Serikali na watumishi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali na watumishi wake

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by NURFUS, Jun 14, 2012.

 1. N

  NURFUS Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yoyote ile ni kama baba kwa watumishi wake, ila pale serikali inapokuwa au inapofanya kitu ambacho pengine kila mtu anakuwa na maswali, hii inampa mtu maswali kwamba hivi ni kweli kwamba serikali inaweza kuwa kama baba kwa watumishi wake. Mfano hivi sasa serikali inaendelea na mchakato wa kuandaa/ ama kufanya maandalizi ya sensa kwa wananchi wake.

  Na kama inavyojulikana, hii ni kazi ambayo kila mtu angependa kuifanya ili kwa namna nyingine aweze kuingiza kipato mbali na mshahara wake wa kawaida. Sasa katika kuilona hili, serikali imeamua kutafuta mtenda ili aweze kufanya kazi ambayo kwa mtazamo wa kaiwada kabisa ingeweza kufanywa na watoto wake,ambao ni waajiri wake. Kuna hawa watu wanaosoma kitu kinachohusu masuala mazima ya kuhamasisha jamii juu ya mambo ya maendele.

  Maafisa maendeleo ya jamii, na sijui kama serikali inajua kuwa watu hawa katika ngazi nyingi serikalini hawana kazi za maana wanazofanya, utawakuta wamekaa tu ofisini mwao toka asubuhi mpaka muda wa kutoka,na sio kweli wakati mwingine kuwa hawana kazi bali ni upungufu mkubwa wa bajeti ili hawa jamaa waweze kutekeleza kazi zao na hivyo kujikuta kwa kiasi kikubwa wapo iddle tu bila kazi na hii kuwafanya maisha yao yaendelee kuwa magumu.

  Sasa hivi inaingia akilini kweli kwa serikali hii kutafuta mtu wa kufanya uhamasishaji masuala ya sensa. Hili kamwe haliwezi ingia akilini kwa serikali yetu hii ambayo tunaamini ni makini. Sasa hawa watumishi wako uliowaajiri kwa kazi hii wafanye nini kama unaamua kumtu mtu kwa tenda.
   
Loading...