Serikali pigeni marufuku hizi local betting machine za kichina zitawamaliza vijana.

Manofu

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
1,317
2,019
Niwasalimu ndugu zangu asa wale walipa kodi wazuri kupitia vinywaji vigumu( hard drinks) na vinywaji nusu vigumu kama bia yani ( semi-hard). Back to the topic kuna machine za kamali za kichina sijui ndo zinaitwa bonanza? Ayseee hzi zitamaliza vijana wetu yani unakuta bodaboda kashinda anaangaika juani kutafta pesa jioni ikiingia labda kakusanya elfu thelathini na kwa bosi wake ajarejesha anakwenda kwenye bonanza ili azalishe japo elfu kumi li machine linameza zote pyuuu yani ndani ya dakika mbili au tatu dude linatafna pesa ambayo mtu kashinda anaiangaikia siku nzima.

Kuna wale wanapata mshahara mwisho wa mwezi, yani benki account ndo imesoma mwisho wa mwezi mtu anaenda kutoa pesa nusu ya mshahara wake kuja kucheza haya madude ili azalishe nusu saa ni nyingi laki mbili kamili kwishineyi.

Kuna watu walikuwa wameanzisha ujenzi wa nyumba zao kwa kasi sana ilikuwa wanaelekea hatua ya kuezeka lkn toka haya madude yamekuja awajawai kuzidi walipo ishia, tafadhali serikali ingilieni ili swala vinginevyo vijana wataishia kuwa walevi na mateja maana akishaliwa pesa yake anatfta jinsi ya kujiliwaza anaishia kubugia viroba vya pombe.

Lakini pia it would be wise kama wamiliki wa haua madude mtawatoza kodi nzito nzito ili wapate ugumu wakulipa wayaludishe kwao au walipe ili serikali nayo inufaike kuliko kuona mtu tena wakigeni anakusanya mamilioni ya pesa kila siku uku wanachi wakiteseka kwa kupoteza vipato vyao.

N.B Do not try it at home or any where.
 
Hiyo midude inameza hela za watu sana
Nimewahi cheza 200 tu tena nilipita mtu kanila jaribu nikajaribu ikaenda
 
Kuna jamaa alipokea mshahara akaenda kwenye hiyo mashine dah, 150 ikaondoka hivi hivi.
 
Back
Top Bottom