Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,653
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezimungu muumba wa vyote,pia niwape hongera wanajukwaa kwa michango mbalimbali ya kuelimisha,kufikirisha ingawaje wengine hukereka kwa baadhi ya maoni ya watu bali tubakie kuvumiliana.
Kwakuanza na mada yangu ya leo nizungumzie wapinza na serikali katika siasa za Tanzania.Wanasiasa kama wanavyotuaminisha sisis raia nikwamba lengo lao kubwa nikila chama kishike dola ili kuboresha maisha/mahitaji ya wananchi wake.
Serikali naomba iwatazame au kuwachukulia wapinzani kama milango ya fahamu,hii nikwasababu milango ya fahamu katika mwili wa binadamu huwa na matumizi na manufaa mbalimbali hususan yaliyochanya.Macho hutumika kuona,masikio kusikia,ulimi kuonja,pua hunusa,ngozi huhisi na ulimi kuonja.Mtu ambaye milango yote ya fahamu inafanya kazi vizuri hupokea hisia haraka na hatimaye aamue kufanyiakazi hisia hizo au aamue kuacha.
Wakati huu ambao serikali inapambana na wahujumu uchumi almaarufu MAJIPU basi isiwatupe mbali wapinzani badalayake iwatumie kama jicho lake kuona waovu,kama sikio kusikilizia wapi penye tatizo,kama ulimi kuonja maeneo yenye ukakasi katika utendaji,kama ngozi kupokea hisia niwapi wahujumu wametegesha mitego yao na kam pua kunusa maeneo ambayo yana viashiria vya kila namna yakulitendea taifa visivyo.Nimeyasema hayo sina maana kwamba ndani ya serikali hawapo wanaoweza kubaini hayo,bali ninaamini awaye nje pembeni tena mbali pia huweza kuona kwa usahihi
Nimtazamo wangu kwamba serikali na apinzani nilazima;wasikilizane,wategemeane,washauriane,wabebane,waathiriane.Kwakuzingatia ukweli huo nikwamba malumbano kama yale ya bungeni yasiyokua na muafaka nilazima yafike mahali yakome.Haiwezekani mambo yaende mrama wakati kuna wazee,viongozi wa dini na serikali pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani na chama tawala
Nimalize kwa kusema kuwasikiliza wengine,kuapatia mrejesho aidha hasi au chanya,kuwavumilia maudhi yao na kuupokea ukweli utokao kwa wengine nijambo jema nalisilo epukika katika dunia hii jumuishi.Hata hiyo milango ya fahamu huleta na au kupokea taarifa nzuri,zakawaida,mbaya na zinazokera lakini hakuna awaye yeyote akasema pua yake ikatwe kwakua inanusa harufu mbaya,au macho yanaona yale yasiyompendeza,masikio kusikia makelele au ngozi kuhisi muwasho,joto au baridi.Hakuna aliyedai akatwe ulimi kisa akila pilipili au chumvi inamuwasha.HIVYO HATA TUSIOWAPENDA YAPO MEMA YATOKAYO KATIKA MIOYO NA VINYWA VYAO
Ninashukuru kwa kutimiza wajibu wa kuisemea nchi yangu.