kisiasa zaidi! Nitatoa mifano ya mambo kadhaa.
Alipoingia madarakani tu, Raisi Magufuli alitembelewa na Prof. Lipumba pale ikulu, Raisi Magufuli akampa Lipumba kazi ya kuandika tathmini ya hali ya uchumi ya nchi, ilitangazwa na wote tukajua, je! Ripoti hiyo tayari Mh. Raisi anayo? Ndio hiyo anayoifanyia kazi? Na kama anayo mbona haikuwekwa katika magazeti ya serikali ili na sisi waajiri wake (wananchi) tupate kuisoma?! Hapa ndio naanza kuyatilia shaka baadhi ya mambo, hili lilifanyika kama tukio la kisiasa zaidi, i believe! Binafsi ningependa nijue hali ya uchumi ya nchi yangu na kwanini tumekuwa tukifanya vibaya gor the last ten years, maana yule mstaafu aliwahi kusema hajui kwanini kaya yake ni maskini, Lipumba angeweza kutoa jibu ambalo wengi tulitamani Raisi wetu mstaafu kulitolea majibu ila alishindwa!
Serikali hii inajinadi kwa kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, ni kauli tamu na nzuri, ila binafsi nilisha kataa kuamini kauli mbiu tamu tamu, waswahili wanasema tamu ni haramu, hapa kazi tu, kazi hizo ni zipi, zimeandaliwa mazingira gani ya kuwa kazi bora?! Sheria za kazi zimebadilishwa?! Kuna sheria kandamizi dhidi ya wafanyakazi, vipi hizi kwanza ziko sawa?! Na vipi viwanda tulivyoambiwa kuwa vitajengwa na ajira tutapewa navyo viko tayari?! Kama lah! Vijana hawa kazi wakazifanyie wapi? Shambani? Sawa! Swala la ruzuku za pembejeo zimetolewa?! Waziri wa kazi anajua nchi yake inaweza kuzalisha ajira ngapi kwa mwaka?
Yakk mengi ambayo yanatakiwa kujibiwa kabla ya kuanza kukurupuka!
Aliyepita kipindi anaingia aliingia hivi, HALI MPYA NGUVU MPYA KASI MPYA.
Baada ya miaka mitano hali ilikuwa mbaya, nguvu ikashuka kabisaaa na kasi ikapungua na kuwa ya kobe.
Akaja tena na HALI ZAIDI NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI, silizungumzi hili, wote tunajua nini kilifuata baada ya hapo (MAJIPU).
Rai yangu (binafsi) kwa serikali hii, ni vizuri zaidi kutatua tatizo moja at a time, Magufuli kuongoza nchi ni kugumu kuliko kuongoza familia, tatua tatizo moja baada ya jingine, HAIWEZEKANI kutatua kila unaloliona tatizo ndani ya mwaka mmoja wa uongozi, ndio maana kuna miaka mi5 ya kuongoza! Ni bora uhangaike na jambo moja kubwa muhimu kwa miaka miwili, na kulilatia ufumbuzi wa kudumu, na tutakukumbuka kwa hilo kuliko kudandia kika tatizo, hapo ndio tutaishi kwa kutumbua majipu tuu bila kusonga mbele, kama uneamua kusafisha ofisi za umma fanya hivyo kwanza na uhakikishe hilo linaisha.
Tujadili.