KILIMANI HEWA
Member
- Sep 18, 2015
- 32
- 16
Wapiga kura Wa mtaa Wa Kidimu na Mkombozi, halmashauri ya mji Wa Kibaha tunaiomba serikali ya awamu ya 5 itusaidie kuondoa kero ya muda mrefu ya kivuko/daraja linalounganisha kati ya mitaa tajwa na mtaa Wa mpiji Magohe uliopo wilaya ya kinondoni.
Kero ya kivuko/daraja ni ya muda mrefu ambayo Kwa miaka kadhaa haijapata kiongozi Wa kuitatua kero hiyo licha ya ahadi zinazotolewa na wanasiasa Wa jimbo la Kibaha katika chaguzi zilizopita. Siyo mbunge wetu Samwel Koka wala viongozi Wa mitaa na diwani, wote wameshindwa kutatua kero hiyo.
Kivuko hicho ni muhimu sana kwani ndiyo njia pekee iliyokaribu kutufikisha katika maeneo yanayotoa huduma muhimu za kiafya, elimu na Maji safi. watu wengi wamepoteza maisha Kwa kuliwa na mamba na kusombwa na Maji wanaojaribu kuvuka Maji kwenda upande Wa pili.
Tunaiomba serikali ya Rais Magufuli, ituonee Huruma sisi wapiga kura wake Kwa kututatulia kero hii japo Kwa kutujengea kivuko kidogo. chonde chonde Mzee wetu Magufuli tunaomba utusaidie.