St Lunatics
JF-Expert Member
- Aug 29, 2015
- 6,644
- 11,166
Vitu viwili Watanzania hawavipendi ni Ukweli na Kukosolewa. Tokea kupata uhuru Tanzania inapata misaada kutoka mataifa ya nje lakini maendeleo yapo machache sana. Hela nyingi huishia mifukoni mwa wakubwa na familia zao baada ya kwenda kwenye lengo halisia. Utakuta kuna misaada ya maji safi kwa kila Mtanzania lakini jiji kama la Dar halina maji achilia vijijini. Utasikia misaada ya Umeme nchi nzima lakini kila siku kuna mgao kila kona ya Tanzania hii. Utasikia kuna misaada ya Barabara lakini foleni kila barabara ya Tanzania hii. Misaada ni mengi imetolewa na Nchi kama America,Uingereza,China,Sweden,Norway na nyengine nyingi tu za Ulaya,Asia na Bara la America. Achilia misaada kuna mikopo inayotolewa na Serikali inayoiomba kwenye Benki za Kimataifa. Suali la kuiuliza serikali yetu tuna zaidi ya miaka 50 ya Uhuru ni lini tutaweza kujitegemea wenyewe? Tuna rasilimali nyingi tu nchini zinatusaidia nini sisi wenye nchi? Ikiwa bajeti ya Serikali tunasaidiwa kwa miaka 50 hivi kweli tutaweza kujisaidia wenyewe kwa kipindi cha miaka 10? Hebu tuangalie maendeleo yalioletwa na Misaada na maendeleo yalioletwa na Serikali yetu yapi yanamshinda mwenzake? Ukweli ni kwamba tatizo sio misaada bali tatizo ni mfumo wa serikali yetu na utendaji wake wote. Huwezi kwenda kuowa na ukapewa mke lakini bado unategemea baba mkwe ndio akuletee msaada wa chakula,maji nguo na hela ya familia. Au ukamlea mtoto akamaliza chuo akapata kazi na mshahara lakini bado anategemea kula kwa mzee.