Mimi naomba kuiuliza serikali yetu iniambie makanisa haya yanayotoza kodi ya asilimia 10 ya mapato ya wafuasi wake, je sheria gani ya nchi inawaruhusu?
Mimi nilidhani kwa mujibu wa sheria Serikali pekee kwa kutumia TRA ndiyo inayoruhusiwa kukusanya kodi.
Au tuelimishwe hii kusema watu watoe asilimia kumi ya mapato yao ni kitu gani kama sio kodi?
Kimsingi kwa wale wanaofuatilia historia maisha ya mwanandamu yana historia ndefu.
Huko nyuma miungu ilifanya kila kitu katika maisha ya wanandamu ambacho unaona kinahusika na serikali. Miungu ndiyo ilikuwa mahakama ikitoa hukumu katika jamii. Ilikuwa ukituhumiwa basi unapelekwa sehemu inaulizwa mizimu wakitegemea kupata ishara kujua kama kweli umekosa au la. Yapo mambo yaliwekewa sheria moja kwa moja na ukituhumiwa moja kwa moja unapewa hukumu zilizotoka kwa mizimu wakiogopa mikosi au kukosea mbele ya miungu.
Miungu hiyo ndiyo ilichagua viongozi, watawala walichaguliwa na mizimu na ikikukataa basi na ikikubali basi. Mizimu ilikuwa inaweka vikwazo kiwa baadhi ya koo na kuziita za mikosi na kuziteua baadhi kuwa ndizo zenye baraka.
Kimsingi mambo yote unayoona yakifanyika leo kuhusu serikali au kufanywa na serikali yalifanywa na miungu.
Lakini wanadamu walibaini hila zilizokuwa zikifanyika na kuachana na tamamduni hizo na kuanza kufanya mambo haya wenyewe lakini bado yapo mambo ambayo yameendelezwa hadi leo kwa kuwa yana maslahi kwa baadhi ya wanadamu.
Moja ya mambo yaliyoendelezwa ni miungu kutoza kodi.
Ushauri wangu kwa serikali kama ambavyo tuliona Mwalimu Nyerere akichukua maamuzi ya kijasiri ya kupiga marufuku Wafalme basi leo hii tunategemea serikali zetu kupiga marufuku taasisi za dini kutoza kodi.
Tusiwaache baadhi ya watu kutake advantage ya watu wenye matatizo na hawajui suluhisho kudaiwa kodi kwa kigezo cha kutatuliwa matatizo yao na muumba wakati sote tunashuhudia watoza kodi hao wakizitumia kuishi maisha ya anasa na huku masikini hawa wakiendelea kutaabika.
Tujiulize hivi kinachoendelea makanisani kweli ni kumtolea mungu matoleo au ni utapeli kupitia maandiko? mfano mtu ana shida anaambiwa ili mungu akutatulie shida zako unatakiwa kutokumwibia mungu na yeye alisema utoe Fungu la kumi yaani asilimia 10 ya mapato yako.
wapo wanadamu wengi wana matatizo na hawajui suluhisho, wapo wenye magonjwa, masikini, matatizo ya kijamii ambao wanakumbana na watu hawa wanaofanya kazi kisheria katika nchi zao na baada ya kukusanya hizi asilimia kumi inaonyesha watoaji matatizo yao yanabaki palepale au yanaongezeka lakini hawa wakusanyaji ndio hutajirika na mali hizi.
je ni kwanini serikali hazioni uwezekano wa kuwepo mchezo katika hili na kulisimamia?