Serikali ondoeni Mabango katikati ya Barabara

Chamoto

Platinum Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
9,883
Reaction score
22,305
Mabango katikati ya barabara ni hatari

Usalama barabarani ni jambo kubwa na la msingi katika maendeleo ya nchi yetu. Moja ya vitu ambavyo vinaweza kuleta ajali barabarani ni vizingiti vinavyo mfanya dereva ashindwe kuona vizuri mbele.

Katika kipindi cha miaka ya nyuma, kumekuwa na ongezeko kubwa sana la mabango makubwa ya kutanganza biashara katikati ya barabara. Yapo Dar es salaam, Dododma, Mwanza n.k, unakuta dude kubwa tuu mbele yako linakuvuta macho uliangalie badala ya unakokwenda, hovyo kabisa. Barabara zinatakiwa ziwe wazi ili dereva aweze kuona mbali zaidi anakokwenda.

Serikali inabidi iyaondoe kabisa mabango yaliyo katikati mwa barabara ilikuongeza usalama kwa wananchi. Nchi zote zilizo endelea zina sheria kali za kuzuia mabango ya kibiashara katikati mwa barabara. Serikali inashindwa vipi kuzuia hili? Naelewa huko nyuma kulikuwa na rushwa na mambo mengi yalikuwa yanaenda kiholela lakini kwa awamu hii ya kutetea wanyonge nini kinashindikana?

 
Kuna bango la matangazo/billboard lilikua Mwanza roundabout ya pale Jengo la CCM mkoa (Imalaseko). Aisee ikifika usiku linaumiza macho balaa yaani kama una-drive unaweza kuvaa miwani ya giza ili upite pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…