Serikali tupeni ufafanuzi kuhusu shutuma hizi za chama cha JUBILEE

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Chama cha Jubilee nchini kenya kimeishutumu serikali ya Tanzania kwa kuruhusu muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga kufungua kituo mbadala cha kuhesabia kura nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa jubilee , NASA baada ya kunyimwa ruhusa ya kuweka kituo hicho nchini kenya, wameoamua kukihamishia Tanzania, kikiwa na malengo ya kufanya ujumuishaji mbadala wa kura, lakini pia kudukua mifumo ya kuhesabu kura ya tume huru ya uchaguzi nchini kenya.

WOTE tunajua uswahiba wa kiongozi wa NASA na mukuru wa nchi hii, hence

MY TAKE:
Serikali inabidi watoe ufafanuzi kama swla hili ni kweli au la.

Kuingilia uchaguzi na demokrasia ya nchi jirani kwa kuruhusu chama kimoja kutumia nchi yetu kufanya mambo yake ya kiuchaguzi ni kosa kubwa kidemokrasia na kidiplomasia.

lakini pia sisi wenyewe kama nchi hatuamini katika vyama kujijumlishia kura, ndo maana CHADEMA na kile kituo chao tuliwashughulikia, lakini pia Zanzibar uchaguzi ulihairishwa baada ya seif kujijumlishia kura na kutangaza matokeo kabla ya tume

Kama swala hili ni uongo, Jubilee na mwenyekiti wao ambaye ndo Rais wa sasa watuombe msamaha kama nchi kwa kutuingiza katika siasa zao za majitaka
 
Uchaguzi unakuwaga na propaganda nyingi...huwezi kukanusha kila propaganda...UK kupitia balozi wake angeweza kuwasilisha malalamiko kwa Ikulu yetu if this matter is true....
UK as UNITED KINGDOM????????????
 
Uchaguzi unakuwaga na propaganda nyingi...huwezi kukanusha kila propaganda...UK kupitia balozi wake angeweza kuwasilisha malalamiko kwa Ikulu yetu if this matter is true....
Uchaguzi upo Kenya halafu balozi wa UK halete malalamiko?
Uhusiano ni upi.?

Au UK ni Uhuru Kenyatta
 
Uchaguzi unakuwaga na propaganda nyingi...huwezi kukanusha kila propaganda...UK kupitia balozi wake angeweza kuwasilisha malalamiko kwa Ikulu yetu if this matter is true....
Hili ndo jibu mkuu..sidhani km kna cha ziada..
 
Kelele zote former deputy speaker Farah Maalim is sending Aden Duale home come Aug. Order order gentlemen.
 
Kipindi cha Kampeni Propaganda ni nyingi. Hata Marekani walisema Russia walimsaidia Trump kushinda.
 
Chama cha Jubilee nchini kenya kimeishutumu serikali ya Tanzania kwa kuruhusu muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga kufungua kituo mbadala cha kuhesabia kura nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa jubilee , NASA baada ya kunyimwa ruhusa ya kuweka kituo hicho nchini kenya, wameoamua kukihamishia Tanzania, kikiwa na malengo ya kufanya ujumuishaji mbadala wa kura, lakini pia kudukua mifumo ya kuhesabu kura ya tume huru ya uchaguzi nchini kenya.

WOTE tunajua uswahiba wa kiongozi wa NASA na mukuru wa nchi hii, hence

MY TAKE:
Serikali inabidi watoe ufafanuzi kama swla hili ni kweli au la.

Kuingilia uchaguzi na demokrasia ya nchi jirani kwa kuruhusu chama kimoja kutumia nchi yetu kufanya mambo yake ya kiuchaguzi ni kosa kubwa kidemokrasia na kidiplomasia.

lakini pia sisi wenyewe kama nchi hatuamini katika vyama kujijumlishia kura, ndo maana CHADEMA na kile kituo chao tuliwashughulikia, lakini pia Zanzibar uchaguzi ulihairishwa baada ya seif kujijumlishia kura na kutangaza matokeo kabla ya tume

Kama swala hili ni uongo, Jubilee na mwenyekiti wao ambaye ndo Rais wa sasa watuombe msamaha kama nchi kwa kutuingiza katika siasa zao za majitaka
Nawaunga mkono NASA wadhibiti kura zao. Hii tabia mbaya ya vyama tawala kuiba kura dawa yao ndio hii... Yaliyotokea Zanzibar, hapa Tanzania bara ambapo ccm waliingilia mtandao wa NEC kwa kuwa na kituo chao na kuizuia ile ya chadema na hata Uganda ni jibu tosha la kuwa na independent vote count, si kura zako zikiisha ibwa ndo unaanza kulalama na kuonekana km mpiga kelele tu haifai.
Ina maana NASA no matter wataweka wapi kituo lkn ni muhimu pia lazima kuwa nacho.
 
so unaunga mkono kituo chao kuwa TANZANIA???
 
Kwanini JUBILEE wanaogopa NASA kujumlisha kura kwa gharama zao? Ukiona hivyo JUBILEE wamepanga kugushi matokeo ndio maana hawataki akina Odinga wayajumlishe. Kama JUBILEE wangekuwa wasafi wasingeogopa ujumlishaji kura. Hata CCM waliwakataza UKAWA kujumlisha kura kwa kuwa walikuwa na njama za kuiba kura, jambo ambalo lilifanikiwa baada ya kukifunga kituo cha kujumlisha matokeo cha UKAWA.
 
Hamna kitu ila serikali ya Kenya wanaelewa kuwa Raila Odinga ni rafiki ya Rais Magufuli hiyo ndiyo inaleta mashaka kidogo.
 
Achen kugombanisha TZ na nchi majirani. Juzi nmemuona UK kabla ya hotuba akiwaomba Wakenya wasimame kuomboleza klcho tokea Tz. Plz, let's stop hypocrisy.
 
Wakenya wasituletee ujinga wao tena wasituzoee kabisa,tunajua wakenya wanaongoza kwa umbea na kutunga uongo ndiyo maana waliweza kupigana 2007 kutokana na ujinga huo.
 
Raila akishinda (God forbid) itakua EA inaongozwa na kundi la washkaji. Raila ni best wa JPM kitambo. JPM ni besti na M7 na PK. Itabaki tu PN ambae nae sio ngumu kumleta kundini.
 
so is that a strong reason for him not to be elected
 
Back
Top Bottom