Serikali na Shirika la Posta

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Salamu zikufikie wewe Serikali kwa huyo mtoto wako SHIRIKA LA POSTA TANZANIA. Hivi hili shirika bado halina mawazo ya kuboresha miundombinu yake kiofisi, kiutendaji na kupanuka nchi nzima maana naona kama mmekariri biashara hivi.

USHAURI: Naomba mpanue shughuli zenu za kitendaji ziende na kufika mpaka ngazi ya kijiji, kata ndipo mziunganishe kwenye wilaya, mikoa na makao yenu makuu. Watu wanapenda kutumia Shirika la Posta kusafirisha vifurushi vyao kutoka Mjini kwenda Vijijini au kinyume chake.

Nawaomba mbadilike kiutendaji na mboreshe miundombinu yenu ofisi gani za SHIRIKA kubwa ndani ya nchi kwenye ofisi zenu kwa nje na ndani hakuna uzuri wowote mazingira ya hovyo kabisa na muache kufanya kazi kwa mazoea bwana.

Jengeni ofisi katika Vijiji na Kata bwana sio mtu hata kutuma barua tu asafiri Kilometa nyingi kwenda wilayani au mkoani kupata huduma haipendezi. Yaani tangu Mwalimu Nyerere aweke ofisi hizo mwaka 1980 mpaka leo sioni mabadiliko yanayoendana na ukuaji wa kimaendeleo nchini.

MAENDELEO NI YETU SOTE, TANZANIA NI YAKO BADILIKA.
 
Back
Top Bottom