Serikali: Utafiti wa kuwa kuna njaa Tanzania sio kweli, nchi hii haina hata dalili za njaa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Tanzania inasisitiza kwamba haina njaa licha ya utafiti wa hivi karibuni uliotolewa na shirika la Twaweza kuonesha kwamba asilimia 78 ya watu wanakabiliwa na ukosefu wa chakula kuanzia kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Taarifa za utafiti unaonesha kuwepo njaa nchini Tanzania zimekuja katika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukizisaidia nchi ikiwemo za Afrika Mashariki kuanzia Kenya,hadi Ethiopia na Somalia kukabiliana na janga la njaa lililosababishwa na ukame uliozikumba nchi hizo kwa muda.

Hata hivyo Tanzania imeendeleza msimamo wake wa kukanusha kuwepo njaa kama alivyobaini waziri wa kilimo Charles Tizeba. Zaidi sikiliza matangazo yetu ya jioni hii.

Chanzo: DW
 
Tusizoee kuomba omba sana wazee, hivi kila kukicha tunataka kuomba mwisho tutajalipa visivotarajiwa sasa
 
Tanzania inasisitiza kwamba haina njaa licha ya utafiti wa hivi karibuni uliotolewa na shirika la Twaweza kuonesha kwamba asilimia 78 ya watu wanakabiliwa na ukosefu wa chakula kuanzia kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Taarifa za utafiti unaonesha kuwepo njaa nchini Tanzania zimekuja katika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukizisaidia nchi ikiwemo za Afrika Mashariki kuanzia Kenya,hadi Ethiopia na Somalia kukabiliana na janga la njaa lililosababishwa na ukame uliozikumba nchi hizo kwa muda.

Hata hivyo Tanzania imeendeleza msimamo wake wa kukanusha kuwepo njaa kama alivyobaini waziri wa kilimo Charles Tizeba. Zaidi sikiliza matangazo yetu ya jioni hii.

Chanzo: DW
UN kwa vigezo vyao, ambao msingi wake ni tafiti, wamezitangaza nchi za, Yemen, Sudan Kusini, Somalia na Nigeria kuwa ndio nchi zinazokabiliwa na hatari ya baa la njaa....Tanzania si moja wapo....upungufu wa chakula tanzania? upo baadhi ya maeneo...upatikanaji wa vyakula masokoni?...kiwango cha utapiamlo kilichosajiliwa? Jiulize, kisha fanya tafakari....
 
mkuu labda muulize huyo mjumbe, kuna kilicho obvious kama taarifa ya UN juu ya nchi zinazokabiliwa na baa la njaa ,za yemeni, sudan kusini, somalia, na kaskazini mashariki ya nigeria?

Mkuu, mambumbumbu ni nyomi...
 
dah nilimsikiliza uyo tizeba DW, kweli alibore nilitamani nimzibue hata vibao kama angekuwa karibu yangu!!! watu wanaegemea kwenye utafiti tena vyanzo vingine co twaweza peke yao japo at least ktk hili wamesimamia ukweli,bt utafiti ulibase kwa nchi za east Africa &central!!! Kweli Kenya hwe na ukame c uku tukose hata sehemu moja?? jamaa anajibu watu wanaongea siasa,magazeti na mitandao yani wenzao wanazungumzia scientific yy anatakiwa hajibu vile vile kitafiti!! Maana utafiti inajibiwa kwa tafiti!!! yeye anajibu pumba tu!!alaf eti ni Dr!!! yaani kwa staili hii watafiti wakae tu na maquestionair yao ndani!!!nchi imekuwa ya porojo tu
 
Back
Top Bottom