Serikali ya awamu ya 4 imeboresha Elimu ya Juu

jaba jumah

Senior Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
150
Reaction score
50
Mpango wa maendeleo ya elimu ya juu wa mwaka 2010 umeandaliwa na utekelezaji wake umechangia wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiunga na vyuo vikuu kuongezeka kutoka wanafunzi 34,564 mwaka 2009/2010 hadi wanafunzi 40,452 mwaka 2014/2015 sawa na asilimia 14.6.

utaraibu wa utoaji na urejeshwaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umeboreshwa ambapo;

- Dawati la mikopo limeanzishwa katika kila chuo

- Idadi ya wanafunzi ambao wamepata mikopo imeongezeka kutoka wanafunzi 72,035 mwaka 2009/2010 hadi kufikia 99,928 mwezi machi,2015 sawa na ongezeko la asilimia 27.9

Bajeti kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu imeendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 186.48 mwaka 2010 hadi shilingi bilioni 328.313,44 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 43.2
 
Wanaandaa povu wanakuja wenyewe wanaojifanya wana hati miliki ya elimu Tanzania.
 
Itakuwa imeboresha kwa wana CCM na si watanzania.
 
Mkuu naona unawapa promo ccm maana ukisema imeboresha kwa wana ccm tu ina maana wasomi wote nchi hii ni wana CCM wengine waliobaki na wasio na elimu ni wajinga na malofa! teh teh teh teh think big wewe!
 
JUMA jabah,

..wewe unazungumzia QUANTITY.

..unapaswa kuangalia na QUALITY au UBORA wa elimu ktk awamu hii ya 4.

..sasa hivi viwango vya elimu ya juu vimeshuka kiasi kwamba wahitimu wetu wanashindwa kupambana na ndugu zao wa kenya na uganda ktk soko la ajira.
 
Last edited by a moderator:
Wizi mtupu........hiyo bodi si ya mikopo ni bodi ya zawadi............maana mikopo haiwafikii walengwa kwa asilimia kubwa......mimi hapa ni mhanga wa hiyo taasisi isiyojielewa........sasa wewe kama una ndugu zako mafisadi kwenye system wamekisaidia kupata mkopo hebu tupishe na kelele zako hapa.... ......idiot.
 
Mpango wa maendeleo ya elimu ya juu wa mwaka 2010 umeandaliwa na utekelezaji wake umechangia wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiunga na vyuo vikuu kuongezeka kutoka wanafunzi 34,564 mwaka 2009/2010 hadi wanafunzi 40,452 mwaka 2014/2015 sawa na asilimia 14.6.

utaraibu wa utoaji na urejeshwaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umeboreshwa ambapo;

- Dawati la mikopo limeanzishwa katika kila chuo

- Idadi ya wanafunzi ambao wamepata mikopo imeongezeka kutoka wanafunzi 72,035 mwaka 2009/2010 hadi kufikia 99,928 mwezi machi,2015 sawa na ongezeko la asilimia 27.9

Bajeti kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu imeendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 186.48 mwaka 2010 hadi shilingi bilioni 328.313,44 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 43.2

The heading should be "Serikali ya awamu ya nne "IMEONGEZA" nafasi za elimu ya juu". Kuhusu UBORA ni questionable. Graduates wana vyeti vya degree lakini knowledge ya form 4. Inasikitisha sana watu kujichimbia makaburi halafu wanashangilia. Kushamiri kwa wamachinga leo ni matokeo ya kudharau elimu ya msingi ya "kujitegemea". Nina uhakika miaka 15 ijayo tutakuwa na jeshi la msituni litakalotengenezwa na wenye "degree" wa leo.
 
Itakuwa imeboresha kwa wana CCM na si watanzania.

Wana CCM sıo watanzania?Kwanza naomba raiş ajaye aondoe huu utaratibu wa kitu kinaitwa mkopo wa elimu ya juu.Mikopo itolewe kwenye vyuo vya ufundi tena vya umma na atakayekosa nafasi vya umma ajisomeshe mwenyewe private.Unıversıty ufadhili utolewe kwa vıjana waliofaulu daraja la kwanza tu na mwisho wa sıfa za kujiunga university iwe n dıv 2 lakn wajitegemee gharama.Magraduates wengi wanapunguza nguvu kazi ya taifa kwani wengi hawahusıkı na uzalıshaji.
 
Mpango wa maendeleo ya elimu ya juu wa mwaka 2010 umeandaliwa na utekelezaji wake umechangia wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiunga na vyuo vikuu kuongezeka kutoka wanafunzi 34,564 mwaka 2009/2010 hadi wanafunzi 40,452 mwaka 2014/2015 sawa na asilimia 14.6.

utaraibu wa utoaji na urejeshwaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umeboreshwa ambapo;

- Dawati la mikopo limeanzishwa katika kila chuo

- Idadi ya wanafunzi ambao wamepata mikopo imeongezeka kutoka wanafunzi 72,035 mwaka 2009/2010 hadi kufikia 99,928 mwezi machi,2015 sawa na ongezeko la asilimia 27.9

Bajeti kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu imeendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 186.48 mwaka 2010 hadi shilingi bilioni 328.313,44 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 43.2

Huku ndiko kuboresha elimu? Hizo ni takwimu na zinaendana na ongezeko la wanafunzi, kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi ndiyo kuboresha elimu?
 
Back
Top Bottom